Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Mi nina kauli mbiu yangu kuwa"kuwa na elimu ni jambo la Kwanza,la pili lazima na ni lazima uitumie elimu uliyonayo to the maximum huwez nambia una masters afu unachowaza kichwani ni udereva bajaji na umeridhika kabisa haya ni matumizi mabaya ya elimu"
mimi kama cheti changu ninacho nitapambana kama nilivyopambana kusoma nipate kazi sio huo udereva

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
What would you do if hutopata kazi?
 
Kujiajiri ni kama walivyofanya kina Mendes wa KopaGas, MakJuice, Wasafi media, Maxence Melo wa JF.

Ni kampuni sustainable, ambazo unaweza kujua kabisa zitaajiri watu, kukuza kipato na kuvutia uwekezaji hata kama ni kupitia DSE.

Sasa yeye biashara ya Bajaj, akilala na yenyewe inalala.
Are you trying to say hao wote waliibuka tu kutoka kwenye makochi ya wazazi wao au shemeji then boom wanamiliki company au business kubwa?

Just like that.
 
What would you do if hutopata kazi?
Ntapambana kimyakimya bila kujisifia magazetini sababu ntakua sijatimiza malengo ya elimu yangu , siku nikitoboa sasa nimejiajiri kwenye fani yangu ndo natoka sasa kuwainspire vijana wa kada yangu na kuwaaajiri pia.
Nisipotoboa nikaishia kwenye bajaji nakaa kimya ili nisiwavunje moyo vijana wengine wakaona elimu haina maana.
 
yani kesho kutwa awe na bajaji kumi???acha ulongo field sio kwepesi kiasi hicho ni ngumu na itachukua muda
Mkuu are you even serious.
Unadhani mtu akiandika kesho kutwa basi ni kesho kutwa amemaanisha?

Umejuaje kama field ni kugumu kama hata wewe mwenyewe na hujawahi hata kujaribu?

Have you ever try to do anything like that?
 
View attachment 1660302

Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.

Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.

Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.

Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.

Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).

Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.

“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.

Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.

Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili

View attachment 1660415
Ni kujisifia ujinga ujinga tu, Hivi kwa kiwango cha elimu alichofikia alipaswa kuwa dereva wa bajaji? Au ni changamoto ya maisha ndio yamesababisha kujiingiza kwenye kazi ambayo haindani na fani yake? Elimu aliyosoma haijamsaidia chochote bali kumfilisi tu , so mnataka kutuambia si ni bora asingesoma na kuanza kuwa dereva wa bajaji?.
 
Ntapambana kimyakimya bila kujisifia magazetini sababu ntakua sijatimiza malengo ya elimu yangu , siku nikitoboa sasa nimejiajiri kwenye fani yangu ndo natoka sasa kuwainspire vijana wa kada yangu na kuwaaajiri pia.
That's good mkuu.

As i can see tatizo ni kuona aibu na mtazamo wa kijamii pia muda waliotumia shule na kutokujua lengo la elimu ndio vyanzo vikuu kwa vijana na watu wazima wengi wenye elimu kushindwa kutumia elimu zao kuanzia chini hiyo inapelekea kuwa na zero execution hivyo zero progress na kuendelea kubaki masikini au kusubiri kuajiriwa huku wakiendelea kuzeeka mategemzi kwa wazazi na mashemeji.

They want big things kwa kushtukiza kitu ambacho impossible in reality na kitaendelea kuwa possible in imagination.
Wanataka vitu vikubwa bila kujua chanzo vya hivyo vitu vikubwa mwisho wanaishia kubaya kwa kupenda shortcut.

That's why wanaponda humu bila kujitambua.

Kingine ni huyo dada kufanya hivyo ni dalili tosha kwamba hajari opinions na perspective za broken society like hawa humu.
Hana hali ya kuwa na aibu wala kuwa inferior na bila shaka atafika malengo yake kuanzia chini.

Huyo dada ni jasiri kuliko asilimia 98 ya graduates wote haijarishi wakiume au wakike.

All in all mfumo wa elimu ni vizuri ubadilishwe ili kuondoa mindset za aina kwa vizazi vijavyo.
 
Kweli mkuu, mtu amesoma shahada ya kwanza hola ya pili anakuwa dereva bajaji.
Hana cha kuwa mtu wa mfano.
Imagine wewe ni masikini then uwe na elimu kubwa na ushamaliza chuo considering una plans za kumiliki company.

