Pre GE2025 Wassira aihakikishia Marekani uchaguzi kuwa huru na haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Paka anamuhakikishia panya uchaguzi wao utakuwa huruπŸ˜†πŸ€£πŸ˜†
 
Simba ndiye wa kutuhakikishia mchezo wao na Azam utachezeshwa kwa haki na siyo refa wa mchezo? Na Kwa nini kaimu balozi aende kwa Simba siyo kwa waamuzi, kwani Simba ndiye msimamizi wa mchezo?. CCM mjitafakari ni wazi Mtawala wa Dunia kamuelewa Lissu. Baada ya kuongea na kaimu kapteni wa Simba subiri sasa akaongee na kapteni wa Azam. CCM mtanyoka mwaka huu. Kila balozi wa Marekani anayekuja kanyoka kama reli ya SGR.
 
Siyo muda mrefu Trump anazungumzia Tanzania. Yaani Wasira anadhani jamaa wajinga kiasi hicho, eti CCM inahakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki. Kwa hiyo CCM anagombea, anasimamia na kutangaza matokeo. Jamaa hajuhi hata kuongea kidiplomasia anaongea kiwizi kabisa. Shame!!!!
 
Mzee siku izi ameanza kuvaa raba ya rangi nyeusi
 
Kila msimu ndio maneno Yao. Sasa uchaguzi ulio huru na Haki unaamuliwa na chama tawala? Uundaji wa tume ya uchaguzi tayari una reflect hakuna uchaguzi huru. Hv na hao ma beberu mbona wanapenda kutuchora Sana, wanajua kabisa Hilo haliwezekani lakini wanavyosikiliza Kwa maakini utadhani sijui nn
 
Duh, hilo dundo la Kasongo ni bab kubwa.
 
Lisu eti hawezi kuzungumza na Wasira!
Watu wanatoka Marekani kuja kumsikiliza Mzee Wasira na kuchota busara zake, sijui huyu Lisu anayesema hawezi kuzungumza na Mzee Wasira yeye ni nani?!
Mbona Lissu alifafanua?
Alisema walizungumza na mtangulizi wake, yaani mzee Kinana mwaka mzima, matokeo yake hakuna uboreshaji wowote uliofanywa.
Wizi wa kura na mauaji viliendelea kutamalaki kwenye uchaguzi wa 2024.

Wahenga walishasema kufanya jambo kwa namna ile ile na kutarajia matokeo tofauti ni uhayawani
 
Duh, hilo dundo la Kasongo ni bab kubwa.
Aloo jombaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nani kamnunulia mzee dundo la Reebook la kwenda? Yan hili dundo akifika lumumba mlangoni ye yupo nje dundo lipo ndani yani kama kwa ndani kulikuwa na vijana wanagombania posho za uchawa wanakaa kimya mana wanajua mwenyewe kashafika....hii ndula yake nimeikubali sana. Kuna dingi mmoja alishakuwepogi mwalimu tusiime alikuwa anaitwa Mzee Amiri alikuwa anakula Madundo kama hayo, huyu mzee mshabiki wa yanga nlikuwa naenjoy sana nkikaa nae...kila nikiliangalia dundo lake nlikuwa nacheka sana
 

Attachments

  • Screenshot_20250221-103741.png
    421.7 KB · Views: 1
Kama ccm na Wasira wake wanataka tuamini anachokisema, lazima sheria mbovu zinazolalamikiwa zerekebishwe. Uchaguzi huru na wa haki hauji kwa matamko yasiyokuwa na misingi ya kisheria. Hayo hayo yalitamkwa na mtangulizi wake, yaliyotokea mwaka jana kila mtu ameona.
 
Uchaguzi huru na haki CCM hata wabunge watano hawapati
 
Yeye kama nani awahakikishie kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki?
 
Je, ccm ipo tayari kufanya mazungumzo na vyama vya upinzani? Wasira : ndiyo.
Kama ni kweli kuna ugumu gani kwa vyama vyote nchini kukubaliana kuhusu katiba mpya?
Hili swali ni mtego kwa CCM. USA wakiwa na jambo lao huwa wanaanzia mbali sana. Ccm jiangalieni!
 
huu ni ukichaa wa wanasiasa
 
Anayeongea ni makamu mwenyekiti wa chama kitakachogombea,amejuaje kuwa utakuwa huru na haki? Na je tanzania inaihakikishia marekani kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki,je marekani ni nani mpaka ahakikishiwe? Je hamuwezi kujisimamia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…