Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

View attachment 1660302

Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.

Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.

Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.

Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.

Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).

Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.

“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.

Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.

Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili

View attachment 1660415
Hapa ndio tunaonyesha ujinga wetu...sasa mtu unafanya kitu ambacho asie na masters anafanya whats the point ya educating that person.
 
Hiyo biashara angeweza kuifanya hata angeishia darasa la saba. Instead jamii ilimuhimiza aendelee kama miaka 13 na shule kwa ajili ya kuusaka ujuzi mwingine, ila sasa amejikuta jamii ile ile inamwambia asipende kutegemea ujuzi aliousaka kwa miaka yote hiyo, maana ni ubishoo.
 
Na wasiojua kiswahili wapitie hapa kuhusu hii !🙄
Ndio maana waswahili tunanunua mwananchi, wanaojua kiingereza wananunua the citizen, hilo ni gazeti moja, same content, lugha tofauti...hamna kitu cha kuji proud hapo, tumia elimu yako vizuri
 
Hiyo biashara angeweza kuifanya hata angeishia darasa la saba. Instead jamii ilimuhimiza aendelee kama miaka 13 na shule kwa ajili ya kuusaka ujuzi mwingine, ila sasa amejikuta jamii ile ile inamwambia asipende kutegemea ujuzi aliousaka kwa miaka yote hiyo, maana ni ubishoo.
Je ! Ni wasomi wangapi wana vyeti vizuri vya elimu juu, lakini wanapata taabu sana baada ya kukosa ajira na hata pesa ya kununua wembe nk ?
1609074711421.png
 
Hapa ndio tunaonyesha ujinga wetu...sasa mtu unafanya kitu ambacho asie na masters anafanya whats the point ya educating that person.
Tutafakari kwa lengo kusaidia jamii ya wasomi waliokosa kazi na kusubiri ajira ya serikali bila mafanikio katika kada mbalimbali kama elimu,afya nk
 
1609075650771.png


Kwenye kujiajiri ni lazima" tukubaliane kuwa sio rahisi,sio rahisi hata kidogo !” Usikubali maisha yako na miaka yote uliyotumia kusoma itolewee maamizi na ‘makaratasi’ ambayo bila shaka huonyesha matokeo ya muda fulani wa elimu yako tu. Nikki wa Pili aliwahi kuimba 'Sitaki Kazi’,kwenye wimbo huo alielezea changamoto za upatikanaji na utendaji wa ajira. Sihitaji kuufanyia uhakiki wimbo huo ila ni wazi kuwa Nikki wa Pili hakuwa anakubaliana na swala la kuajiriwa. Lengo sio kupinga uwepo wa elimu wala ajira,lengo ni kuonyesha ni namna gani elimu uliyo nayo inawezaje kukusaidia kufanya uzalishaji.

Maoni ya Classmate Maeda

1609075686127.png
 
Tulisema tu hiki chuo cha UDOM kitatutolea takataka ona Sasa. Eti mtu ana MASTAZ dereva bajaj. Jinga kabisa. UDOM ni janga jamani.
University Of Dodoma
Haa😂😁
Kwenye Mpira Wanasema Amerudisha Kwa Kipa Mpaka Goal
 
Tumelaliwa sana ndugu zangu
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu

Tumeliwa Sana Ndugu Zangu

Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu

Tumegongwa Sana Ndugu Zangu
Vyovyote Mtakavyosema Najua Mmenielewa
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Support sio ngazi ya familia tu ni mpaka kwa ngazi ya serikali😂😂😂
Bro! all in all still ni kwamba unatakiwa uwe na mtaji wako mwenyewe kama una elimu yeyote Tz, na kwa mifumo ya maisha yetu ambayo mtu msomi hata kula kwa familia aliyotoka bado ni shida. Wazungu na wamarekani msomi aliyemaliza chuo anauwezo wa kuwa nyumbani akila na kupata nauli na mahitaji mengine mhimu kutoka kwenye familia yake, anaweza kupelekwa kuangalia michezo ya mipira na michezo mingine kwa gharama ya familia.Wakati huku kwetu nadra sana kuona baba anabeba familia kwenda kwenye michezo kwa garama ya mwanafamilia mmoja. Hii inamaanisha Mhitimu wa Tz unatakiwa kusimama kama yeye wenzetu wanapata support toka familia zao wakati sisi ni watu wachache wanaoweza kupata hiyo support ni ngumu kusema elimu ya tz ni mbovu ila jamii haina uwezo wa kusupport wasomi wetu

Sent from my MI PLAY using JamiiForums mobile app
 
Uko twitter kuna ujumbe wa Salha binti Aziz kwa "Vijana (wasomi na wasio wasomi) kwamba wafahamu kuwa Ajira ni chache ila kazi za kufanya zipo nyingi sana, maamuzi ni yetu" ...............!
 
Back
Top Bottom