Ipo hvi mkuu..
Kwanza mwizi hawi mmoja....lazima wawe zaid ya waili.
Kinachofanyika... Kwanza wanapima akili ya wakala, usiniulize wanapimaje.
Wakishajua hilo ndo wanasuka mipango....wanaenda kwa wakala wakiwa watatu au wanne ndani ya dkka 1 wote wanakuwa washafika kwa huyo wakala...wataomba huduma mbalimbali ukiwa busy kuwahudumia mmoja anaeweka atajifanya anaharaka sana au amesahau namba, sasa wakala anapotaka namba ya mteja ili amtumie pesa yule mteja anamwambia lete simu nikuandikie chap, wakala anampa akiamini password hazijui mteja.
Apo ndo game inachezwa ndani ya sekunde 30 sio dakika ni sekunde.
Jamaa anachofanya ni kukanseli menu... Na kusevu namba zake kwa majina ya mpesa, au tigopesa sana sana wanatumiaga mpesa au Airtel money na kuangalia balance la muamala wa mwisho wa wakala alioufanya....afu anarudi tena kwenye menu ya uwakala na kuweka namba yake anayotaka ipatiwe huduma.
Kumbuka ndani hzo sekunde 30 kuna jamaa wengine wanamkeep busy wakala.
Baada ya apo wanaondoka.....sasa anakuja mwengine kutoa pesa kwa kuifowadia msg ile namba iliseviwa mpesa au Airtel money.....kumbuka wezi wana final balance yako so kama ulikuwa na balance 100, 299 anaekuja kutoa anatoa 1,500,000 na balance wanaedit lisome 1,600,299.... Akitoa wakala anaangalia juu anaona mpesa akiangalia balance limeongezeka anatoa cash na apo ndo anakuea ametapeliwa.
Na atakuja kugundua adi atakapo taka kuitoa hyo pesa....anakuta balance halitoshi na apo kuja kugundua kama kuna namba iliseviwa adi akague vzuri simu yake.