Wassira: Ieleweke wazi tunapoandika Katiba Mpya Sera ya CCM ni Serikali 2 kuelekea 1 na Siyo vinginevyo

Wassira kaongea ukweli mchungu.
 
Ccm wataiingiza hii nchi kwenye majanga makubwa sana, wenye nchi ni wananchi na Wala sio ccm, wananchi wakitaka serikali tatu hakuna wa kukataa.
 
Katiba ya nchi siyo Sera ya vyama, hao wote hawana akili kichwani.

Tunahitaji katiba ya wananchi siyo ya chama chochote kile cha siasa.
 
Chadema imesetiwa katika wrong footing! It is very vulnerable. Ni mpaka hapo itakaposetiwa kwenye right footing ndipo itakuwa very robust, strong if you like, na reliable. Sitaki maswali, dadavua mwenyewe Nina maanisha nini
Kwa hiyo wewe una akili sana kuliko wengine wakati hata familia tu inakushinda kuongoza?
 

Majadiliano ya zamani kila mara unayaleta haya haya kama ni mahojiano mapya. Huko TBC wanawekaga mambo ya zamani na huyarudia mara kwa mara hadi yanaboa.
 
Watanganyika hawaitaki tanganyika yao...
Sio watanganyika sema viongozi wanufaika ndio hawaitaki !! Watanganyika mpaka wapige kura ya maoni ikisimamiwa na tume huru ndio tutajua kama watanganyika hawaitaki au wanaitaka !!
 
Hakuna Katiba itapatikana Nchii hii. Huyu Mama anawaremba ili 2025 msimsumbue. Akishapita ataambiwa amalize mda wake asepe, mambo ya Katiba hayamhusu..
 

Sasa CHADEMA imekujaje hapo mkuu?? [emoji1787][emoji1787]Vijana wa Tanzania wa sasa kuna kazi sana katika hii nchi
 
Serikali moja itaimeza Z'bar; Serikali tatu zitaidhoofisha Z'bar. Italazimika kuendesha wizara za muungano kwa pesa zake na wakilega lega hasa kwenye sekta ya ulinzi, itakuwa ni rahisi kwa Z'bar kupinduliwa hata tu na Panya road.
So serikali mbili is not the best but optimal choice.
 
Hivi huyu mzee ana rest lini? Atuachie na sisi tuwe na mawazo mbadala?
 
Watanganyika mpaka wapige kura ya maoni ikisimamiwa na tume huru ndio tutajua kama watanganyika hawaitaki au wanaitaka !!
Kwa nchi iliyojaa wajinga kama hii, zinaweza kupigwa kura chini ya tume huru kabisa ukashangaa watanganyika zaidi ya 50% wanataka waendelee na mfumo wa serikali 2.

Tume ya Nyalali tuliambiwa zaidi ya 70% walitaka tuendelee na mfumo wa chama kimoja. Nchi ya ajabu sana hii.
 
Nadhani upinzani usikazanie kupata kila kitu.

Tume huru ni mwarubaini wa matatizo mengi.
Wanasiasa nao wanaangali upande wao kwenye hiyo katiba mpya kama hakuna wenye kuwanufaisha kisiasa moja kwa moja sasa waitaikubali hiyo katiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…