Pre GE2025 Wasira: Lissu aje, tufanye Mdahalo halafu Watanzania waamue, adai CHADEMA kwasasa imekatika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Nani awe Mwamuzi wa mnyukano huu?

Mzee Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, amemwita mezani Tundu Lissu kufanya mdahalo ili Watanzania waweze kutoa maoni yao na kufanya maamuzi bora katika uchaguzi ujao.

"Lissu sio size ya Rais, Lissu ni mdogo na Rais ni mtu mzito sana. Niliwahi kufanya majadiliano na Lissu pale Blue Pearl Dar es salaam yeye akiwa na Lipumba mwisho akaishia kukimbia. Kama anataka aje afanye Mdahalo na mimi, najua hawezi ataishia kukimbia tu"

Your browser is not able to display this video.
 
Wakuu

Mzee Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, amemwita mezani Tundu Lissu kufanya mdahalo ili Watanzania waweze kutoa maoni yao na kufanya maamuzi bora katika uchaguzi ujao.

View attachment 3225342
Kwani anagombea wasira? Anaposema kuwa watanzania wafanye maamuzi katika uchagu ujao, kwani anagombea lisu na wasira? Mbona kama huyu mzee kaanguka mdahalo hata kabla hawajaingia ulingoni?
 
Nimeandika ,,nikafuta ,nimeandika tena nikafuta.

Ila mzee wangemuacha tu apumzike , hizi mbilinge mbilinge hazimfai kwa umri wake
 
Ataumbuliwa saa 1:00 asubuhi
 
Nimeandika ,,nikafuta ,nimeandika tena nikafuta.

Ila mzee wangemuacha tu apumzike , hizi mbilinge mbilinge hazimfai kwa umri wake
Hata hivyo, jamaa ni chuma cha pua. Majority ya wazee wa umri wake wamebaki na akili inayolingana na ya mtoto wa miaka 6!
 
Kwanza mdahalo kuhusu nini? Na Kwa nini yeye amejiteua kufanya mdahalo na Lissu?

Huo mdahalo lengo lake ni nini, Halafu wananchi wataamua kwa kutumia kigezo gani na hayo maamuzi yatapimwaje?
 
Hata hivyo, jamaa ni chuma cha pua. Majority ya wazee wa umri wake wamebaki na akili inayolingana na ya mtoto wa miaka 6!
Lifestyle... Hao unanaosema wamebakia na akili za mtoto wa miaka 6, maisha yamewapiga.

Kwa miaka 60 ya maisha yake Wassira hajawahi kutoka kwenye kundi la wateule wachache wanaokula mema ya nchi hii.
 
Huyu mzee kikongwe anataka umaarufu kupitia Lisu, apuuzwe tu.
Lisu sio size yake
 
Anamtaka Lisu yeye kama nani? Aombe mjahalo na Heche!!
 
HUyo babu hana hadhi ya kufanya mdahalo na lisu wamlete hangaya wasira tutampa sugu au ntobi achuane naye
 
Itapendeza sanaaaaaaa

Lissu akubali umuone... inaonekana Mzee nae ana maneno maana yupo tayari 😂😂😂 supaaaaa

Kazi iendeleeeee...
🗣️🗣️🗣️🗣️🗣️
 
Tundu Lisu vs. Stephen Wasira a.k.a Pono usingizi😂🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…