Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Mfano wa kuigwa, sio kila siku kulia lia na kulaumu tu, kumbe maisha yako unayo wewe mkononi mwako, yaani wewe ndiyo unatakiwa kuyafanya unavyotaka na si kusubiri hisani kutoka kwa mwingine
Ni Jukumu la lazima kwa serikali kuajiri watu wake au kuwasaidia wajiajiri. Na wanalipwa pesa za walipa kodi kwa sababu hiyo.

Kama wameshindwa kufanya hilo, wap8she wawaachie wanaoweza.

Huwezi kumlipa mtu alime barabara upite, pesa anakula kila siku halafu anakwambia tatizo lako boss hutaki kujiongeza kulima tu mwenyewe upite.

Na wakati huo huo, hataki kuachia hiyo tenda ya kutengeneza barabara.

Wanachokifanya watawala ni kutafuta namna ya kukwepa wajibu wao ili watafune kodi za walalahoi bila kufanya kazi wala kupigiwa kelele.
 
1609070056691.png

Hivi elimu ya Tanzania ina ubora gani? Kiwango cha wasomi wetu kutatua changamoto mbalimbali za kimaisha kiko dunia

Nancy Lema ni msomi wa Elimu ya Masters ya Project Management Chuo cha SAINT MARY’S UNIVERSITY OF MINNESOTA Nchini Marekani na ameishi Marekani kwa miaka 10, mwaka 2015 aliamua kurudi rasmi Tanzania na kwenda kwao Mwanza na kuanza kutafuta kazi kwenye Makampuni bila mafanikio ndipo akaja na wazo la kuuza chakula aina ya makande kwenye ofisi Mwanza.

“Nilijua nimemaliza Masters yangu nakuja Tanzania kutafuta Kazi haitakuwa ngumu lakini kila sehemu niki-apply naambiwa subiri kwanza ilinifanya nifikirie nini cha kufanya” Nancy Lema

” Wazazi wangu hawakukubliana na mimi nianze kupika wakati wamenisomesha walitegemea niwe Meneja Kampuni flani na elimu kubwa, Ila kwa sasa ndio Wateja wangu wakubwa” Nancy Lema

Dada huyu msomi naye gumzo kwa kutafuta pesa bila kujali elimu kwani anaelewa nini maana ya neno moshi kwa wachaga !
 
View attachment 1660302

Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.

Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.

Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.

Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.

Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).

Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.

“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.

Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.

Kilichomfanya aendeshe bajaji
Mwasu aliamua kuwa dereva bajaji kwa kuangalia fursa baada ya kuona wengine wanaofanya biashara hiyo wanafanikiwa, akitolea mfano rafiki yake aliyekuwa anaendesha bajaj ambaye alimhamasisha kufanya kazi hiyo. “Nikiwa dereva bajaj najua kuwa ni lazima mtu asafiri, tofauti na kuvaa nguo. Mtu anaweza kununua nguo baada ya muda mrefu,” alisema.

Mwasu alisema alipata taarifa kuwa Benki ya CRDB inakopesha bajaj kwa Sh6 milioni, na katika kufuatilia alitakiwa kuwa na mdhamini ambaye ni mwajiriwa na mshahara wake unapitia katika akaunti ya taasisi hiyo, ili akishindwa kurejesha wawe wanamkata fedha hiyo. Na baada ya kukamilisha vigezo hivyo, alikabidhiwa bajaji na kuanza kufanyia biashara tangu Desemba 2018. Alisema ‘kijiwe’ chake cha kwanza kilikuwa katika eneo la hoteli ya Royal Village, lakini baada ya muda akaamua kuhamia maeneo ya mjini ili kupata abiria zaidi. Na Desemba 2019 alimaliza marejesho kwa muda uliokuwa umepangwa na kuanzia hapo akawa mmiliki halali bajaj hiyo.

