PreGE2025 Wasira: Martha Karua kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, aende DRC au ashughulikie matatizo ya Kenya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Tanzania hatuvurugi amani ya Afrika Mashariki isipokuwa tunaendesha mambo yetu kwa amani na salamu ninazompatia Mwanasheria Martha Karua ni kwamba aache kujipima na CCM, CCM ni chama kikubwa Afrika kinachoanza na nyumba kumi," alisema.

Aliongeza kuwa "CCM haina hofu na chama chochote lakini hatuwezi kuingilia kazi ya Mahakama na hatuwezi kuingilia shughuli za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwa ni vyombo vyenye mamlaka, lakini kama ni mjuzi ashughulike na mambo ya Kenya."

Kulingana na Wasira aliyekuwa akizungumza hayo huku akishangiliwa na umma, alisema kama anaona chama chake ni kidogo na anataka umaarufu basi aangalie mataifa mengine ya Afrika yenye migogoro akatatue.

"Akishindwa arudi nyumbani akaendeshe chama chake ambacho sera zake hazijulikani. Atuache Tanzania tuchaguane kwa utaratibu wetu hata mwenyewe na zungumza hapa nilichaguliwa kwa kishindo katika nafasi hii ndani ya Chama, naamini dozi hii inamtosha," amesema

Alisema katika uchaguzi uliopita Kenya, Martha alikuwa mgombea Mwenza wa Raila Odinga, walikuwa wanalalamikia uamuzi wa tume yao ya uhaguzi walienda hadi 'Supreme Cort (Mahakama ya juu), lakini hawakupata kitu akaenda Mahakama ya Afrika Mashariki na alitoka patupu.

"Kama alitoka patupu amuache Lissu na kesi yake matokeo yatapatikana na yeye atayakubali kama alivyokuyakubali yale ya Kenya," alieleza.

Wakati Wasira anamjibu mwanasheria huyo wa Kenya alisema Chama kinamheshimu kwa kuwai ni mtu wa Afrika Mashariki, pia kinaheshimu taaluma yake ya sheria.

Martha ni Mwenyekiti wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP) cha Kenya.

“Anahaki kama mwanasheria kama ameitwa na watu wanaoshtakiwa, sasa pale kuna 'katatizo' tuna Polisi, Mahakama na Tundu Lissu. Sasa Polisi wakikukuta umekosea hawaendi kwa Wasira kusema kwamba umekosea wao wamesomeshwa kujua kama umekosea, wakikuchukua hawaruhusiwi kukaa na wewe muda mrefu.

“Wanakuambia ukae ikifika saa 24 uwe umeshafika mahakamani kwa sababu kwa mujibu wa katiba, Mahakama ndicho chombo cha kikatiba cha kutoa haki hapa nchini, sasa polisi walimkuta Lissu wakamchukua...

“Lakini hapa duniani imewekwa mahakama ndicho chombo kinachotoa haki, hatuingilii kukiamrisha, na sasa Martha Karua mwanasheria aliebobea anajua mgawanyo wa mamlaka kwamba ukiwa na mahakama Rais hawezi kuingilia mahakama.

“Anajua mahakama peke yake ndiyo inaweza kuamua mtu kakosea au hajakosea na sheria inasema mtu hawezi kuhesabiwa kosa mpaka mahakama imuone ana kosa kwa hiyo hatujui kama anakosa ama laa, polisi ndio wanajua na Mahakama ndio imepelekewa.” alisisitiza.

Akifafanua zaidi Wasira alisema Lissu angekuwa hana kosa wangemuachia na juzi walimkamata mwingine anaitwa Heche (John Heche ambaye ni Makamu MwenyekitiwaChadema) Bara, lakini wakamshikilia kwa muda wakamuachia.

"Na sisi Chama Cha Mapinduzi na serikali tuliyoiunda kwa idhini ya Watanzania hatuingilii Mahakama, tunaiachia Mahakama ifanye kazi yake hatuiambii imuachie au imfunge Martha Karua anajua hayo mambo lakini kaja anaseama anakofia mbili.

"Moja ni mwanasheria tukasema hiyo kofia tunaiheshimu aende Kisutu kwa wanasheria wenzake, lakini akasema kofia ya pili ni mwenyekiti wa chama kwa hiyo ana uhuru na anasema CCM inaiogopa CHADEMA ndio maana inawakamata ili ishinde uchaguzi.

"Martha nataka nimuambie asikie na wanaompelekea habari kwamba nimesema hapa Tanzania kwa mwaka huu hakuna chama kinaweza kukishinda CCM, chama gani? Maana ukienda mahali ugenini ni vizuri ukajua mambo ya hapo kabla hujalalamika.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini inawaonea Chadema.

"CHADEMA waliambiwa Aprili 12 waende wakatie saini masharti ya maadili ambayo walishapelekewa siku nyingi wao ndio walikataa kwenda lazima waanzishe zogo ili magazeti wapate cha kuandika, wakakataa kwenda sasa kama wao wana uwezo washauriane na tume sisi CCM tunawangoja.

