Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Mimi pale UDOM (bachelor ) na UDSM (master's) sikusomea kuendesha bajaji. Ningetaka kusomea kuendesha bajaji ningeenda VETA au NIT. yani na B.COM finance yangu na MA-FINANCE plus CPA juu nikawe dereva bajaji kwelii?? Hebu serikali iwe na adabu na elimu za watu.
Kwa hiyo huwezi kumiliki company ya usafiri inayotumia bajaj sababu hukusoma kuendesha bajaj?
 
Hapana.

Ila ilianzia chini na haikuibuka tu from nowhere.

Au unataka kusema uber ilitokea tu?

Unajuaje hana idea ya kuwa mmiliki baadae and maybe right now anawekeza kutokana na changamoto zake instead ya kumlipa mtu?

Do you understand kwamba kila mtu anapitia changamoto zake na kila mtu anafight battle binafsi ndani yake?

Mkuu huwezi jua amepanga nini kwenye future yake.
Utajuaje ameamua kufanya mwenyewe kwa period of time ili akiajiri watu ajue kila kinachoendelea na kinachotokea kwenye hiyo biashara.
Utajuaje anachokifanya ni uchunguzi wa biashara hivyo hataki kukurupuka?

And you mean chaajabu sababu ni mwanamke na mwenye elimu kubwa?
Sababu society yetu inaamini mwanamke hatakiwi kufanya kazi za aina hiyo like kuendesha bajaj.
Na society yetu inaamini kwamba elimu ni kuajiriwa tu.
Au kufanya makubwa bila kujua kila kikubwa kilianzia chini.
Na mwenye elimu kubwa hatakiwi kufanya kazi za aina fulani even if kwake analala njaa na ni masikini.

In that way i agree our society is stupid.
Duuuude...hapa kinachoongelewa ni FUTURE ama CURRENT situation??? Maana ushanipoteza tayari.

Binafsi sijaona chochote cha ajabu na ndio maana sioni mantiki ya kusifia ama kusema eti tujifunze kutoka kwake. Tujifunze nini sasa???
 
Bakhresa alianza kuuza urojo saivi ana maviwanda

Hapo je[emoji1787][emoji1787]
Hapana bosi....bakheresa alikuwa focus zaidi labda na huyu mdada naye yupo focused....then nafkiri bakheresa hana degree mbili kwa kukuongezea tu mtoto wa bakheresa Jamali pia alikataa kuendelea na shule akaingia ktk bishara za mzee wake na yeye nafkiri ni second in command ktk hiyo kampuni....inshu ni kujua unataka nini.....huyu dada hakutaka kupata masters kisha akaendeshe bajaji NO WAY ila baada ya kuona hali ilivyobana ndo kajichomeka huko ni jambo zuri.....
wait a minute majaji 2 shi ngapi vile? Huyu alikuwa na base nyingine ya uchumi na atarudi alipokuwa muda si mrefu....Nguvu kubwa ina mpa kiki huyu dada ni kupotosha tatizo lililopo la ajira na kulifanya tatizo ni la mtu binafsi.....

Leo yupo ktk page ya FB ya mwananchi yaaani anakula proma si mchezooooo
 
Sidhan kama neno kujiajiri limetumika vizur hapa hasa ukilinganisha na kiwango cha elimu yake
 
Duuuude...hapa kinachoongelewa ni FUTURE ama CURRENT situation??? Maana ushanipoteza tayari
You can't talk about CURRENT without FUTURE.
Unless you know what's gonna happen in the future.
Binafsi sijaona chochote cha ajabu na ndio maana sioni mantiki ya kusifia ama kusema eti tujifunze kutoka kwake. Tujifunze nini sasa??
Right.
 
Kwa hiyo huwezi kumiliki company ya usafiri inayotumia bajaj sababu hukusoma kuendesha bajaj?
Tofaitisha kumiliki kampuni ya usafiri was bajaji na mimi kuwa dereva was bajaji eti jioni naoeleka kioande kwa bosi au hata kama bajaji ni yangu niwe naendesha mwenyewe ni umbuzi
 
View attachment 1660302

Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.

Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.

Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.

Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.

Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).

Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.

“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.

Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.

Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili

View attachment 1660415
Sasa kama shida/lengo lilikuwa ni kuendesha bajaji alivyohitimu kidato cha nne si angejiunga veta kujifunza ufundi na udereva tu?
Maana yake ni kuwa amepoteza muda wake na rasilimali zake tu.
 
Usitake kuhalalisha mambo ya hovyo bwn! Unataka kunambia huyo angejua kama ataishia kuwa dereva wa bajaji angejihangaisha kuzitafuta hizo degree 2? Kama hatuwezi kuajiri watu wetu kwa nafasi zinazoendana na elimu zao, kwa nini kuwaingiza kwenye gharama na upotevu wa muda kuwapa hiyo elimu kubwa?

Tukubali tu kuwa tumeshafeli!!!!
Mavyuo ndiyo yamefunguliwa chungu tele

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Mfano wa kuigwa, sio kila siku kulia lia na kulaumu tu, kumbe maisha yako unayo wewe mkononi mwako, yaani wewe ndiyo unatakiwa kuyafanya unavyotaka na si kusubiri hisani kutoka kwa mwingine
Huyo dada mshamba tu wenzie hata lanne hatujamaliza tunasukuma bajaj yeye hadi na midigrii miwili
 
Hivi elimu ya Tanzania ina ubora gani? Kiwango cha wasomi wetu kutatua changamoto mbalimbali za kimaisha kiko dunia

Achana naye huyo mbuteee ! Kujiajiri yeye anawaza labda uwe na nakampuni la kwako binafsi ??
Anyway tukiachana na huyo Mbutee, Elimu yetu Tanzania imekuwa ikisaidia japo sio sana kwa maana watunga sera wa nchi hii wengi wanachumia matumbo yao na pia mfumo wetu wa Elimu ni Ovyo sana. Watu wanaandaliwa kuwa waajiriwa kuliko kujiajiri, hivyo kupelekea kuwa na Mbutee wengi mtaani kama huyu @MoseKing ...! Hii ni Mbute ambayo haioni kujiajiri kwa kuendesha Bajaji kama kazi ambayo inatosha kabisa kumtoa mtu kimaisha.
Kuna haja ya kupitia upya mitaala yetu na tuachane nayo mitaala ya Enzi za mababu ambayo ililenga kuandaa watu kufanya kazi kwenye ofisi za Wakoloni na sio kujiajiri au kuwa wagunduzi au watatuaji wa matatizo ya kijamii
 
Utopolo mtupu.
Hivi unajua kuwa kuna kazi zingine za serikali matangazo yake huishia ofisini ndani kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa Wilaya na ndani ofisi ya mkuu wa kitengo mkoa au wilaya?
Na ifahamike wengine huajiriwa na hawakai ofisini.
Kuna mama muuza mihogo barabarani VETA dar , yule mama ile kazi ya kuzurura juani haitegemei, yupo pale kwa mission.
Kama hadi wengine hujifanya machizi ili wapate info mtaani unakuja kushangaa huyo dada na shahada zake 2 kudrive bajaji?
Unamjua mmiliki wa hiyo baiaji?.
Kabla hamjaja juu kuhusu habari za mtu yeyote tafuteni nature yake mtajua ukweli.
Afisa kipenyo sio!!!
 
Kwani Tanzania Kuna wasomi? au wale wanaokariri darasani?
 
Tulisema tu hiki chuo cha UDOM kitatutolea takataka ona Sasa. Eti mtu ana MASTAZ dereva bajaj. Jinga kabisa. UDOM ni janga jamani.
Bhana wee Tanzania hakuna wasomi, wasomi gani wanashindwa hata kubuni toothpick!!
 
Back
Top Bottom