Wasiojulikana wamtisha Maguire kuwa aondoke Man United ndani ya saa 72 au auliwe

Wasiojulikana wamtisha Maguire kuwa aondoke Man United ndani ya saa 72 au auliwe

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Beki wa Manchester United, Harry Maguire alipewa vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana walipomwambia wanampa saa 72 ajiondoe klabuni hapo au asubiri kifo kwa kulipuliwa na bomu.

Ujumbe huo ulitumwa kwake kwa njia ya barua pepe wakati akiwa mazoezini baada ya United kufungwa mabao 4-0 na Liverpool, ambapo watu hao walimwambia wametegesha mabomu matatu nyumbani kwake na kumtaka afanye vile walivyomuagiza.

Polisi walifika na mbwa wenye mafunzo ya mabomu nyumbani kwa mchezaji huyo kufanya uchunguzia lakini hawakupata chochote. Mchumba wa beki huyo, Fern Hawkins na mabinti zao wawili walihama kwa muda kwenda sehemu salama na ulinzi umeongezwa kwa familia ya Maguire

Inaelezwa kuwa Maguire yupo kwenye mchakato wa kuongeza kamera maalum za CCTV na kuweka ulinzi kwa saa 24 kila siku.

Source: The Sun
 
Huyo Maguire aondoke tu kwani ndio miongoni mwa wachezaji wabovu sana katika klabu ya Manchester United hafai na hana msaada wowote kwa timu.
 
Huyo Maguire aondoke tu kwani ndio miongoni mwa wachezaji wabovu sana katika klabu ya Manchester United hafai na hana msaada wowote kwa timu.
Mbona Leo hajacheza na Man Utd imechezea 3 - 1 kwa Arsenal. Wanamwonea bure Mkuu.
 
Arsenal 3 –1 Manchester United
Yule Maguire ni bonge moja la beki ila man u kuna shida kwenye kuwa control na kuwa train wachezaji haiwezekani yule jese lingard alikuwa tishio alipokuwa west ham leo hii karudi man u amekuwa kiazi wa mwisho kabisa.
 
Mbona Leo hajacheza na Man Utd imechezea 3 - 1 kwa Arsenal. Wanamwonea bure Mkuu.
Kuna post yangu moja humu nimetaja baadhi ya wachezaji na yeye akiwemo, yaani hawafai hata bure.

Manchester United need a major team overhaul if they're to claim their lost glory.
 
wanamuonea tu.ila na yeye aelewiki wakati mwingine ,kuna mechi aliinua mkono kumuita refa kwa mpira alioshika mchezaji wa timu yake[emoji22][emoji28]
 
Back
Top Bottom