WADANGANYIKA bwana, si unaona wameanza kusahau.....?
Juzi juzi tu hapa walikuwa wanasema Kikwe hafai, leo wameanza eti maandamano ya kumuunga mkono kuchukua fomu.
Ubongo wa Taifa hili umeoza. Hivi wasomi wa nchi hii, na ninyi wanafunzi mlio vyuoni. Tafakarini mkaelewe, ni lini mtakubali KUACHA kutumiwa ili kufanikisha ajenda za watu fulani kisiasa? Si ni ninyi mlikuwa mnalia ukata wa Mikopo ya Elimu ya juu? Si ni ninyi mlikuwa mnalia mishahara ya wahadhiri haitoshi? Si ni ninyi mlikuwa mnalia na kulalama kuwa elimu ya siku hizi ni majengo tu, ubora haupo ( shule kibaaaao za kata zimejengwa lakini hazina huduma muhimu kama maabara, maktaba, vitabu, waalimu wakutosha n.k). Jamani tutafika kwa mwendo huu?
Ama kwakuwa mnategemea kupata chochote kwa takrima ndo mnaanza kusahau majanga na majonzi yaliwasibu kwa miaka mitano inayokamilika mwaka huu?
Mimi nasema, historia, umaskini wowote uliosababishwa na utawala huu wa awamu wa nne, vifo, majonzi, vilio, masikitiko, mashaka VIWE JUU YA VICHWA VYENU NA NYUMBA ZENU! Kama mmeshiriki kwa namna yoyote ile, na iwe LAANA juu yenu!
Ninyi kama wasomi mmeshindwa kulisaidia taifa lenu, na kwa mantiki hiyo, jamii hii haiwahitaji na inajuta kujinyima ili kuwasomesha, inasikitishwa, inafedheheshwa kwa kupoteza lengo kwenu, tazama sasa mwazigeukia faraja na za kitambo kidogo tu wakati wa uchaguzi: Pesa, pombe, ahadi za nafasi nzuri n.k na kusahahu machungu na huzuni nyingi mlizozivumilia katika miaka mitano iliyopita na sasa mpo tayari kufanya makosa yale yale!
Jamani, tunazungumzia maisha ya watu na kesho yao na vizazi vijavyo! Mbona mnaanza kuchukulia rahisi rahisi tu? Kama hatuna upendo kwa watanzania wenzetu, basi tuwe japo na UTU wa kutambua kuwa japo keki hii ya Taifa ni ndogo, tuigawane kwa usawa na haki!