Ngoja mie nichangie kama niko Bungeni vile:
1. Kwa kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi, na
2. Kwa kuwa wanatakiwa kuwa wamechaguliwa na wananchi, na
3. Kwa hiyo inapaswa Wabunge wachaguliwe moja kwa moja na wananchi.
Wabunge wa viti maalum ufutwe, hauhitajiki. Pia ubunge kwa kuteuliwa na Rais ufutwe(hapa wamo Sophia Simba, Makamba , Kingunge etc). Hii ni mizigo tu kwa walipa kodi, na hawamuwakilishi yeyote. Ni deal za kupeana ulaji tu.
4. Kwa kuwa mbunge mmoja anamgharimu mlipa kodi kiasi kikubwa sana kwa matumizi yakwe (mbunge), idadi ya majimbo ingepunguzwa hadi yabaki 150 tu. Hii ukiongeza wale 5 kutoka Baraza la wawakilishi Z'bar na Attorney General, tuwe na Wabunge 156 tu. Hawa wanatosha sana tu.
Kifupi ni kuwa wabunge ambao ni wapambe wa mafisadi EL na RA ndio wang'olewe (Wakiwemo wenyewe EL na RA) pamoja na wezi wenzao akina Chenge, na wapambe wao akina Makamba, Kingunge, Mahanga etc.,
Naomba kuwasilisha...