Wasomaji wa Biblia Kwanini shetani hakumgusa mke wa Ayubu

Inanna

Member
Joined
Jul 8, 2024
Posts
39
Reaction score
96
Wanatheolojia wa jf, baada ya kupitia kitabu cha Ayubu kilicho andikwa mambo mengi ambayo shetani alimtendea Ayubu kama majaribu.

Kama ilivyo andikwa shetani alirdhuru mifugo,wajakazi,utajiri,watoto na zaidi afya ya Ayubu mwenyewe ,ila mke wake yeye tu alikua safe, wanasema Kila kitu na sababu hapo imekaaje wajuzi.
 
Alimtumia kwa kumwambia amtukane Mungu ili afe!
 
Shetani anafanya kazi yake kwa malengo na mikakati. Anajua nani amfanyie nini na kwa namna gani ili amwangushe.

Si ajabu alimwendea Kristu jangwani akiwa amefunga siku 40 mchana na usiku, lakini akashindwa pia.

Tageti hapa ilikuwa ni Ayubu kwa sababu ndiye alikuwa mwakilishi wa Mungu kiroho na kitabia, tofauti na mkewe ambaye alikuwa mguu pande, mguu sawa.

Ingekuwa rahisi zaidi kummaliza Ayubu kupitia mtu wake wa karibu zaidi - mkewe. Japo pia akashindwa! Mungu atukuzwe milele amina!

Maana jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lile lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (1Kor 10:13).
 
Umemaliza,awe tuu mbishi kama Thomas!
 
Kitabu hakikubainisha ukaribu wa mke wa Ayubu na Mungu.

Angekuwa kwenye viwango vya utumishi vya Ayubu, angesifiwa. Najaribu kusema mke wa Ayubu alikuwa wa shetani tayari😅

Ama tunaweza sema tu tamaduni za kiyahudi zinabagua wanawake na hivyo hata miungu yao ilikuwa na muelekeo huo huo, miungu si inatengenezwa na watu tu?
 
Wanatheolojia wa jf, baada ya kupitia kitabu cha Ayubu kilicho andikwa mambo mengi ambayo shetani alimtendea Ayubu kama majaribu.
Kama ilivyo andikwa shetani alirdhuru mifugo,wajakazi,utajiri,watoto na zaidi afya ya Ayubu mwenyewe ,ila mke wake yeye tu alikua safe, wanasema Kila kitu na sababu hapo imekaaje wajuzi.
Sasa kama mwanamke n nyoka na nyoka n shetan sasa atamgusaje shetan mwezie wakat wote n Wa moja
 
(Ayubu 2:9)
Mke wa Ayubu akasema: Makufuru Mungu ufe.

Ndipo utajua shetani alimwacha Ili aje kuwa silaha ya mwisho.

Lakini pia ujue, shetani alikatazwa na Mungu kugusa uhai wa Ayubu, mke wa Ayubu ni sehemu ya uhai wa Ayubu sababu ni mwili mmoja, ndio sababu hakuguswa.
 
Wanatheolojia wa jf, baada ya kupitia kitabu cha Ayubu kilicho andikwa mambo mengi ambayo shetani alimtendea Ayubu kama majaribu.
Kama ilivyo andikwa shetani alirdhuru mifugo,wajakazi,utajiri,watoto na zaidi afya ya Ayubu mwenyewe ,ila mke wake yeye tu alikua safe, wanasema Kila kitu na sababu hapo imekaaje wajuzi.
Shetani siku zote hahangaiki na wale wote walio kwenye zizi lake never. Hao ni mali yake tayari. Anahangaika na wale wasio kwenye himaya yake.

Hata hivyo hatuwezi kusema hakuguswa. Aliathiriwa moja kwa moja. Madhara aliyopata mume yalimuumiza moja kwa moja yeye pia. Fikiria mali zote zilipotezwa na kurudi kwenye umaskini wa kutupwa. Unaweza sema hakuguswa? Watoto wote walikufa, je unafikiri hakuguswa? Mumewe aliyempenda alipata ugonjwa wa ajabu wakiwa na hali mbaya kiuchumi unafikiri hakuguswa?

