4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 11,613
- 13,543
Uyu mzee Wasira ,unajikuta unacheka kijinga ,kweli nimeamini mtu mzima akizeeka hurudi utotoni.Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amemjibu Kiongozi Mstaafu wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kuwa CCM haibishani na CHADEMA kwa kuwa iliwaambia wazungumze wakajibu hawako tayari kupotezewa muda.
Pia, Wasira ametumia nafasi hiyo kuwaambia CHADEMA wajitokeze hadharani wawaambie wanataka nini na kama wanashindwa kuiambia CCM basi waiambie Tume.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza Leo machi 30 2025 katika mkutano wa hadhara mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Wasira alitumia nafasi hiyo kumjibu Zitto Kabwe ambaye akiwa Lindi alisema Wasira anajua historia hivyo kwa nini anabishana na CHADEMA badala ya kuzungumza.
“Mimi niliwaambia tuzungumze Tundu Lissu akasema tutawapotezea muda, sasa mtu ana muda wake na hataki upotee wewe umlazimishe kupoteza muda wake wa nini? Kwa hiyo sisi tunawaambia wakiwa na jambo linazungumzika na linawezekana waje tuzungumze.
Mzee wasira anaswaga za kitoto aisee ,ccm imepatwa na jua