Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Vyema angeeleza utofauti wake kibiashara na wale waliomaliza la 7 wakaanza kuendesha bajaji?.What's so different , hapo ndo usomi wake utaonekana ila kama anapark tu barabarani na kusubiri abiria like others do sidhani kama ni kitu cha kutangaza sana.
Nampongeza kwa uthubutu wake, kuweka pembeni vyeti na kusaka shekeri kwa nguvu zote.
 
Hata kuendesha Bajaj Ni kitu Bora.
Kuingiza elfu 50 kwa siku sio Jambo dogo
Kweli kabisa mkuu. Lakini ujue shida ya hizi kazi ni asipoamka hakiingii kitu.
Ila nadhani kwa hicho kipato anaweza kuwa nazo kadhaa akazigawa yeye akawa anakusanya mapato ama akaanzisha/akafanya kitu kisichomhitaji yeye kuwepo physically ill kiende.
 
Hapo uenda ana nyumba yake.
Na vimradi vingine hatuwezi jua.
Ila kwa siku kuingiza elfu 50.
Ni hela nyingi sana.ni zaidi ya kuajiriwa.
Kweli kabisa mkuu. Lakini ujue shida ya hizi kazi ni asipoamka hakiingii kitu.
Ila nadhani kwa hicho kipato anaweza kuwa nazo kadhaa akazigawa yeye akawa anakusanya mapato ama akaanzisha/akafanya kitu kisichomhitaji yeye kuwepo physically ill kiende.
 
tayari mbona wasomi kibao tunatembeza mitumba, tunauza saa,Katanga,ubuyu nk
 
Jambo la aibu sana!

Jitu na madigrii yake linaendesha bajaji- ati na serikali nayo inajivunia!!

Serikali inatumia mabilioni ya fedha kusomesha watu ambao wanaishia kuwa bodaboda!! NA WANAFIKIRI WAKO SAWA?

Propaganda za ajabu sana! Ujanja ujanja wa kisiasa tu huu hakuna la kujifunza hapo!

Wameshindwa kuwasaidia vijana, badala yake wameamua kuja na propaganda uchwara!

AIBU! AIBU! AIBU! AIBU! AIBU! AIBU!
 
-kuna wadau humu wanadai huyo 'Madam Mwasu' ni mtu wa kitengo
-Lakini pia angalieni degree alizosomea Sociology and political science, MA public administration hizo zimejaa sana mtaani.
 
Na hili gazeti la mwananchi wanafeli sana, badala ya kutuletea emerging youth billionaires watu wawe inspired, tunarudishana kwenye udereva wa bajaji
Huyo kawekwa particularly ili bajaji ionekane kawaida kwa wasomi ... Mshushe munkari degree 1 muendeshe hata boda boda..
 
Hongera zake hapo baro kuna gaps kadhaa ningependa kujua alipitaje , mf kutoka kuchuuza nguo za kariakoo Hadi kwenda china
 
Kwahyo kasoma ya kwanza..akahis akiongeza gamba atapata ajira,,akaongeza ya pili holaaaa..duh..akaamua kuwa dereva tu
 
-kuna wadau humu wanadai huyo 'Madam Mwasu' ni mtu wa kitengo
-Lakini pia angalieni degree alizosomea Sociology and political science, MA public administration hizo zimejaa sana mtaani.
Umeongea pointi ya msingi Saveya ! Labda akaombe kazi kwenye vyama vya siasa tena kwa kuanza kujitolea.
 
Vyema angeeleza utofauti wake kibiashara na wale waliomaliza la 7 wakaanza kuendesha bajaji?.What's so different , hapo ndo usomi wake utaonekana ila kama anapark tu barabarani na kusubiri abiria like others do sidhani kama ni kitu cha kutangaza sana.
Nampongeza kwa uthubutu wake, kuweka pembeni vyeti na kusaka shekeri kwa nguvu zote.
Dunia ya sasa kuna kauli kwamba "hapendwi mtu bali Pesa" ! Vijana wasomi katika maisha ya leo tafuteni pesa kwa njia halali msiabike mitaani.
 
Shahada mbili boss ni elimu kubwa sana kuja na mawazo ya kuendesha bajaji kwakweli lazima jamii isikitike na wale waliokupa pesa ya kwenda shule watamwaga machozi
Mkuu imagine wewe wazazi wako ni masikini then huku uwe na elimu kubwa kama hiyo na ushamaliza chuo.
Na unataka kumiliki company kubwa utafanya nini ili ufikie plans zako?

Utaamka tu kitandani na umasikini wako then pop up unamiliki company?

What would you do?
 
Tungekuwa tunajua future zetu wengi tusingehangaika na Chuo Kikuu. Usomee uhandisi hadi upate degree halafu uiweke pembeni uanze kilimo cha matikiti?? 5 good years wasted!!! Bora mtu ungejua mapemaaaaa na kuanza mara tu baada ya kumaliza form 6
Then uko tayari kuwa tegemezi maisha yako yote kama usingekuwa na ajira au kama usipopata ajira?
 
Back
Top Bottom