Wassira: Ieleweke wazi tunapoandika Katiba Mpya Sera ya CCM ni Serikali 2 kuelekea 1 na Siyo vinginevyo

Wassira: Ieleweke wazi tunapoandika Katiba Mpya Sera ya CCM ni Serikali 2 kuelekea 1 na Siyo vinginevyo

Wassira anajidanganya. Hakuna Mzanzibar atakayekubali serikali moja!. Hata Wazanzibar wana CCM hakuna anayekubaliana na hilo. Afanye utafiti tu ataona!
 
Zanzibar nao waseme kabla ya kuanza huo mchakato wanatakaje ? Isije ikawa kazi ya kuzipoteza tena pesa za walipa kodi kwa kitu kinachojulikana kuwa hakitowezekana !! Ccm ya Wassira imeshasema lake je upande wa pili nao wapo pamoja na Wassira au vipi ?!
Zanzibar wanataka serikali tatu, wapinzani wanataka serikali tatu, ccm wanataka serikali mbili kuelekea serikali moja.

Ndio maana nikasema hapa panahitaji akili kubwa maana hili linaweza likawa chaka la ccm kujifichia
 
Huyo ni
Mzee Wassira kupitia mahojiano maalum yaliyofanywa na TBC yakimuhusisha pia Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo amesema Sera ya CCM kuhusu muundo wa Serikali haitabadilika.

Wassira amemwambia Zitto Kabwe kwamba Ukitaka Serikali 3 ujue hakuna Katiba Mpya itakayopatikana.

Ukweli Mchungu!
Mjumbe wa kamati kuu ya chama,huenda ndiyo msimamo wa chama,lakini chama hakiwezi kuwa na nguvu zaidi kuliko Watanzania akiwepo na yeye. Upeo wa kuzeeka kifikra na kimwili kumbe viko sawa.
 
NIMEPENDA UKWELI WA MZEE WETU WASSIRA, NA HUO NDIO UKWELI WENYEWE. SEREKALI TATU ITAHARIBU UMOJA WETU ADHIMU, TUWE MAKINI, KATIKA KUULINDA MUUNGANO WETU, MUUNGANO NI BORA KULIKO CHOCHOTE KILE.
Umoja ambao Wazanzibari milioni moja wana haki kuliko Watanganyika milioni 60?
 
Madhara ya serikali moja ni kwamba zanzibar itakuwa imezikwa rasmi. IMEUZWA

Nini madhara ya serikali tatu?

Na nini madhara ya serikali mbili?
 
Hoja yako haina mantiki kabisa.
Kivipi serikali tatu zitaharibu umoja wetu badala ya kuuimarisha?
Kama kuwa na serikali nyingi(tatu) ni tatizo, kwanini usije na hoja ya kutaka kuwa na serikali moja badala ya mbili?
Lengo ni kuelekea kwenye serekali moja, ukiongeza ya tatu, itakuwaje? Hapa kwenye mbili ndio rahisi kuelekea kwenye moja!, yenye maendeleo yenye uwiano sawa! Kwa kila kipande ndani ya muungano wetu.
 
Zanzibar wanataka serikali tatu, wapinzani wanataka serikali tatu, ccm wanataka serikali mbili kuelekea serikali moja.

Ndio maana nikasema hapa panahitaji akili kubwa maana hili linaweza likawa chaka la ccm kujifichia
Haswaaa ! Hata hao wazanzibari Ccm je wao pia ndio msimamo wao kama wa Mzee wa Ccm Bara !! Ndio swali kuu !!!
 
Back
Top Bottom