Andrew Tate
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 4,503
- 6,861
Kwa hiyo huwezi kumiliki company ya usafiri inayotumia bajaj sababu hukusoma kuendesha bajaj?Mimi pale UDOM (bachelor ) na UDSM (master's) sikusomea kuendesha bajaji. Ningetaka kusomea kuendesha bajaji ningeenda VETA au NIT. yani na B.COM finance yangu na MA-FINANCE plus CPA juu nikawe dereva bajaji kwelii?? Hebu serikali iwe na adabu na elimu za watu.
Atatumiaje Elimu vizuri wakati tumefundishwa kuajiriwa!! [emoji3][emoji3][emoji3]Anaendesha Bajaj Kama Dereva mwenye Masters au Kama seven B leaver?
Atumie Elimu Vizuri.
Duuuude...hapa kinachoongelewa ni FUTURE ama CURRENT situation??? Maana ushanipoteza tayari.Hapana.
Ila ilianzia chini na haikuibuka tu from nowhere.
Au unataka kusema uber ilitokea tu?
Unajuaje hana idea ya kuwa mmiliki baadae and maybe right now anawekeza kutokana na changamoto zake instead ya kumlipa mtu?
Do you understand kwamba kila mtu anapitia changamoto zake na kila mtu anafight battle binafsi ndani yake?
Mkuu huwezi jua amepanga nini kwenye future yake.
Utajuaje ameamua kufanya mwenyewe kwa period of time ili akiajiri watu ajue kila kinachoendelea na kinachotokea kwenye hiyo biashara.
Utajuaje anachokifanya ni uchunguzi wa biashara hivyo hataki kukurupuka?
And you mean chaajabu sababu ni mwanamke na mwenye elimu kubwa?
Sababu society yetu inaamini mwanamke hatakiwi kufanya kazi za aina hiyo like kuendesha bajaj.
Na society yetu inaamini kwamba elimu ni kuajiriwa tu.
Au kufanya makubwa bila kujua kila kikubwa kilianzia chini.
Na mwenye elimu kubwa hatakiwi kufanya kazi za aina fulani even if kwake analala njaa na ni masikini.
In that way i agree our society is stupid.
Hapana bosi....bakheresa alikuwa focus zaidi labda na huyu mdada naye yupo focused....then nafkiri bakheresa hana degree mbili kwa kukuongezea tu mtoto wa bakheresa Jamali pia alikataa kuendelea na shule akaingia ktk bishara za mzee wake na yeye nafkiri ni second in command ktk hiyo kampuni....inshu ni kujua unataka nini.....huyu dada hakutaka kupata masters kisha akaendeshe bajaji NO WAY ila baada ya kuona hali ilivyobana ndo kajichomeka huko ni jambo zuri.....Bakhresa alianza kuuza urojo saivi ana maviwanda
Hapo je[emoji1787][emoji1787]
You can't talk about CURRENT without FUTURE.Duuuude...hapa kinachoongelewa ni FUTURE ama CURRENT situation??? Maana ushanipoteza tayari
Right.Binafsi sijaona chochote cha ajabu na ndio maana sioni mantiki ya kusifia ama kusema eti tujifunze kutoka kwake. Tujifunze nini sasa??
Tofaitisha kumiliki kampuni ya usafiri was bajaji na mimi kuwa dereva was bajaji eti jioni naoeleka kioande kwa bosi au hata kama bajaji ni yangu niwe naendesha mwenyewe ni umbuziKwa hiyo huwezi kumiliki company ya usafiri inayotumia bajaj sababu hukusoma kuendesha bajaj?
Sawa hata kama bt siwezi endesha bajajiHata bcom ungekwenda IFM.
Sasa kama shida/lengo lilikuwa ni kuendesha bajaji alivyohitimu kidato cha nne si angejiunga veta kujifunza ufundi na udereva tu?View attachment 1660302
Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.
Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.
Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.
Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.
Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).
Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.
“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.
Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.
Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili
View attachment 1660415
Vita sikuzote havina kuchagua silaha kulingana na mazingira. Na maisha ni mapambano kila itwapo leo mnyonge wa hali ya chini !Sasa kama shida/lengo lilikuwa ni kuendesha bajaji alivyohitimu kidato cha nne si angejiunga veta kujifunza ufundi na udereva tu?
Maana yake ni kuwa amepoteza muda wake na rasilimali zake tu.
Mkuu unaelewa maana ya pun?Unadhani kwanini ifutwe?
Mavyuo ndiyo yamefunguliwa chungu teleUsitake kuhalalisha mambo ya hovyo bwn! Unataka kunambia huyo angejua kama ataishia kuwa dereva wa bajaji angejihangaisha kuzitafuta hizo degree 2? Kama hatuwezi kuajiri watu wetu kwa nafasi zinazoendana na elimu zao, kwa nini kuwaingiza kwenye gharama na upotevu wa muda kuwapa hiyo elimu kubwa?
Tukubali tu kuwa tumeshafeli!!!!
Sherehe kwa mkufunzi, kilio kwa mwanachuo.
Huyo dada mshamba tu wenzie hata lanne hatujamaliza tunasukuma bajaj yeye hadi na midigrii miwiliMfano wa kuigwa, sio kila siku kulia lia na kulaumu tu, kumbe maisha yako unayo wewe mkononi mwako, yaani wewe ndiyo unatakiwa kuyafanya unavyotaka na si kusubiri hisani kutoka kwa mwingine
Hivi elimu ya Tanzania ina ubora gani? Kiwango cha wasomi wetu kutatua changamoto mbalimbali za kimaisha kiko dunia
Afisa kipenyo sio!!!Utopolo mtupu.
Hivi unajua kuwa kuna kazi zingine za serikali matangazo yake huishia ofisini ndani kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa Wilaya na ndani ofisi ya mkuu wa kitengo mkoa au wilaya?
Na ifahamike wengine huajiriwa na hawakai ofisini.
Kuna mama muuza mihogo barabarani VETA dar , yule mama ile kazi ya kuzurura juani haitegemei, yupo pale kwa mission.
Kama hadi wengine hujifanya machizi ili wapate info mtaani unakuja kushangaa huyo dada na shahada zake 2 kudrive bajaji?
Unamjua mmiliki wa hiyo baiaji?.
Kabla hamjaja juu kuhusu habari za mtu yeyote tafuteni nature yake mtajua ukweli.
Bhana wee Tanzania hakuna wasomi, wasomi gani wanashindwa hata kubuni toothpick!!Tulisema tu hiki chuo cha UDOM kitatutolea takataka ona Sasa. Eti mtu ana MASTAZ dereva bajaj. Jinga kabisa. UDOM ni janga jamani.
Right.Mkuu unaelewa maana ya pun?