KERO Wastaafu Rorya Wanamizwa na Mikopo Umiza ya Mtu Anayeitwa 'Adriano', Serikali Ingilieni Kati!

KERO Wastaafu Rorya Wanamizwa na Mikopo Umiza ya Mtu Anayeitwa 'Adriano', Serikali Ingilieni Kati!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna unyanyasaji mkubwa na wa kutisha unaoendelea katika Wilaya ya Rorya dhidi ya wazee wetu wastaafu, hususan walimu waliolitumikia taifa hili kwa uaminifu. Kuna mtu mmoja anaitwa Adriano, amekuwa akitumia mwanya wa kutoa mikopo isiyo rasmi (mikopo umiza) ili kupora mafao ya wastaafu kwa nguvu. Unakuta mtu anakaribia kustaafu anakopa laki tatu na hapewi namna ya kurejesha ila ghafla tu anaibuka na kudai milioni 10 baada ya kugundua wanakaribia mafao.

Mtu huyu amekuwa "sheria" yeye mwenyewe. Yeye ndiye anayeamua nani akamatwe, nani afungwe gerezani, na kwa miezi mingapi. Hataki kabisa kusikia makubaliano ya kulipa deni taratibu; anataka fedha zote kwa mkupuo. Kibaya zaidi, hata deni likiisha, anatafuta mbinu za kufungua madai mapya ya uongo, na cha kusikitisha ni kwamba anafanikiwa kupitia baadhi ya vyombo vya dola na sheria vya ngazi ya chini ambavyo vimekuwa vikimkingia kifua.

Wazee wetu wengi wa Rorya wanapoteza maisha kwa msongo wa mamawazjuu ya huyu mtu, na hata wengine baada ya kufariki mali zaokama nyumba ziliuzea ili kulipa mikopo hiyo. Serikali iliwahi kuingilia kati suala hili huko nyuma, lakini cha kusikitisha ni kwamba wale waliopewa dhamana ya kulisimamia waligeuka.

Hali hii imekithiri na imekuwa kero ya wilaya nzima ya Rorya. Tunaomba viongoxi wakuu na vyombo vya juu vya uchunguzi viingilie kati dhuluma hii inayofanywa na huyu mtu dhidi ya wazee wetu.
 
Back
Top Bottom