Ungefanyaje?
 
Ujinga huu nao niwakujivunia?? Master unaenda kuendesha bajaji?? Kweli? Elimu yetu ni ya hovyo sana, badala ya kwenda kutatua changamoto za kijamii na kuja na kitu kipya kama msomi, unakwenda kuendesha bajaji na na yule wa shule msingi atafanya kazi gani?
Wewe kama kweli elimu uliyosoma imekuelimisha basi jibu hilo swali.

Imagine wewe ni mtoto wa masikini then umemaliza chuo.
But una ndoto za kumiliki company kubwa itakayo tatua changamoto za kijamii.

Hapo wewe utafanyaje as mtoto wa masikini ili utimize hizo plans?
 
What would happen if kila mtu angeajiriwa?
Unakurupuka. Mimi sina tatizo mtu kujiajiri.

Ila alivosema amekosa ajira na ana masters hapo ndo nikataka kucomment.

Angesema kua mayb mshahara mdogo ndo mana nimeamua kujiajiri sawa....ila kasema amekosa ajira tena ana hiyo masters....hapo tatizo lipo maana kazi zinatangazwa wenye uwezo wanapata bila kujuana na watu.

Sawa kazi ni chache ila if you are good...hukosi kazi unless uwe umejambiwa....

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Ntapambana kimyakimya bila kujisifia magazetini sababu ntakua sijatimiza malengo ya elimu yangu , siku nikitoboa sasa nimejiajiri kwenye fani yangu ndo natoka sasa kuwainspire vijana wa kada yangu na kuwaaajiri pia.
Nisipotoboa nikaishia kwenye bajaji nakaa kimya ili nisiwavunje moyo vijana wengine wakaona elimu haina maana.
Kumtangaza magazetini isha mpa popularity, anaweza pata wateja wengi zaidi.Hata ikitokea kazi hutaweza kupambana nae, tayari ana confidence.Kufahamika kuna faida zaidi kuliko hasara.
 
Masters degree ili uje uendeshe tri- cycle? Ni uharibifu wa raslimali fedha na raslimali muda
 
Ukitaka kujua mfumo wetu wa elimu ni mbovu na unazalisha wajinga ni hizi comments za humu.
Siungi mkono kuendesha bajaj ila kwa masikini hata uwe na PhD huwezi kuanzisha au kufanya vitu vikubwa bila pesa ya kutosha.
Hivyo ni lazima uanzie chini no matter what kama una nia ya kufanya vikubwa au nenda kaajiriwe kama mfumo mbovu wa elimu na jamii kama humu zinavyosema.

Mnajua ana plan gani au ana wekeza nini kwenye hicho anachokifanya?

Kama wewe ni masikini au kwenu hamjiwezi na wewe una elimu kubwa pia una ndoto za kumiliki vitu vikubwa na hutaki kuanzia chini.
Basi endelea kubaki hapo kwa wazazi au shemeji na uendelee kuota hizo ndoto au uendelee kusubiri ajira huku unazeeka.

Kama mnayoandika haya mmesoma basi elimu zenu ni useless pia mfumo wa elimu ubadilishwe mara moja sababu unatengeneza watu ambao ni dreamers, delusional and useless sababu hakuna execution katika chochote wanachosema.

If everything is that easy as you think then you shouldn't be where you are right now.
Hivi umetafiti kuwa mfumo wa elimu yetu haufanani na nchi zingine? Kozi za sociology hazijatungwa ulaya kwel? Political science!! Unataka afundishwe nii ambacho PS haijamfundisha.
Hivi katika dunia ya utandawazi unalaumu mfumo wa elimu huku utandawazi unakupa chance ya kujifunza chochote kilicho kosekana kwetu? .
Naweza kukuunga mkoni kwa upande wa sayansi kwa sababu teknolojia inabadirika kila kukicha, vilevile zinatakiwa maabara za kisasa kuendana na teknokojia ila sio kozi za ART muilamu serikali hapan.
Tunifunze kutumia teknolojia kufidia gepu, halafu to a mbadala elimu iboreshwe nini sio lawama tu.
Lawama ni dalili ya kushindwa.
 
Back
Top Bottom