"Tume ikikubali tuko tayari waje tumejipanga vizuri na watashindwa kama walivyoshindwa sertikali za mitaa, na safari hii anasema Martha Karua kwa nini hatiuzungumzi nao, nani anakataa kuzungumza nao? CCM hatuogopi," alisema.

Hata hivyo alisema demokrasia ya kuchochea watu wagome uchaguzi ni kupinga haki za wengi kwa sababu wengi wanataka kupiga kura lakini CHADEMA inadai kuwa na haki ya kuzuia hivyo alihoji hiyo ni demokrasia?
 
WASIRA AMTAHADHARISHA MARTHA KARUA WA KENYA KUJIPIMA UBAVU NA CCM.

Asema kama anajiona anaweza kutatua migogoro aende nchi nyingine za Afrika

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amemjia juu Mwanasheria maarufu na mwanasiasa wa nchini Kenya Martha Karua, ambaye amekuja nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, anayekabiliwa na tuhuma za uhaini na kuchapisha picha za uongo mtandaoni.

Wasira amemtaka mwanasheria huyo kuacha kujipima uzito na Chama Cha Mapinduzi huku akimwambia pia kuwa Chama kinaheshimu mamlaka ya Mahakama na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Amesisitiza kama Karua anajiona anaweza kushughulika na migoro basi atatue matatizo yaliyoko nchini kwake au mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza mbele ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma Leo Aprili 25, 2025 , akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuelezea faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Wasira alitumia nafasi hiyo kumjibu Karua hatua kwa hatua na kumtaka aache kuingilia mambo asiyoyajua vizuri.

“Tanzania hatuvurugi amani ya Afrika Mashariki isipokuwa tunaendesha mambo yetu kwa amani na salamu ninazompatia Mwanasheria Martha Karua ni kwamba aache kujipima na CCM, CCM ni chama kikubwa Afrika kinachoanza na nyumba kumi," alisema.

Aliongeza kuwa "CCM haina hofu na chama chochote lakini hatuwezi kuingilia kazi ya Mahakama na hatuwezi kuingilia shughuli za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwa ni vyombo vyenye mamlaka, lakini kama ni mjuzi ashughulike na mambo ya Kenya."

"Akishindwa arudi nyumbani akaendeshe chama chake ambacho sera zake hazijulikani. Atuache Tanzania tuchaguane kwa utaratibu wetu hata mwenyewe na zungumza hapa nilichaguliwa kwa kishindo katika nafasi hii ndani ya Chama, naamini dozi hii inamtosha," amesema

Wakati Wasira anamjibu mwanasheria huyo wa Kenya alisema Chama kinamheshimu kwa kuwa ni mtu wa Afrika Mashariki, pia kinaheshimu taaluma yake ya sheria.

Martha ni Mwenyekiti wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP) cha Kenya.

“Anahaki kama mwanasheria kama ameitwa na watu wanaoshtakiwa, sasa pale kuna 'katatizo' tuna Polisi, Mahakama na Tundu Lissu. Sasa Polisi wakikukuta umekosea hawaendi kwa Wasira kusema kwamba umekosea wao wamesomeshwa kujua kama umekosea, wakikuchukua hawaruhusiwi kukaa na wewe muda mrefu.

===
 
Attachments

  • IMG-20250425-WA1632.jpg
    IMG-20250425-WA1632.jpg
    315.2 KB · Views: 39
  • IMG-20250425-WA1638.jpg
    IMG-20250425-WA1638.jpg
    504.2 KB · Views: 41
  • IMG-20250425-WA1634.jpg
    IMG-20250425-WA1634.jpg
    588.8 KB · Views: 36
  • IMG-20250425-WA1636.jpg
    IMG-20250425-WA1636.jpg
    631.4 KB · Views: 39
  • IMG-20250425-WA1640.jpg
    IMG-20250425-WA1640.jpg
    372.7 KB · Views: 48
  • IMG-20250425-WA1644.jpg
    IMG-20250425-WA1644.jpg
    707.7 KB · Views: 44
  • IMG-20250425-WA1646.jpg
    IMG-20250425-WA1646.jpg
    830.6 KB · Views: 42
  • IMG-20250425-WA1648.jpg
    IMG-20250425-WA1648.jpg
    500.6 KB · Views: 43
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira, amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

“Kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, basi aende DRC au ashughulikie matatizo ya nchini kwake. Aache kuleta siasa za mtaani hapa. Tanzania tuna mfumo wa sheria unaofanya kazi,” amesema Wasira mbele ya umati wa wananchi.
Gari ni injini sio bodi 😂😂😂😂…. Wasira asijifananishe na iron lady Martha Karua!! Maana hata huyo mwenyekiti wake hampati Karua hata kwa robo!!
Huyu mama alipambana na Moi pamoja na makucha yake mwisho wa siku waliiangusha KANU!

Namkumbuka Martha siku tulienda Kenya na Team ya Mkapa kusuluhisha mgogoro wao alimtukana Mkapa kama mtoto!! 😂😂
 
WASIRA AMTAHADHARISHA MARTHA KARUA WA KENYA KUJIPIMA UBAVU NA CCM.

Asema kama anajiona anaweza kutatua migogoro aende nchi nyingine za Afrika

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amemjia juu Mwanasheria maarufu na mwanasiasa wa nchini Kenya Martha Karua, ambaye amekuja nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, anayekabiliwa na tuhuma za uhaini na kuchapisha picha za uongo mtandaoni.

Wasira amemtaka mwanasheria huyo kuacha kujipima uzito na Chama Cha Mapinduzi huku akimwambia pia kuwa Chama kinaheshimu mamlaka ya Mahakama na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Amesisitiza kama Karua anajiona anaweza kushughulika na migoro basi atatue matatizo yaliyoko nchini kwake au mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza mbele ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma Leo Aprili 25, 2025 , akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuelezea faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Wasira alitumia nafasi hiyo kumjibu Karua hatua kwa hatua na kumtaka aache kuingilia mambo asiyoyajua vizuri.

“Tanzania hatuvurugi amani ya Afrika Mashariki isipokuwa tunaendesha mambo yetu kwa amani na salamu ninazompatia Mwanasheria Martha Karua ni kwamba aache kujipima na CCM, CCM ni chama kikubwa Afrika kinachoanza na nyumba kumi," alisema.

Aliongeza kuwa "CCM haina hofu na chama chochote lakini hatuwezi kuingilia kazi ya Mahakama na hatuwezi kuingilia shughuli za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwa ni vyombo vyenye mamlaka, lakini kama ni mjuzi ashughulike na mambo ya Kenya."

"Akishindwa arudi nyumbani akaendeshe chama chake ambacho sera zake hazijulikani. Atuache Tanzania tuchaguane kwa utaratibu wetu hata mwenyewe na zungumza hapa nilichaguliwa kwa kishindo katika nafasi hii ndani ya Chama, naamini dozi hii inamtosha," amesema

Wakati Wasira anamjibu mwanasheria huyo wa Kenya alisema Chama kinamheshimu kwa kuwa ni mtu wa Afrika Mashariki, pia kinaheshimu taaluma yake ya sheria.

Martha ni Mwenyekiti wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP) cha Kenya.

“Anahaki kama mwanasheria kama ameitwa na watu wanaoshtakiwa, sasa pale kuna 'katatizo' tuna Polisi, Mahakama na Tundu Lissu. Sasa Polisi wakikukuta umekosea hawaendi kwa Wasira kusema kwamba umekosea wao wamesomeshwa kujua kama umekosea, wakikuchukua hawaruhusiwi kukaa na wewe muda mrefu.

===
😂
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira, amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

“Kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, basi aende DRC au ashughulikie matatizo ya nchini kwake. Aache kuleta siasa za mtaani hapa. Tanzania tuna mfumo wa sheria unaofanya kazi,” amesema Wasira mbele ya umati wa wananchi.
Matha Karua, Iron lady of Kenya, ni mwanasiasa mropokaji tu ambae hakubaliki kabisa hadi kwenye eneo bunge lake huko Kenya, mara zote karibu kila uchaguzi hushindwa vibaya sana na wadada wadogo hata kwenye county yake tu ya Kirinyaga.

Huwezi amini hata MCA wake tu ambae huku kwetu nadhani ni kama diwani, anatoka chama kingine ambacho sio chake. Kiujumla ni mwanasiasa asie kubalika licha ya unafiki wa kujifanya anatetea sana wanasiasa wa nje ya Kenya.

Ni furaha iliyoje,
Makamu mwenyekiti wa CCM taifa amempa makavu yake live bila kusubiri afike Kenya 🐒
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira, amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, basi aende DRC au ashughulikie matatizo ya nchini kwake. Aache kuleta siasa za mtaani hapa. Tanzania tuna mfumo wa sheria unaofanya kazi,” amesema Wasira mbele ya umati wa wananchi.

Sahihi nakubali ,inatakiwa apewe kichapo au akamatwe awe deported.

By the way nani alimpa permit ya kuja 🇹🇿?
 
Sahihi Martha Kalua akamalize kwanza ukabila Kenya atakumbukwa milele kama akiweza
Aache kuruka ruka kama bisi zikikaangwq kwenye chungu

Martha Karua tupe timeline ya kumaliza ukabila nchini kwako Kenya kwanza lini mtaumaliza?

Una kazi kubwa ya kufanya Kenya kuliko Tanzania
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira, amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, basi aende DRC au ashughulikie matatizo ya nchini kwake. Aache kuleta siasa za mtaani hapa. Tanzania tuna mfumo wa sheria unaofanya kazi,” amesema Wasira mbele ya umati wa wananchi.

Huyu Baba anazeeka hadi akili
Ccm wana laana.
 
Back
Top Bottom