Ingekuwa hekima kama wangeanza kwa kuukemea "ugaidi" uliotendwa na Hamas ndipo waikemee Israel. Kwa kuikemea Israel bila kuonesha kukerwa na ukatili uliotendwa na Hamas kunaweza kutafsiriwa kuwa ni upendeleo wa wazi.
Hamas waliwaua raia wasio na hatia, wakiwemo watoto. Inasemekana miongoni mwa waliouwa, kuna raia wachache wa kigeni. Kwa hiyo hata Watanzania wangeweza kuingia katika hiyo kadhia kama wangekutwa na Hamas maeneo waliyoyavamia.
Hao raia waliouawa walikuwa na kosa gani? Kama Hamas walikuwa na hasira na Serikali ya Israel, si wangevikabili vyombo vya dola kama Polisi na Jeshi la Ulinzi?
Waliwateka na wengine, si Wayahudi tu, bali hata raia wa Mataifa mengine.
Japo silaha za kivita hazimtofautishi raia na askari , lakini alau kidogo, Israel wameonesha ustaarabu kwa kutoa tahadhari juu ya maeneo wanayoyavamia, hivyo wahusika wanaweza kuchukua tahadhari. Ni tofauti na uvamizi uliofanywa na Hamas.
Kwa mtazamo wangu, tamko halijabalance. Limekaa kiuonevu.