Musundi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,584
- 2,613
YesAngeenda veta
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
YesAngeenda veta
Lecture atalipwa shs ngapi na kwenye bajaji anapata shs ngapi?Inamana ameshindwa kuwa hata lecture , anauzamivu wa nini, ? Huyo binti
Sent using Jamii Forums mobile app
Ishu hapa ni pesa unazopata , kama kuchoma mahindi kunamlipa kuliko udaktari kwa nini asichome?Na hawa ukiangalia ni watu waliojiajiri kupitia taaluma zao, Mimi natamani sana kujiajiri Niwe Mkandarasi au niwe na Consultancy Firm, hapo sitokuwa nilipoteza muda wa zaidi ya miaka 18 ya kutafuta Elimu. Lakini mtu kasoma leo ni Daktari kesho tukute anachoma Mahindi afu tushangilie eti kajiajiri huu utakuwa uendawazimu kabisa
Watanzania wenye bima na nssf ni wachache sana kuna kundi kubwa la wakulima, wafugaji na wafanyabiashara hawajui nini maana ya nssf na bima na wanaishiAna bima ya afya?
Ana nssf?
Akizeeka ataishije
Unajua walikoanzia haoKujiajiri ni kama walivyofanya kina Mendes wa KopaGas, MakJuice, Wasafi media, Maxence Melo wa JF.
Ni kampuni sustainable, ambazo unaweza kujua kabisa zitaajiri watu, kukuza kipato na kuvutia uwekezaji hata kama ni kupitia DSE.
Sasa yeye biashara ya Bajaj, akilala na yenyewe inalala.
yani kesho kutwa awe na bajaji kumi???acha ulongo field sio kwepesi kiasi hicho ni ngumu na itachukua muda na uzee utakua umesha mnyemelea na hata akifikisha ni nje ya matalajio yake kabisaUnajua walikoanzia hao
Huyu anaweza akawa kaanza na bajaji
Kesho kutwa akiwa na Bajaj kumi daladala,bodaboda utamtukana ?
Akili zingine bana
Huwa siwaelewagi watu ambao wanakatisha tamaa mtu akianza moja
Halafu siku akitusua utasikia "jamaa bana nilisoma nae yule ,aaah yule alikuwa muuza mitumba tu"
Wabongo nuksi sana roho mbaya za kichawi
Umejichoka sio eeeh [emoji849]Daa hiv amna mtu mwenye Namba Ya Jiwe Nimcheki ........!!!!
Maana sijui tunaenda wap!! Nahtaj kumuuliza tu:
Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
At the end of the day we only consider how much you have made .Jambo hili linaonyesha Elimu yetu sisi haina msaada wala thamani yeyote, na hii inawakatisha tamaa sasa Walio ngazi za Chini kama mtu aliyeishia darasa la Saba anaweza kuendesha Bajaji kwanini upoteze Pesa na muda kusoma shahada mbili afu uje uendeshe bajaji? Jibu ni kwamba Dada anafanya kazi hiyo ili asukume siku baada ya kukosa mazingira ya kumfanya atumie Elimu yake.
jambo Hili sio la kujivunia hata kidogo, kwamba Taifa linasomesha watu ambao haliwezi kuwatumia wala kuwasaidia kutumia ujuzi wao, Dada huyu angejiajiri kupitia taaluma yake ningemuelewa sana. Kujiairi sio vibaya lakini kuajiriwa pia sio vibaya kwasababu ni ukweli uliowazi kwamba hatuwezi sote kujiajiri hiyo haitokaa itokee. Ni vema viongozi watafakari tulipojikwaa hali ikiendelea hivi hakutakuwa na maana ya kwenda Chuo kikuu kabisa
Well said!Na hawa ukiangalia ni watu waliojiajiri kupitia taaluma zao, Mimi natamani sana kujiajiri Niwe Mkandarasi au niwe na Consultancy Firm, hapo sitokuwa nilipoteza muda wa zaidi ya miaka 18 ya kutafuta Elimu. Lakini mtu kasoma leo ni Daktari kesho tukute anachoma Mahindi afu tushangilie eti kajiajiri huu utakuwa uendawazimu kabisa
Bima ya afya yenyewe ya siku hizi pasua kichwaAna bima ya afya?
Ana nssf?
Akizeeka ataishije
Risk taking ndio Jambo la msingi ili ufanikiweHizi kasumba ndo zinashusha hadhi ya elimu.
Halafu chunguza Mara nyingi Hawa wasio na sifa za kuajiriwa, kwa kukosa vigezo ndo wanakimbilia kuinajisi Elimu. Unakuta mtu kweli kamaliza chuo na Ana degree Sawa, lakn Sasa ufaulu wake (GPA) alipata ndo unamkwamisha kupata Ajira, matokeo yake ndo anakimbilia huku na kujinadi kuwa yeye kasoma lakini amejiajiri, kumbe ukweli anaujua mwenyewe.
Mwisho wa siku usishangae mwanao akakwambia sitaki kusoma, naomba uninunulie Boxer nipige kazi. Je wewe kama mzazi mwenye malengo utakubali?.
We unafikiri mzazi wake aliemsomesha elimu ya Awali angejua kama anakuja kuendesha Bajaji angekubali kulipia Ada yote hiyo hadi kufika kuendesha Bajaji. HIYO SIO SIFA. Angalau angekuwa mwanaume.
Kwanza si kazi ya kujivunia maana Ana Risk, maana ni mtoto wa kike anashawishi kuibiwa Bajaji au kubakwa, Na pia anytym anaweza kupata ajali, akatekwa au kuvamiwa na wahalifu. halafu Hao watoto Wataangaliwa na nani, na yeye ndo mama.
Sio kila jambo la kuunga mkono, mengine ni ya kushauri au ikiwezekana kupinga kabisa. Anapaswa ajitafakari, kwanza yeye anaona sifa kupata publicity huyo kwenye magaazeti, kumbe ndo amewapa watu fursa ya kumtafuta, maana hata walikua hawamjui.
Ni kheri hata angeenda kuuza chakula, matunda au juice. Lah, kama Anapenda mambo ya usafirishaji ni kheri angekuwa Dereva wa maroli au konda wa maBus ya mikoani, Risk yake sio kubwa kama hiyo kazi.
We Ngoja tutakuja kuskia mwisho wa hiyo kazi yake kama utakuwa wa kheri .
Usikute wewe ndio kilaza hujui Nini anatakaKilaza tu huyo...ajira zinatangazwa na Utumishi kila day..kama ana uwezo angepata kazi za utumishi. Huo ndio ukweli
Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
View attachment 1660302
Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.
Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.
Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.
Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.
Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).
Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.
“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.
Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.
Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili
View attachment 1660415
Shahada mbili boss ni elimu kubwa sana kuja na mawazo ya kuendesha bajaji kwakweli lazima jamii isikitike na wale waliokupa pesa ya kwenda shule watamwaga machoziHamna Bilionea aliyeajiriwa,
Wengi wao hawakuamaliza chuo kabisa, Mark Zuckerberg, Bill Gates ect.
Sasa cha ajabu nini hapo