Manufaa ya bajaji
Dada Mwasu, amesema usafiri huo umemsaidia kwa kiasi kikubwa kupanga mipango yake kupitia fedha anazozipata -- analisha familia yake na anasomesha watoto shule binafsi. Na kwa sasa hana mawasiliano na baba watoto wake, mtoto wake wa kwanza yupo darasa la pili na mwingine yupo chekechea na anatarajia kujenga nyumba yake ya kuishi kwa fedha anazozipata kwenye usafiri huo. Anasema mipango yake kwa siku ni kupata Sh50,000, lakini kuna siku anapata zaidi ya hizo na wakati mwingine anaishia kupata hata Sh20,000.

Changamoto aipatayo
Mwasu anazungumzia kile anachoita unyanyasaji unaofanywa na trafiki barabarani kuwakamata na kuwasingizia makosa mbalimbali ikiwemo kuzidisha abiria. Aliwahi kukamatwa na kusingiziwa kuwa alibeba abiria saba kwenye bajaji yake, kitu ambacho alisema haikuwa kweli, kesi hiyo ilifika hadi mahakamani lakini alionekana hakuwa na kosa lolote. “Upo uonevu unaofanywa na trafiki hata kama huna kosa wanakusingizia makosa, ingekuwa ni mtu wa kukata tamaa baada ya kufikishwa mahakamani asingeendelea na kazi hiyo, ila mimi ni strong woman (mwanamke jasiri) ndio maana bado napambana,” alisema na kuongeza. “Tumekuwa tukipakia abiria kwa Sh500 ukitumia mfumo huo unapata pesa nyingi kuliko ukiwa unasubiri wanaokukodi.

Chanzo Mwananchi: Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili
Umeandika Mambo mengi Sana mimi nimesoma kichwa Cha habari na aya ya kwanza....

Binafsi sitarajii wasomi wa degree mpaka masters kuja na idea cheap Kama izi....

Ukiamua kua boda boda au dereva wa bajaji na degree yako au masters.... Just shout your mouth....

Hizoo Kazi za Bajaji au boda boda.......
Ange zianza MIAKA kumi iliyo pita pengine angekua mbali huo muda alio Soma na kutesa akili na kujibu assignment na quiz na test, UE Mpka kuvaa Joho sio lelemama....

Tunataka aje na wazo jipya la kiutendaji kwenye bajaji.......

Kwa watu wenye ELIMU za vyuo vikuu then kuja kufanya Kazi za vibarua vya zege haikubariki

Otherwise Kama ni ku survive maana kweny MAISHA Kuna point unafika the only thing you need is just to survive...

Aluta continue kwa vijana wote....
Informal sector
wanao pambana all over the World........
 
Yeye hana kosa. Anatafuta namna ya kuishi. Ila hiyo ni dalili of the failed state.

The government has failed the youth na hivyo hakuna any reason ya kuwaambia watu ooh huyo mfano wa kuigwa sijui nini.

Wengi wanaokwambia hivyo target yao ni kukwepa Jukumu lao kama watawala.
Tatizo la kutoajiriwa ni janga kwa kizazi kipya tofauti na karne iliyopita; hata kwa mataifa makubwa duniani.
 
Daa hiv amna mtu mwenye Namba Ya Jiwe Nimcheki ........!!!!

Maana sijui tunaenda wap!! Nahtaj kumuuliza tu:

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Jambo hili linaonyesha Elimu yetu sisi haina msaada wala thamani yeyote, na hii inawakatisha tamaa sasa Walio ngazi za Chini kama mtu aliyeishia darasa la Saba anaweza kuendesha Bajaji kwanini upoteze Pesa na muda kusoma shahada mbili afu uje uendeshe bajaji? Jibu ni kwamba Dada anafanya kazi hiyo ili asukume siku baada ya kukosa mazingira ya kumfanya atumie Elimu yake.

jambo Hili sio la kujivunia hata kidogo, kwamba Taifa linasomesha watu ambao haliwezi kuwatumia wala kuwasaidia kutumia ujuzi wao, Dada huyu angejiajiri kupitia taaluma yake ningemuelewa sana. Kujiairi sio vibaya lakini kuajiriwa pia sio vibaya kwasababu ni ukweli uliowazi kwamba hatuwezi sote kujiajiri hiyo haitokaa itokee. Ni vema viongozi watafakari tulipojikwaa hali ikiendelea hivi hakutakuwa na maana ya kwenda Chuo kikuu kabisa
 
Kujiajiri ni kama walivyofanya kina Mendes wa KopaGas, Wasafi media, Maxence Meli wa JF.

