Wasomi wengi na wanaopenda elimu wanamuunga Tundu Lisu kugombea uenyekiti. Upande Ule wengi wao Elimu Yao ni tiamaji tiamaji.

Wasomi wengi na wanaopenda elimu wanamuunga Tundu Lisu kugombea uenyekiti. Upande Ule wengi wao Elimu Yao ni tiamaji tiamaji.

Habari Wakuu!

Ukifuatilia kwa umakini uchaguzi huu. Utagundua Wasomi wengi na watu wanaopenda elimu wengi wao wanamuunga Mkono Tundu Antipas Lisu kuwa Mwenyekiti.

Hii ni tofauti na upande wa pili ambao wengi wao hata Elimu yao ni yamashaka, Elimu ya kuungaunga, huku wengine wakiwa wamekimbia shule na hawaamini katika shule.

CHADEMA zamani kidogo walikuwa wanasifika kwa kuwa na vijana wengi na Wasomi wengi.

Kwa kupenda Elimu, ndio wakaleta Ile Sera ya Elimu bure kuanzia shule ya msingi Mpaka Chuo kikuu ambayo baadaye CCM waliichukua wakafanya Elimu bure shule ya msingi Mpaka shule ya sekondari.

Sio ajabu wanachama wengi wa CHADEMA waliohamia kwenda CCM iwe Kwa kupenda kwao au kushinikizwa Elimu Zao zilikuwa za uhakika. CCM walifanya usajili muhimu kuchukua vijana wa CHADEMA na kuwatumia katika shughuli zao za kiserikali.

Mwenyekiti Mbowe ikiwa atashinda itampasa ajitafakari, ajitathmini kwa nini vijana Wasomi haswa, yaani vipanga na wenye fikra kubwa hawamsapoti yeye na badala yake walimsapoti Tundu Lisu

Huwezi kuzungukwa na Watu wenye upeo WA Kati au UPEO mdogo alafu wakati huohuo wenzako CCM wanavijana maelfu kwa maelfu ya Wasomi WA uhakika ambao wapo kuwatumia na kuwalinda kivyovyote.

CHADEMA ili iende mbele inahitaji watu. Lakini katika Safu ya juu lazima wawepo watu wenye akili kubwa na elimu ya kidunia isiyotia mashaka, au Elimu ya kudunduliza au kuungaunga.

Kisha inahitaji watu wenye misimamo mikali, wazalendo, Jasiri na ambao wapo kwaajili ya mabadiliko ya kweli.

Ukifuatilia hata huku mitandaoni, Wanaomuunga Mkono Lisu wanauwezo Mkubwa wa kiakili, kujenga hoja, na elimu zao sio za kuungaunga. Na wanapenda Elimu na mabadiliko chanya

Moja ya dalili ya mtu mwenye AKILI, UPEO na ELIMU ni kukubali mabadiliko chanya.

Karibuni kwa mjadala
Umepiga kwenye mshono kabisa imagine simbilisi kama Yericko Nyerere ndiyo wapambe wa Sultan Mbowe
 

Attachments

  • GfMNLpyXYAA8ucg.jpeg
    GfMNLpyXYAA8ucg.jpeg
    58.9 KB · Views: 2
Sema wanaharakati wasaka tongue ndio wanaomsapoti bwana roporopo
 
Hapa Tanzania tofauti inaonekana kuwa huyu ana vyeti na huyu hana... ila nje ya vyeti na picha za siku ya graduation watanzania wote tunafana akili tu
 
Sema wanaharakati wasaka tongue ndio wanaomsapoti bwana roporopo
Wasaka tonge wanamshabikia Mbowe kwa vile anawatupia makombo,tofauti na wanaomfuata Lissu wanafuta misimamo yake ambayo inaweza kuinasua Chadema kwenye mkwamo iliopo nao kwa sasa. Lissu hana hela ya kugawa kama sadaka.
 
*TAL akifanikiwa kushinda uchaguzi huu,nimuoa Binti wa Kinyatur... *
 
Mbowe haungwi Mkono na Wasomi wengi.
Mfano, wote waliojitokeza kumuunga Mkono Mbowe hadharani Elimu Zao ni ushahidi tosha.

Alafu linganisha na Wanaomuunga Mkono Lisu



Mtazamo wako upo kinyume Kabisa na Hali Halisi.

Tukija kwenye uhalisia, unafikiri ni Kwa nini maeneo yenye watu wengi waliosoma hapa nchi yameendelea kuliko ambayo hawana Elimu?
Alafu bado useme waliofeli shule wamefanikiwa kuliko waliofaulu.
Tatizo lenu mnadhani waliofaulu ndio wenye upeo, kumbe kuna watu kibao wana uwezo na darasani hawakuwa bright.

Maeneo gani yameendelea, kwa viwango gani mkuu. Bado hii ni shithole country, hatuna maendeleo yoyote ya kupigiwa mfano, najua utazitaja Moshi nk kama mifano yako, ila kwangu bado sana.
 
Pia kuna upande unaamini siasa ni kumsema vibaya mwenzako mitandaoni ikiwemo elimu yake, wakati upande mwingine upo kimya, wala haumshambulii mgombea mwingine kwa kejeli, bali upo diplomatic zaidi ukiheshimu sifa za elimu zilizobainishwa na katiba iliyotungwa na pande zote

Ushambulie ili madudu mengine yaibuliwe?
 
Tatizo lenu mnadhani waliofaulu ndio wenye upeo, kumbe kuna watu kibao wana uwezo na darasani hawakuwa bright.

Maeneo gani yameendelea, kwa viwango gani mkuu. Bado hii ni shithole country, hatuna maendeleo yoyote ya kupigiwa mfano, najua utazitaja Moshi nk kama mifano yako, ila kwangu bado sana.

Huwezi tenganisha maendeleo na elimu.
Huwezi tenganisha maendeleo na akili, ujuzi na maarifa.

Nimetaja makundi zaidi ya matatu.
Mtu anaweza kuwa hakupata Elimu lakini anapenda na kuamini katika Elimu. Hilo kundi hujaliona kwenye post
 
Back
Top Bottom