mwekwa ntandu
JF-Expert Member
- Aug 24, 2019
- 1,040
- 2,428
Ndungai karidhika sasa kumuona mgogo mwenzie anaendesha bajaji na kuwa kama mfano wa kuigwa kwa graduate!! Pambav
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
The point NI kuwa ana surviveUmeandika Mambo mengi Sana mimi nimesoma kichwa Cha habari na aya ya kwanza....
Binafsi sitarajii wasomi wa degree mpaka masters kuja na idea cheap Kama izi....
Ukiamua kua boda boda au dereva wa bajaji na degree yako au masters.... Just shout your mouth....
Hizoo Kazi za Bajaji au boda boda.......
Ange zianza MIAKA kumi iliyo pita pengine angekua mbali huo muda alio Soma na kutesa akili na kujibu assignment na quiz na test, UE Mpka kuvaa Joho sio lelemama....
Tunataka aje na wazo jipya la kiutendaji kwenye bajaji.......
Kwa watu wenye ELIMU za vyuo vikuu then kuja kufanya Kazi za vibarua vya zege haikubariki
Otherwise Kama ni ku survive maana kweny MAISHA Kuna point unafika the only thing you need is just to survive...
Aluta continue kwa vijana wote....
Informal sector
wanao pambana all over the World........
Hivi bado yupo huyo jamaaMakjuisi je
Hahahahahaha nmecheka kikuma yani😂😂😂Kwahiyo kazi ya watawala ni ipi ?
Maana naona unauliza swali la kichoko sana.
Huyo cooma mtie kofi kwa heshima yangu 😂🤣🤣Tunasubiri sasa amiliki kiwanda cha bajaji,
Manake kuna motivesheni spika hapa anasema alianza kula yai la kuku moja la kukaanga sasa hivi ana miliki kuku wa mayai 10,000
Zero IQ AT WORKUko sahihi huyu kapoteza muda wake bure kupata hizo digrii 2. Hata std 7 wanaendesha bajaj vizuri tuu so hakuna la kujifunza hapo. Halafu M&E officer kwenye NGOs inalipwa laki 4?? Ninafahamu watu wengi tuu wanalipwa 1.5 to 2M kwa hiyo post, labda alishindwa kujiuza kwenye interview... Halafu kama alifikia kwenda hadi China but still akashindwa kuwa na duka kubwa la nguo hiyo nayo inatia shaka. Watu wengi tuu wana bajaj mpaka 3 na bodaboda huku wanafanya kazi zingine.
Mkuu hapo Ni Maisha yanamfanya yanavyotaka!Mfano wa kuigwa, sio kila siku kulia lia na kulaumu tu, kumbe maisha yako unayo wewe mkononi mwako, yaani wewe ndiyo unatakiwa kuyafanya unavyotaka na si kusubiri hisani kutoka kwa mwingine
Shukrani kwa maelezo DoonMaana ya kujiajri ni "kama walivyofanya kina" fulani.
Mkuu hapo hujatoa tafsiri ya kujiajiri bali umeelezea hisia zako tu.
Hata hivyo ni haki yako ya kikatiba kujieleza.
Kingine sidhani kama ni fair kujudge sustainability ya biashara kwa kuangalia business structure.
Kama business structure ni determinant ya sustainability ungetueleza kwa nini makampuni mengi tu yenye wafanyakazi kibao yamekuwa yakideclare bankruptcy kila kukicha.
Suala la mtu kulala na biashara kulala ni disadvantage tu ya hiyo business structure ila hatuwezi hitimisha ya kuwa biashara zote zenye status hiyo sio sustainable kwa sabb mtu atalala.
Na ndio maana kuna wafanyabiashara wengi walianza ktk status hiyo, na sasa wana makampuni yaliyoajiri watu wengi and sustainable.
Hivyo business sustainability ni zaid ya structure, kuna suala la malengo, mipango, mikakati, risk management n.k
So hata huyo binti ana equal chance ya kuwa sustainable endapo akifuata business sustainability principles regardless of her business structure kwa sasa.
Wanabodi tuelezane kweli kuhusu ajira kwa wasomi. Ninawafahamu vijana wana masters lakini ni mama lishe na mwingine dereva daladala na wamejisali Recruitment portal ya utumishi ni miaka [ Recruitment Portal ] !Uko sahihi huyu kapoteza muda wake bure kupata hizo digrii 2. Hata std 7 wanaendesha bajaj vizuri tuu so hakuna la kujifunza hapo. Halafu M&E officer kwenye NGOs inalipwa laki 4?? Ninafahamu watu wengi tuu wanalipwa 1.5 to 2M kwa hiyo post, labda alishindwa kujiuza kwenye interview... Halafu kama alifikia kwenda hadi China but still akashindwa kuwa na duka kubwa la nguo hiyo nayo inatia shaka. Watu wengi tuu wana bajaj mpaka 3 na bodaboda huku wanafanya kazi zingine.
Ada alilipiwa na
Mtu anawezaje kuvuka mpaka wa mawazo yake bila msaada wa mwingine kama si Mungu kumsaidia ?Shahada mbili boss ni elimu kubwa sana kuja na mawazo ya kuendesha bajaji kwakweli lazima jamii isikitike na wale waliokupa pesa ya kwenda shule watamwaga machozi
Pitia uzi kusoma maelezo. Asante !Ada alilipiwa na nani?
Mkuu unadhani kumiliki biashara au company kubwa unadhani ni kitendo cha kuibuka tu?Na hawa ukiangalia ni watu waliojiajiri kupitia taaluma zao, Mimi natamani sana kujiajiri Niwe Mkandarasi au niwe na Consultancy Firm, hapo sitokuwa nilipoteza muda wa zaidi ya miaka 18 ya kutafuta Elimu. Lakini mtu kasoma leo ni Daktari kesho tukute anachoma Mahindi afu tushangilie eti kajiajiri huu utakuwa uendawazimu kabisa
Naye msomi mwenye shahada ya utawala inabidi aige kwa watu wengine kuzaa kwa mpango, hao watoto watatu wanaonekana wanatofautiana umri wa chini ya miaka miwili.View attachment 1660302
Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.
Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.
Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.
Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.
Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).
Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.
“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.
Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.
Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili
View attachment 1660415
Dah...isije kuwa ni mdada wa Macumb Show [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huko siyo kujiajiri bali ni kuganga njaa tu.
No any sustainability
Ana utofauti gani na walioishia darasa la 7B?maana hata walioishia darasa la 3B pia wanaendesha bajajiMfano wa kuigwa, sio kila siku kulia lia na kulaumu tu, kumbe maisha yako unayo wewe mkononi mwako, yaani wewe ndiyo unatakiwa kuyafanya unavyotaka na si kusubiri hisani kutoka kwa mwingine
Hongera yake. Hope kwa hayo mapato atajipanga afanye kitu kingine bora zaidi.
Mungu akamsimamie