PreGE2025 Wasira: Martha Karua kama anadhani anaweza kushughulika na migogoro, aende DRC au ashughulikie matatizo ya Kenya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Gari ni injini sio bodi 😂😂😂😂…. Wasira asijifananishe na iron lady Martha Karua!! Maana hata huyo mwenyekiti wake hampati Karua hata kwa robo!!
Huyu mama alipambana na Moi pamoja na makucha yake mwisho wa siku waliiangusha KANU!

Namkumbuka Martha siku tulienda Kenya na Team ya Mkapa kusuluhisha mgogoro wao alimtukana Mkapa kama mtoto!! 😂😂
Kama ni mpambanaji apambanie mambo yao ya Kenya sio kuleta pua yake Tanzania. Halafu wewe mngese ulifurahia Mkapa kutukanwa?
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Tanzania hatuvurugi amani ya Afrika Mashariki isipokuwa tunaendesha mambo yetu kwa amani na salamu ninazompatia Mwanasheria Martha Karua ni kwamba aache kujipima na CCM, CCM ni chama kikubwa Afrika kinachoanza na nyumba kumi," alisema.

Aliongeza kuwa "CCM haina hofu na chama chochote lakini hatuwezi kuingilia kazi ya Mahakama na hatuwezi kuingilia shughuli za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwa ni vyombo vyenye mamlaka, lakini kama ni mjuzi ashughulike na mambo ya Kenya."

Kulingana na Wasira aliyekuwa akizungumza hayo huku akishangiliwa na umma, alisema kama anaona chama chake ni kidogo na anataka umaarufu basi aangalie mataifa mengine ya Afrika yenye migogoro akatatue.

"Akishindwa arudi nyumbani akaendeshe chama chake ambacho sera zake hazijulikani. Atuache Tanzania tuchaguane kwa utaratibu wetu hata mwenyewe na zungumza hapa nilichaguliwa kwa kishindo katika nafasi hii ndani ya Chama, naamini dozi hii inamtosha," amesema

Alisema katika uchaguzi uliopita Kenya, Martha alikuwa mgombea Mwenza wa Raila Odinga, walikuwa wanalalamikia uamuzi wa tume yao ya uhaguzi walienda hadi 'Supreme Cort (Mahakama ya juu), lakini hawakupata kitu akaenda Mahakama ya Afrika Mashariki na alitoka patupu.

"Kama alitoka patupu amuache Lissu na kesi yake matokeo yatapatikana na yeye atayakubali kama alivyokuyakubali yale ya Kenya," alieleza.

Wakati Wasira anamjibu mwanasheria huyo wa Kenya alisema Chama kinamheshimu kwa kuwai ni mtu wa Afrika Mashariki, pia kinaheshimu taaluma yake ya sheria.

Martha ni Mwenyekiti wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP) cha Kenya.

“Anahaki kama mwanasheria kama ameitwa na watu wanaoshtakiwa, sasa pale kuna 'katatizo' tuna Polisi, Mahakama na Tundu Lissu. Sasa Polisi wakikukuta umekosea hawaendi kwa Wasira kusema kwamba umekosea wao wamesomeshwa kujua kama umekosea, wakikuchukua hawaruhusiwi kukaa na wewe muda mrefu.

“Wanakuambia ukae ikifika saa 24 uwe umeshafika mahakamani kwa sababu kwa mujibu wa katiba, Mahakama ndicho chombo cha kikatiba cha kutoa haki hapa nchini, sasa polisi walimkuta Lissu wakamchukua...

“Lakini hapa duniani imewekwa mahakama ndicho chombo kinachotoa haki, hatuingilii kukiamrisha, na sasa Martha Karua mwanasheria aliebobea anajua mgawanyo wa mamlaka kwamba ukiwa na mahakama Rais hawezi kuingilia mahakama.

“Anajua mahakama peke yake ndiyo inaweza kuamua mtu kakosea au hajakosea na sheria inasema mtu hawezi kuhesabiwa kosa mpaka mahakama imuone ana kosa kwa hiyo hatujui kama anakosa ama laa, polisi ndio wanajua na Mahakama ndio imepelekewa.” alisisitiza.

