Mkosa Kabila
New Member
- Mar 22, 2025
- 1
- 5
View: https://www.instagram.com/reel/DHvHL1bOb01/?igsh=azBpMGl4d2VlbW4z
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Stephen Wasira amesema hakuna Mtu wala Chama cha Siasa chenye uwezo wa kuzuia Uchanguzi Mkuu wa Mwaka 2025 usifanyike na kuwataka Watanzania kuwapuuza Viongozi wa Vyama vya siasa vinavyowahadaa kuhusiana na Uchanguzi na badala yake kuendelea kufanya Maandalizi ya kushiriki haki yao ya Kikatiba ya Kuchagua au kuchaguliwa.
"Ibara ya 41 ya Katiba ya Tanzania inasema hakuna mtu anayeweza kuahirisha Uchanguzi wa Tanzania ila unaweza kuahirishwa kama kuna vita,niwaombe Watanzania msiwasilize hao Viongozi wa CHADEMA wanaopotosha Umma uchanguzi ulikwisha anza tangu zamani,"amesema Wasira.
Sambamba na hili Wasira amesikitishwa na Kitendo cha mmoja wa Kada wa CHADEMA kupigwa baada ya kuonekana hakubaliani na Viongozi wa Chama hicho kuhusiana na Msimamo wake wa kushiriki Uchaguzi mkuu, kwani imeonesha hawana ukomavu wa kisiasa.