Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Mfano wa kuigwa, sio kila siku kulia lia na kulaumu tu, kumbe maisha yako unayo wewe mkononi mwako, yaani wewe ndiyo unatakiwa kuyafanya unavyotaka na si kusubiri hisani kutoka kwa mwingine
Ni Jukumu la lazima kwa serikali kuajiri watu wake au kuwasaidia wajiajiri. Na wanalipwa pesa za walipa kodi kwa sababu hiyo.

Kama wameshindwa kufanya hilo, wap8she wawaachie wanaoweza.

Huwezi kumlipa mtu alime barabara upite, pesa anakula kila siku halafu anakwambia tatizo lako boss hutaki kujiongeza kulima tu mwenyewe upite.

Na wakati huo huo, hataki kuachia hiyo tenda ya kutengeneza barabara.

Wanachokifanya watawala ni kutafuta namna ya kukwepa wajibu wao ili watafune kodi za walalahoi bila kufanya kazi wala kupigiwa kelele.
 

Hivi elimu ya Tanzania ina ubora gani? Kiwango cha wasomi wetu kutatua changamoto mbalimbali za kimaisha kiko dunia

Nancy Lema ni msomi wa Elimu ya Masters ya Project Management Chuo cha SAINT MARY’S UNIVERSITY OF MINNESOTA Nchini Marekani na ameishi Marekani kwa miaka 10, mwaka 2015 aliamua kurudi rasmi Tanzania na kwenda kwao Mwanza na kuanza kutafuta kazi kwenye Makampuni bila mafanikio ndipo akaja na wazo la kuuza chakula aina ya makande kwenye ofisi Mwanza.

“Nilijua nimemaliza Masters yangu nakuja Tanzania kutafuta Kazi haitakuwa ngumu lakini kila sehemu niki-apply naambiwa subiri kwanza ilinifanya nifikirie nini cha kufanya” Nancy Lema

” Wazazi wangu hawakukubliana na mimi nianze kupika wakati wamenisomesha walitegemea niwe Meneja Kampuni flani na elimu kubwa, Ila kwa sasa ndio Wateja wangu wakubwa” Nancy Lema


Dada huyu msomi naye gumzo kwa kutafuta pesa bila kujali elimu kwani anaelewa nini maana ya neno moshi kwa wachaga !
 
Umeandika Mambo mengi Sana mimi nimesoma kichwa Cha habari na aya ya kwanza....

Binafsi sitarajii wasomi wa degree mpaka masters kuja na idea cheap Kama izi....

Ukiamua kua boda boda au dereva wa bajaji na degree yako au masters.... Just shout your mouth....

Hizoo Kazi za Bajaji au boda boda.......
Ange zianza MIAKA kumi iliyo pita pengine angekua mbali huo muda alio Soma na kutesa akili na kujibu assignment na quiz na test, UE Mpka kuvaa Joho sio lelemama....

Tunataka aje na wazo jipya la kiutendaji kwenye bajaji.......

Kwa watu wenye ELIMU za vyuo vikuu then kuja kufanya Kazi za vibarua vya zege haikubariki

Otherwise Kama ni ku survive maana kweny MAISHA Kuna point unafika the only thing you need is just to survive...


Aluta continue kwa vijana wote....
Informal sector
wanao pambana all over the World........
 
Tatizo la kutoajiriwa ni janga kwa kizazi kipya tofauti na karne iliyopita; hata kwa mataifa makubwa duniani.
 
Daa hiv amna mtu mwenye Namba Ya Jiwe Nimcheki ........!!!!

Maana sijui tunaenda wap!! Nahtaj kumuuliza tu:

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Jambo hili linaonyesha Elimu yetu sisi haina msaada wala thamani yeyote, na hii inawakatisha tamaa sasa Walio ngazi za Chini kama mtu aliyeishia darasa la Saba anaweza kuendesha Bajaji kwanini upoteze Pesa na muda kusoma shahada mbili afu uje uendeshe bajaji? Jibu ni kwamba Dada anafanya kazi hiyo ili asukume siku baada ya kukosa mazingira ya kumfanya atumie Elimu yake.

jambo Hili sio la kujivunia hata kidogo, kwamba Taifa linasomesha watu ambao haliwezi kuwatumia wala kuwasaidia kutumia ujuzi wao, Dada huyu angejiajiri kupitia taaluma yake ningemuelewa sana. Kujiairi sio vibaya lakini kuajiriwa pia sio vibaya kwasababu ni ukweli uliowazi kwamba hatuwezi sote kujiajiri hiyo haitokaa itokee. Ni vema viongozi watafakari tulipojikwaa hali ikiendelea hivi hakutakuwa na maana ya kwenda Chuo kikuu kabisa
 
Na hawa ukiangalia ni watu waliojiajiri kupitia taaluma zao, Mimi natamani sana kujiajiri Niwe Mkandarasi au niwe na Consultancy Firm, hapo sitokuwa nilipoteza muda wa zaidi ya miaka 18 ya kutafuta Elimu. Lakini mtu kasoma leo ni Daktari kesho tukute anachoma Mahindi afu tushangilie eti kajiajiri huu utakuwa uendawazimu kabisa
 
Umesema kweli Granite
 
Kuna jambo anatuficha , kafanya kazi za NGOs tangu 2009

Kama mshahara ulikua mdogo ada ya kusoma masters na pesa ya kujikimu alipata wapi ?

Kwa position alizotaja kufanyia kazi napata mashaka na huo mshahara aliotaja

Namalizia , kuna jambo anatuficha

Lakini kuhusu biashara nadhani ni suala la kuyumba kiuchumi tu limetokea maana inaonekana tayari alikua na biashara kubwa ya nguo
 
Hivi kweli UWEZO WETU , wasomi kiwango hata cha diploma, hatuwez kubuni bali kuvamia idea iliyobuniwa na std seveni,? " hii inasikitisha Sana Sana, ina maana IRR(internal rate of return) kwa serikali KUWEKEZA kwenye elimu linakomea kumonitor kutoa tu mikopo, baada ya kumaliza tu biashara imeisha, kuna haja ya mfumo yetu iliangalie hili, kama Kweli msomi nguri kama Huyo anafaa ku-compete Sokoni na wale less than std seven?. Mr.einstern, amewahi sema,"UKIOONA MWANAFUNZI wako hajaelewa, jua wewe una mbinu kidogo na uelewa mdogo kumuelimisha MWANAFUNZI". Naona hili si tatizo la Wanafunzi bali mfumo, kwani same class mmoja anaajiliwa Kampuni A, anafanya vizur, mwingine analaumiwa kwasabab tu mazingira yake sio rafik. !! ".Stefan's Law of black body, alisema, temperature flow from high concentration to low temperatures under certirice per bus" aliimanisha, kuwa joto litatoka palipo na joto kubwa kwenda palipo na joto kidogo, hivyo chenye joto kubwa kitapoteza HARAKA joto lake, ,namuona msomi Huyu akipoteza uwezo wake wa KUFIKIRI kwani anaokutana nao kwenye maeneo yake ya kazi ni std seven (low temperature) kifikra, hivyo atajikuta anafanana nao, Na kuwaza level moja. Siku tukioona msomi mmoja kuwa kundi lisilo lake ni tatizo la sote basi TUTAWAZA SAWA.. iam not voting this kind of entrepreneur as appropriate to be promoted as a legacy to the rest of university graduates.
 
Ana bima ya afya?
Ana nssf?
Akizeeka ataishije
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…