Akifafanua zaidi Wasira alisema Lissu angekuwa hana kosa wangemuachia na juzi walimkamata mwingine anaitwa Heche (John Heche ambaye ni Makamu MwenyekitiwaChadema) Bara, lakini wakamshikilia kwa muda wakamuachia.

"Na sisi Chama Cha Mapinduzi na serikali tuliyoiunda kwa idhini ya Watanzania hatuingilii Mahakama, tunaiachia Mahakama ifanye kazi yake hatuiambii imuachie au imfunge Martha Karua anajua hayo mambo lakini kaja anaseama anakofia mbili.

"Moja ni mwanasheria tukasema hiyo kofia tunaiheshimu aende Kisutu kwa wanasheria wenzake, lakini akasema kofia ya pili ni mwenyekiti wa chama kwa hiyo ana uhuru na anasema CCM inaiogopa CHADEMA ndio maana inawakamata ili ishinde uchaguzi.

"Martha nataka nimuambie asikie na wanaompelekea habari kwamba nimesema hapa Tanzania kwa mwaka huu hakuna chama kinaweza kukishinda CCM, chama gani? Maana ukienda mahali ugenini ni vizuri ukajua mambo ya hapo kabla hujalalamika.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini inawaonea Chadema.

"CHADEMA waliambiwa Aprili 12 waende wakatie saini masharti ya maadili ambayo walishapelekewa siku nyingi wao ndio walikataa kwenda lazima waanzishe zogo ili magazeti wapate cha kuandika, wakakataa kwenda sasa kama wao wana uwezo washauriane na tume sisi CCM tunawangoja.

"Tume ikikubali tuko tayari waje tumejipanga vizuri na watashindwa kama walivyoshindwa sertikali za mitaa, na safari hii anasema Martha Karua kwa nini hatiuzungumzi nao, nani anakataa kuzungumza nao? CCM hatuogopi," alisema.

Hata hivyo alisema demokrasia ya kuchochea watu wagome uchaguzi ni kupinga haki za wengi kwa sababu wengi wanataka kupiga kura lakini CHADEMA inadai kuwa na haki ya kuzuia hivyo alihoji hiyo ni demokrasia?
Hii sasa ndiyo siasa ..Kama vyombo vya dola vitakaa pembeni wanasiasa wakaanza kusumbuana na maneno kama hivi nchi itakuwa nzuri sana

Kusema ukweli nimependa maneno ya Wasira...Na wangeachwa wapambane ki hivi Kisha wananchi wachague nani mshindi ingekuwa vyede sana
 
Sokwe mtu
 
Kweli hili zee jinga sana yaani linajipambanisha na martha?
 
Kama ni mpambanaji apambanie mambo yao ya Kenya sio kuleta pua yake Tanzania. Halafu wewe mngese ulifurahia Mkapa kutukanwa?
Kenya ukabika mno ukiongozwa na kabila lake la wakikuyu amalize hilo kwanza

Watanzania sio saizi yake yuko chini mno
 
Kama vyombo vya dola vitakaa pembeni wanasiasa wakaanza kusumbuana na maneno kama hivi nchi itakuwa nzuri sana
Kenya hapo tu vyombo vya dola vilikaa pembeni wakaachia wanasiasa matokeo waliuana kikabila hadi kuzalisha wakimbizi wa ndani

Hadi mahakama ya kimataifa ya ICC ikaingilia kati na Kenya baada ya kuona nchi haitawaliki wakamuomba Raisi Kikwete akasaidie usuluhishi

Vyombo vya dola vikikaa pembeni ni hatari kwa amani na usalama wa nchi

Juzi tu hapa kenya hapo vyombo vya usalama vilikaa pembeni kuachia wanasiasa Gen z wakachoma maduka,kuvamia jengo la bunge na kuteketekeza jengo la mahakama kuu na uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kufungwa utalii kusimama,biashara, kusimama nk

Kwa taarifa yako kwa Tanzania hilo halipo na haliji kutokea jipangeni kufanya siasa safi huku vyombo vya dola vikiwazunguka na bunduki ,virungu na mabomu