Ni kampuni sustainable, ambazo unaweza kujua kabisa zitaajiri watu, kukuza kipato na kuvutia uwekezaji hata ni kupitia DSE.

Sasa yeye buashara ya Bajaj, akilala na yenyewe inalala
Na hawa ukiangalia ni watu waliojiajiri kupitia taaluma zao, Mimi natamani sana kujiajiri Niwe Mkandarasi au niwe na Consultancy Firm, hapo sitokuwa nilipoteza muda wa zaidi ya miaka 18 ya kutafuta Elimu. Lakini mtu kasoma leo ni Daktari kesho tukute anachoma Mahindi afu tushangilie eti kajiajiri huu utakuwa uendawazimu kabisa
 
Jambo hili linaonyesha Elimu yetu Isi to na msaada wala thamani yeyote, na hii inawakatisha tamaa sasa Walio ngazi za Chini kama mtu aliyeishia darasa la Saba anaweza kuendesha Bajaji kwanini upoteze Pesa na muda kusoma shahada mbili afu uje uendeshe bajaji? Jibu ni kwamba Dada anafanya kazi hiyo ili asukume siku baada ya kukosa mazingira ya kumfanya atumie Elimu yake.

jambo Hili sio la kujivunia hata kidogo, kwamba Taifa linasomesha watu ambao haliwezi kuwatumia wala kuwasaidia kutumia ujuzi wao, Dada huyu angejiajiri kupitia taaluma yake ningemuelewa sana. Kujiairi sio vibaya lakini kuajiriwa pia sio vibaya kwasababu ni ukweli uliowazi kwamba hatuwezi sote kujiajiri hiyo haitokaa itokee. Ni vema viongozi watafakari tulipojikwaa hali ikiendelea hivi hakutakuwa na maana ya kwenda Chuo kikuu kabisa
Umesema kweli Granite
 
Kuna jambo anatuficha , kafanya kazi za NGOs tangu 2009

Kama mshahara ulikua mdogo ada ya kusoma masters na pesa ya kujikimu alipata wapi ?

Kwa position alizotaja kufanyia kazi napata mashaka na huo mshahara aliotaja

Namalizia , kuna jambo anatuficha

Lakini kuhusu biashara nadhani ni suala la kuyumba kiuchumi tu limetokea maana inaonekana tayari alikua na biashara kubwa ya nguo
 
Hivi kweli UWEZO WETU , wasomi kiwango hata cha diploma, hatuwez kubuni bali kuvamia idea iliyobuniwa na std seveni,? " hii inasikitisha Sana Sana, ina maana IRR(internal rate of return) kwa serikali KUWEKEZA kwenye elimu linakomea kumonitor kutoa tu mikopo, baada ya kumaliza tu biashara imeisha, kuna haja ya mfumo yetu iliangalie hili, kama Kweli msomi nguri kama Huyo anafaa ku-compete Sokoni na wale less than std seven?. Mr.einstern, amewahi sema,"UKIOONA MWANAFUNZI wako hajaelewa, jua wewe una mbinu kidogo na uelewa mdogo kumuelimisha MWANAFUNZI". Naona hili si tatizo la Wanafunzi bali mfumo, kwani same class mmoja anaajiliwa Kampuni A, anafanya vizur, mwingine analaumiwa kwasabab tu mazingira yake sio rafik. !! ".Stefan's Law of black body, alisema, temperature flow from high concentration to low temperatures under certirice per bus" aliimanisha, kuwa joto litatoka palipo na joto kubwa kwenda palipo na joto kidogo, hivyo chenye joto kubwa kitapoteza HARAKA joto lake, ,namuona msomi Huyu akipoteza uwezo wake wa KUFIKIRI kwani anaokutana nao kwenye maeneo yake ya kazi ni std seven (low temperature) kifikra, hivyo atajikuta anafanana nao, Na kuwaza level moja. Siku tukioona msomi mmoja kuwa kundi lisilo lake ni tatizo la sote basi TUTAWAZA SAWA.. iam not voting this kind of entrepreneur as appropriate to be promoted as a legacy to the rest of university graduates.
image_bc34caea-f65d-4b2b-9212-c8fd47230f1d20201117_181659.jpeg
image_b2f4bc19-472b-44a7-97fd-b0c1c50cc3a920201222_170621.jpeg
 
