Katika kupita pita huko kwenye mitandao ya kijamii nilikutana na clip ya chawa mmoja wa CCM akiwakebehi walimu wa vyuo vikuu nchini.
Inasadikiwa walikutana walimu wa vyuo vikuu mia moja ili kujadili juu ya kesi inayomkabili mwenzao wa Udom.
Michango ikapitishwa na kilichopatikana ni sh laki tano.
Chaww huyu anadhihaki walimu wa vyuo vikuu mia moja kuchanga laki tano tu.
Hii inaonyesha msomi na mtu muhimu kwenye taifa hili hana thamani mbele ya jamii. Ila CCM inawathamini machawa kwa udi na uvumba
Kufikiri usomi ni utajiri ni ulimbukeni.
Kuna watu si matajiri kwa sababu ni wasomi. Wana ma principle ya kukataa mapesa kijamaa jamaa kama Nyerere.
Nyerere alistaafu masikini ukiondoa zawadi za serikali na watu. Hata nyumba ya Msasani alioewa zawadi. Akajengewa nyingine Butiama zawadi.
Akafanya kazi South to South Commission baada ya kustaafu. Mwisho wakampa kama dola za Kimarekani laki tatu, siku hizo oesa nyingi, kama shukurani. Yule Mzee alizikataa zile pesa. Akisema ni nyingi sana. Mpaka wale wakina Butiku wakamwambia zichukue tu kama wewe huzitaki unaweza kuzigawa kwa watu wenye uhitaji. Ndiyo akazichukua.
Yule Mzee hakutaka pesa, yeye alitaka control tu. Ukiwa na sura yako kwenye pesa unaona pesa kitu cha kawaida tu 😂
Halafu jamii yetu haina amana, watu wanaweza kuwa wanachangiana wenyewe kwa wenyewe bila ya kujiandikisha, kwa sababu ukijiandikisha list inaweza kupitiwa na wasiojulikana ikakupa matatizo, hususan kama ni ntumishi wa umma.
Kuna jamaa alikuwa anafanya kazi benki Dar, aliachishwa kazi kwa sababu alimchangia Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi, jina lake likawa kwenye list. Jamaa ilibidi auze vitu vya nyumbani na kuwatoa watoto shule za English Medium. Kwa sababu ya list.
Pia, katika jamii yetu, kwenye kuchangishana, ukijionesha umeweza kuchangisha pesa nyingi ni kama unawavunja hamasa wengine wasichangie, mchango unatakiwa kuonekana haujatimia na una hatari ya kutofikisha kengo ili watu wengi zaidi wachangie. Mimi nilikuwa nashangaa michango inaitishwa mimi nataka kumaliza naambiwa usimalize kwanza. Labda wasomi ndio wametumia mbinu hizi za Watanzania.
Sasa wakwambie wamechanga mamilioni halafu waulizwe hela wamepata wapi na wao watumishi wa umma mishahara yao inajulikana?
Kuna mchango mmoja ulioita, Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati huo akachanga laki moja, nikashangaa sana, mbona Waziri Mkuu kachanga kidogo?
Nikasema angechanga nyingi tungehoji kapata wapi pesa wakati yeye hana biashara ni mtumishi wa umma tu?