Mkichemka tu jiandaeni kuuawa,kutiwa vilema nk na polisi hilo wala sio siri
 
Namkumbuka Martha siku tulienda Kenya na Team ya Mkapa kusuluhisha mgogoro wao alimtukana Mkapa kama mtoto!! 😂😂
Baadaye wenyewe wakikuja kumpigia magoti Raisi Kikwete awasuluhishe kusaidia kumaliza hiyo migogoro yao Kenya

Huyu Martha Karua mwambieni Tanzania sio saizi yake kabisa

Kwa Tanzania ni mdogo sana kana kidonge cha piriton
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira amemkosoa vikali mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini," amesema.

Akizungumza Aprili 25, 2025 jijini Dodoma, Wasira amesema Karua ameletwa nchini kama wakili wa utetezi lakini ametumia nafasi hiyo kuingilia uhuru wa Mahakama na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jambo ambalo ni kinyume na misingi ya sheria na utawala bora.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Tanzania hatuvurugi amani ya Afrika Mashariki isipokuwa tunaendesha mambo yetu kwa amani na salamu ninazompatia Mwanasheria Martha Karua ni kwamba aache kujipima na CCM, CCM ni chama kikubwa Afrika kinachoanza na nyumba kumi," alisema.

Aliongeza kuwa "CCM haina hofu na chama chochote lakini hatuwezi kuingilia kazi ya Mahakama na hatuwezi kuingilia shughuli za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwa ni vyombo vyenye mamlaka, lakini kama ni mjuzi ashughulike na mambo ya Kenya."

Kulingana na Wasira aliyekuwa akizungumza hayo huku akishangiliwa na umma, alisema kama anaona chama chake ni kidogo na anataka umaarufu basi aangalie mataifa mengine ya Afrika yenye migogoro akatatue.

"Akishindwa arudi nyumbani akaendeshe chama chake ambacho sera zake hazijulikani. Atuache Tanzania tuchaguane kwa utaratibu wetu hata mwenyewe na zungumza hapa nilichaguliwa kwa kishindo katika nafasi hii ndani ya Chama, naamini dozi hii inamtosha," amesema

Alisema katika uchaguzi uliopita Kenya, Martha alikuwa mgombea Mwenza wa Raila Odinga, walikuwa wanalalamikia uamuzi wa tume yao ya uhaguzi walienda hadi 'Supreme Cort (Mahakama ya juu), lakini hawakupata kitu akaenda Mahakama ya Afrika Mashariki na alitoka patupu.

"Kama alitoka patupu amuache Lissu na kesi yake matokeo yatapatikana na yeye atayakubali kama alivyokuyakubali yale ya Kenya," alieleza.

Wakati Wasira anamjibu mwanasheria huyo wa Kenya alisema Chama kinamheshimu kwa kuwai ni mtu wa Afrika Mashariki, pia kinaheshimu taaluma yake ya sheria.

Martha ni Mwenyekiti wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP) cha Kenya.

“Anahaki kama mwanasheria kama ameitwa na watu wanaoshtakiwa, sasa pale kuna 'katatizo' tuna Polisi, Mahakama na Tundu Lissu. Sasa Polisi wakikukuta umekosea hawaendi kwa Wasira kusema kwamba umekosea wao wamesomeshwa kujua kama umekosea, wakikuchukua hawaruhusiwi kukaa na wewe muda mrefu.

“Wanakuambia ukae ikifika saa 24 uwe umeshafika mahakamani kwa sababu kwa mujibu wa katiba, Mahakama ndicho chombo cha kikatiba cha kutoa haki hapa nchini, sasa polisi walimkuta Lissu wakamchukua...

“Lakini hapa duniani imewekwa mahakama ndicho chombo kinachotoa haki, hatuingilii kukiamrisha, na sasa Martha Karua mwanasheria aliebobea anajua mgawanyo wa mamlaka kwamba ukiwa na mahakama Rais hawezi kuingilia mahakama.