View attachment 1660302

Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.

Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.

Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.

Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.

Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).

Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.

“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.

Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.

Kilichomfanya aendeshe bajaji
Mwasu aliamua kuwa dereva bajaji kwa kuangalia fursa baada ya kuona wengine wanaofanya biashara hiyo wanafanikiwa, akitolea mfano rafiki yake aliyekuwa anaendesha bajaj ambaye alimhamasisha kufanya kazi hiyo. “Nikiwa dereva bajaj najua kuwa ni lazima mtu asafiri, tofauti na kuvaa nguo. Mtu anaweza kununua nguo baada ya muda mrefu,” alisema.

Mwasu alisema alipata taarifa kuwa Benki ya CRDB inakopesha bajaj kwa Sh6 milioni, na katika kufuatilia alitakiwa kuwa na mdhamini ambaye ni mwajiriwa na mshahara wake unapitia katika akaunti ya taasisi hiyo, ili akishindwa kurejesha wawe wanamkata fedha hiyo. Na baada ya kukamilisha vigezo hivyo, alikabidhiwa bajaji na kuanza kufanyia biashara tangu Desemba 2018. Alisema ‘kijiwe’ chake cha kwanza kilikuwa katika eneo la hoteli ya Royal Village, lakini baada ya muda akaamua kuhamia maeneo ya mjini ili kupata abiria zaidi. Na Desemba 2019 alimaliza marejesho kwa muda uliokuwa umepangwa na kuanzia hapo akawa mmiliki halali bajaj hiyo.

Manufaa ya bajaji
Dada Mwasu, amesema usafiri huo umemsaidia kwa kiasi kikubwa kupanga mipango yake kupitia fedha anazozipata -- analisha familia yake na anasomesha watoto shule binafsi. Na kwa sasa hana mawasiliano na baba watoto wake, mtoto wake wa kwanza yupo darasa la pili na mwingine yupo chekechea na anatarajia kujenga nyumba yake ya kuishi kwa fedha anazozipata kwenye usafiri huo. Anasema mipango yake kwa siku ni kupata Sh50,000, lakini kuna siku anapata zaidi ya hizo na wakati mwingine anaishia kupata hata Sh20,000.

Changamoto aipatayo
Mwasu anazungumzia kile anachoita unyanyasaji unaofanywa na trafiki barabarani kuwakamata na kuwasingizia makosa mbalimbali ikiwemo kuzidisha abiria. Aliwahi kukamatwa na kusingiziwa kuwa alibeba abiria saba kwenye bajaji yake, kitu ambacho alisema haikuwa kweli, kesi hiyo ilifika hadi mahakamani lakini alionekana hakuwa na kosa lolote. “Upo uonevu unaofanywa na trafiki hata kama huna kosa wanakusingizia makosa, ingekuwa ni mtu wa kukata tamaa baada ya kufikishwa mahakamani asingeendelea na kazi hiyo, ila mimi ni strong woman (mwanamke jasiri) ndio maana bado napambana,” alisema na kuongeza. “Tumekuwa tukipakia abiria kwa Sh500 ukitumia mfumo huo unapata pesa nyingi kuliko ukiwa unasubiri wanaokukodi.

Chanzo Mwananchi: Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili
Ana bima ya afya?
Ana nssf?
Akizeeka ataishije
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom