Pre GE2025 Wasira awatetemesha akina Tundu Lissu na Wenzake: "Kauli Mbiu ya "No Reform, No Election" Haina Maana Kwa Sasa"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stevin Wasira, amesema kauli mbiu ya "No Reform, No Election" haina maana yoyote kwa sasa, akisisitiza kuwa muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria umekwisha kutokana na uchaguzi mkuu kukaribia.
1737795778316.png

Akizungumza leo, Januari 23, 2025, jijini Dodoma, Wasira alieleza kuwa badala ya kushikilia kauli hiyo, CHADEMA wanapaswa kushiriki uchaguzi na kuhakikisha wanakubaliana na maridhiano yaliyopo.

"Kauli ya 'No Reform, No Election' haina nafasi kwa sasa. Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wameonyesha utayari wa mazungumzo, na bunge linakaribia kuvunjwa, hivyo hakuna muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria yanayohitaji muda mrefu," alisema Wasira.

Aliongeza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaotarajiwa kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani, unapaswa kuwa nafasi ya vyama vyote kushindana kwa hoja badala ya kutafuta visingizio.

Wasira aliwataka viongozi wa CHADEMA kutumia nafasi za mazungumzo zilizopo badala ya kusimamia misimamo isiyotekelezeka kwa wakati huu. "Ni muhimu kushiriki uchaguzi na kuwa sehemu ya demokrasia badala ya kupoteza muda na kauli ambazo hazina tija kwa wananchi," alisisitiza.
 
View attachment 3213528

Ukweli mtupu tena usio na mawaa hata kidogo 🐒
 
Kwani Wasira si alisema hakuna maridhiano na CHADEMA, sasa mbona anayataka. Hii Nchi ni yetu wote tatizo Hawa viongozi wanadhani ni mali yao.
Maridhiano siyo na CHADEMA pekee. Kama CHADEMA hawataki Maridhiano, shauri yao
 
Back
Top Bottom