“Anajua mahakama peke yake ndiyo inaweza kuamua mtu kakosea au hajakosea na sheria inasema mtu hawezi kuhesabiwa kosa mpaka mahakama imuone ana kosa kwa hiyo hatujui kama anakosa ama laa, polisi ndio wanajua na Mahakama ndio imepelekewa.” alisisitiza.

Akifafanua zaidi Wasira alisema Lissu angekuwa hana kosa wangemuachia na juzi walimkamata mwingine anaitwa Heche (John Heche ambaye ni Makamu MwenyekitiwaChadema) Bara, lakini wakamshikilia kwa muda wakamuachia.

"Na sisi Chama Cha Mapinduzi na serikali tuliyoiunda kwa idhini ya Watanzania hatuingilii Mahakama, tunaiachia Mahakama ifanye kazi yake hatuiambii imuachie au imfunge Martha Karua anajua hayo mambo lakini kaja anaseama anakofia mbili.

"Moja ni mwanasheria tukasema hiyo kofia tunaiheshimu aende Kisutu kwa wanasheria wenzake, lakini akasema kofia ya pili ni mwenyekiti wa chama kwa hiyo ana uhuru na anasema CCM inaiogopa CHADEMA ndio maana inawakamata ili ishinde uchaguzi.

"Martha nataka nimuambie asikie na wanaompelekea habari kwamba nimesema hapa Tanzania kwa mwaka huu hakuna chama kinaweza kukishinda CCM, chama gani? Maana ukienda mahali ugenini ni vizuri ukajua mambo ya hapo kabla hujalalamika.

"Yeye amefika tu na ndege mara anasema CCM inaiogopa CHADEMA, chama chenyewe cha kuogopa wao wenyewe wameshagawanyika sijui kuna G55 wanatafuta chama cha kwenda anailaumu tume anasema kwa nini inawaonea Chadema.

"CHADEMA waliambiwa Aprili 12 waende wakatie saini masharti ya maadili ambayo walishapelekewa siku nyingi wao ndio walikataa kwenda lazima waanzishe zogo ili magazeti wapate cha kuandika, wakakataa kwenda sasa kama wao wana uwezo washauriane na tume sisi CCM tunawangoja.

"Tume ikikubali tuko tayari waje tumejipanga vizuri na watashindwa kama walivyoshindwa sertikali za mitaa, na safari hii anasema Martha Karua kwa nini hatiuzungumzi nao, nani anakataa kuzungumza nao? CCM hatuogopi," alisema.

Hata hivyo alisema demokrasia ya kuchochea watu wagome uchaguzi ni kupinga haki za wengi kwa sababu wengi wanataka kupiga kura lakini CHADEMA inadai kuwa na haki ya kuzuia hivyo alihoji hiyo ni demokrasia?
Nashauri Karua asijibu hili kokoro kwa sababu siyo size yake mbali na kuchakatwa aka recycled.
 
Huyu Mzee simwelewagi kabisa.

Nikimwona naona nakwazika sijui kwa nini? Nilianza kumwona kipindi cha Kikwete.
 
Hili zee likumbushwe kuwa kwa umri wake tayari lipo fainali. Ni umri ambao wenzake wanaojitambua wameshamrudia Mungu na wanajitahidi kulea wajukuu zao kwa maadili na ucha Mungu. Lenyewe ndo kwanza linatumia nusu saa nzima jukwaani kuongea upumbavu likifahamu kabisa linayoyazungumza ni kinyume na uhalisia, eti hatuingilii mahakama, polisi, tume 'huru'... Pumbavu!
 
unataka kusemaje?
Mzee Wassira hajachelewa kuandika vitabu angalau viwili.

Na kwa kuwa alisomea applied economics, basi angasaidia sana kuandika vitabu kuhusu kunyanyua sekta ya kilimo kiwe cha kisasa na kiinue uchumi wa wakulima khasa wale wadogowadogo.

Au angeandika kitabu kinohusu uchumi wa gigi au "Gig economy" kwa wajasiliamali wadogo kutoa mbinu mbalimbali za biashara za aina hiyo.

What is Gig Economy- segment of service economy based on temporary or flexible jobs, often evolving connecting clients and customers through online economy ( Investopedia, 2024).
 
Back
Top Bottom