PreGE2025 Wasira: Martha Karua kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, aende DRC au ashughulikie matatizo ya Kenya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira, amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, basi aende DRC au ashughulikie matatizo ya nchini kwake. Aache kuleta siasa za mtaani hapa. Tanzania tuna mfumo wa sheria unaofanya kazi,” amesema Wasira mbele ya umati wa wananchi.

OUTDATED POLITICIAN
 
Kabla kujadili mtu kama Martha Kalua vizuri umjue kwanza kabla kulaumu wengine
Nafahamu tu kuwa ni mmoja wa wasomi wazuri tu.

Tarehe 10 April alitoa mhadhara pale chuo kikuu cha Howard, Washington DC na nikahudhuria.

Alikuwa akichambua kitabu chake cha "Against The Tide".

Sasa sifahamu kama mzee Wassira hadi umri wake wa sasa kisiasa na kibinadamu kama ameandika kitabu chochote.
 
Wakiona kichwa hicho na uso kama tako la Samia?
downloadfile-4.jpg
 
Gari ni injini sio bodi 😂😂😂😂…. Wasira asijifananishe na iron lady Martha Karua!! Maana hata huyo mwenyekiti wake hampati Karua hata kwa robo!!
Huyu mama alipambana na Moi pamoja na makucha yake mwisho wa siku waliiangusha KANU!

Namkumbuka Martha siku tulienda Kenya na Team ya Mkapa kusuluhisha mgogoro wao alimtukana Mkapa kama mtoto!! 😂😂
Alijiuzulu kutoka serikali ya Moi.

Pia aliwahi kusimama na kuondoka Moi akiwa anahutubia.
 
Wasira asimamie tume huru iwepo asije kulia kama hivi.
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira, amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, basi aende DRC au ashughulikie matatizo ya nchini kwake. Aache kuleta siasa za mtaani hapa. Tanzania tuna mfumo wa sheria unaofanya kazi,” amesema Wasira mbele ya umati wa wananchi.

Sema huyu mzee angezaliwa pwani angekuwa bingwa wa mipasho.
 
Gari ni injini sio bodi 😂😂😂😂…. Wasira asijifananishe na iron lady Martha Karua!! Maana hata huyo mwenyekiti wake hampati Karua hata kwa robo!!
Huyu mama alipambana na Moi pamoja na makucha yake mwisho wa siku waliiangusha KANU!

Namkumbuka Martha siku tulienda Kenya na Team ya Mkapa kusuluhisha mgogoro wao alimtukana Mkapa kama mtoto!! 😂😂
Hii inatosha kumfahamu ni mtu wa Namna gani, anashida asaidiwe aisee.
 
Nafahamu tu kuwa ni mmoja wa wasomi wazuri tu.

Tarehe 10 April alitoa mhadhara pale chuo kikuu cha Howard, Washington DC na nikahudhuria.

Alikuwa akichambua kitabu chake cha "Against The Tide".

Sasa sifahamu kama mzee Wassira hadi umri wake wa sasa kisiasa na kibinadamu kama ameandika kitabu chochote.
unataka kusemaje?
 
Back
Top Bottom