Kuna pindi alimwambia mumewe mtukane Mungu ufe. Unafikiri ni sababu zipi zilifanya atoe kauli hiyo? Tayari alikuwa amekata tamaa ya maisha kuliko hata Ayubu, alikuwa amechoka na umaskini, alikuwa amechoka kumuuguza Ayubu katika hali ya umaskini. Tayari alikuwa na depression na ndio maana uwezo wa kufikri ulipungua kiasi kwamba alikuwa tayari kufa.
Sisi tulio na ndoa mke akiumwa mume unakuwa mgonjwa mara dufu kuliko aliye kitandani. Nafikiri inaweza kuwa hivyo kwa wanawake pia.

So ni wazi mke wa Ayubu aliguswa moja kwa moja na mashambulizi ya shetani kwa familia yao
 
Na pia kupitia mke wa Ayubu kuna kitu cha kujifunza

Ni muhimu sana unapokuwa na mwenza Imani zenu ziambatane pamoja yaani wote kama mnamtumikia Mungu basi mumtumikie Mungu kiuwaminifu haswa hata linapotokea. Jaribu kwa pamoja mnaweza kusolve

Hapa inaonesha mke wa Ayubu hakuwa vizuri na Mungu yaani alikuwa mjanja janja mlokole jina😀 na usikute jamaa hakustukia mpaka pale mke alivyomwambia amkufuru Mungu wake ndipo jamaa akaona sura halisi ya mkewe ni wa aina gani.

(Ayubu 2:9)
Mke wa Ayubu akasema: Makufuru Mungu ufe.

Ndipo utajua shetani alimwacha Ili aje kuwa silaha ya mwisho.

Lakini pia ujue, shetani alikatazwa na Mungu kugusa uhai wa Ayubu, mke wa Ayubu ni sehemu ya uhai wa Ayubu sababu ni mwili mmoja, ndio sababu hakuguswa.
 
Shetani anafanya kazi yake kwa malengo na mikakati. Anajua nani amfanyie nini na kwa namna gani ili amwangushe.

Si ajabu alimwendea Kristu jangwani akiwa amefunga siku 40 mchana na usiku, lakini akashindwa pia.

Tageti hapa ilikuwa ni Ayubu kwa sababu ndiye alikuwa mwakilishi wa Mungu kiroho na kitabia, tofauti na mkewe ambaye alikuwa mguu pande, mguu sawa.

Ingekuwa rahisi zaidi kummaliza Ayubu kupitia mtu wake wa karibu zaidi - mkewe. Japo pia akashindwa! Mungu atukuzwe milele amina!

Maana jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lile lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (1Kor 10:13).
Hapo umeiweka vizuri mkuu
 
Ukioa wewe na mkeo ni mwili mmoja,,,Kwa hio ayubu na mkewe mbele za Mungu walionekana kama Ayubu.....Sasa MUNGU alimwambia shetani afanye ubaya wote dhidi ya Ayubu Ila asiutoe uhai wake,,Kwa hio shetani asingeweza kumgusa mke WA Ayubu wakati wao walikuwa roho moja....

NB Mke WA Ayubu kumwambia amkufuru MUNGU ilikuwa ni hisia ya huruma,,mapenzi na kukata tamaa...Ayubu hakumsikiliza ila kadiri wakati ungeenda pasipo na kupoa Kwa maumivu yake bila shaka angeusikiliza ushauri wa mkewe.
 
(Ayubu 2:9)
Mke wa Ayubu akasema: Makufuru Mungu ufe.

Ndipo utajua shetani alimwacha Ili aje kuwa silaha ya mwisho.

Lakini pia ujue, shetani alikatazwa na Mungu kugusa uhai wa Ayubu, mke wa Ayubu ni sehemu ya uhai wa Ayubu sababu ni mwili mmoja, ndio sababu hakuguswa.
Shetani Na Mungu Ni Washikaji Kinoma
 
Back
Top Bottom