Kuna mchezo unachezwa hapa!
Media zimetishiwa na pia bahasha za kadi ili habari za kina kutoandikwa
Kiongozi wa Ngome ya vijana wa upinzani Tanzania atupwa ufukweni baada ya kutekwa nyara
2 Desemba 2024
Image: ACT Wazalendo
Kiongozi wa ngome ya vijana wa upinzani Tanzania ACT Wazalendo, Abdul Nondo amepatikana baada ya kutupwa ufukweni, chini ya siku moja baada ya kuripotiwa kutekwa nyara katika jiji kuu la Dar es Salaam.
Chama chake, ACT Wazalendo, kinasema Nondo alipigwa na kujeruhiwa vibaya na amelazwa hospitalini.
Naibu Mwenyekiti wa chama hicho, Isihaka Mchinjita, alisema Nondo amezibwa macho na kushambuliwa mara kwa mara huku akitishiwa kuuawa.
Polisi wametoa taarifa kuthibitisha kisa hicho katika ufukwe wa Coco beach Oysterbay jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili usiku, wakisema wanachunguza kisa hicho.
Walisema alikuwa ametelekezwa ufukweni na watekaji wake na aliomba msaada kwa mwendesha teksi ya pikipiki bodaboda , ambaye alimpeleka katika ofisi za chama.
āKutoka hapo viongozi wa chama walimkimbiza hospitalini kwa matibabu. Tunachunguza na tutachukua hatua za kisheria,ā msemaji wa polisi David Misime alisema Jumatatu asubuhi.
Baada ya kumtembelea hospitalini, Mchinjita alisema katika taarifa yake ya awali saa 7 usiku , kwamba Nondo alipigwa "muda mrefu" kabla ya kutupwa ufukweni ambako watekaji "walimvua kitambaa machoni na kumpiga. pinguā.
"Nondo alisema waliomteka nyara walimtisha na kumuonya kwamba wakimkamata tena, hawatamuokoa maisha yake," aliongeza. Sababu ya kutekwa nyara kwake haijabainika.
Siku ya Jumapili, ACT Wazalendo kilisema Abdul Nondo alinyakuliwa dakika chache baada ya kuwasili kutoka eneo la Magharibi mwa nchi la Kigoma ambako alikuwa akiwapigia kampeni wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa mitaa uliofanyika wiki iliyopita uliogubikwa na utata kiasi kuitwa uchafuzi wa uchaguzi wa TAMISEMI 2024
.
Alikuwa amechukuliwa kutoka kituo cha basi jijini Dar es Salaam alfajiri ya Jumapili na watu wawili waliokuwa wakisafiri kwa gari jeupe la magurudumu manne.
Polisi sasa wanasema uchunguzi unaendelea ili kubaini washukiwa na kubaini nia yao.
Tukio hili linafuatia kutekwa nyara na kuuawa kwa kiongozi mwandamizi kutoka chama kikuu cha upinzani CHADEMA mwezi Septemba 2024.
Katika utekaji wa kiongozi mwandamizi, Ali Mohamed Kibao wa CHADEMA alitolewa kwenye basi na kupigwa kisha kumwagiwa tindikali. Rais Samia Suluhu Hassan alikemea tukio hilo na kutaka uchunguzi wa mauaji hayo ufanyike.
Chanzo: BBC