Historia inapotoshwa,hakuna Muungano wa kulazimishana, Muungano ulikuwa wa makubaliano kwa mkataba wa miaka 10. Kwao kwa kuwa wamezoea vya kunyonga Muungano ubaki kuwa fumbo la imani. Zanzibar imebadilika katiba kama nchi,inataka itambulike hivyo kuwa na mamlaka kamili ndani ya Muungano. Wamevunja katiba ya JMT inayoitambua Zanzibar kama sehemu ya Muungano siyo nchi yenye mamlaka kamili. Katiba ya JMT inasema kutakuwa na nchi mmoja yenye serikali mbili,lakini leo tuna nchi mbili zenye serikali mbili,shida hii iko ndani ya CCM wenyewe,CCM ya Zanzibar haikubakiana na CCM ya bara kutokuwa nchi yenye mamalaka yake kamili.