Wastaafu wawe wanaandaliwa kisaikojia kabla ya kukabidhiwa mafao

Wastaafu wawe wanaandaliwa kisaikojia kabla ya kukabidhiwa mafao

Mkuu Sky Eclat umenena vema sana lakini kwa namna hii ni sawa na mtu kutatua matawi ya matatizo ambayo chanzo kikuu hakiguswi.

Huyu mtumishi anayepokea mshahara kabla ya kustaafu hajui hata namna ya kupangilia hiki kiasi kidogo anachokipata kila mwezi, unategemea hicho kiasi kikubwa kikiingia baada ya kustaafu ataweza kukipangilia vizuri na kuiwekea malengo ya faida.

Nakupa mfano, mtumishi anapokea pesa mwisho wa mwezi ila ile hela yote inaishia kwenye matumizi ya nyumbani na ya kawaida. Pesa imeingia kalipa ada ya watoto, chakula, malazi na mavazi. Kiufupi hakuna kiasi anachotenga kwaajili ya malengo ya muda mrefu au uwekezaji wowote anaoufanya either katika biashara au kitu kingine, na hii yote ni kwasababu ya kukosa financial education yenye kumsaidia katika kufanya management ya pesa zake za kila mwezi.

Mshahara unaingia ana madeni ya kutosha, pesa akipiga hesabu yote imekwisha kabla hata hajaipokea. Mtu kama huyu akutane na mill 60 ghafla unategemea atafanyia nini pesa hii iendelee kuonekana??

Hivyo ishu siyo kutoa elimu wiki chache kabla ya kupokea pesa hii, yaani unatibu ugonjwa uliokomaa kwa muda mrefu ndani ya wiki moja ni ngumu sana.

Hii elimu wahusika wajifunze kuanzia mwanzo katika kufanya management ya mshahara ule anaopokea kwa mwezi. Maisha ya pata na kula, pata na kula, yaani pesa inaingia mwezi huu ikiisha unasubiria ya next month nayo ikiisha unasubiria nyingine hivyohivyo hujiangaishi ni kwa namna gani naweza tumia pesa ya miezi sita au 12 kujenga side income ambayo inaweza nisaidia kiasi kwamba hii ya miezi mingine nisiiguse kabisa au niiguse kidogo sana na inayobaki ifanye mambo mengine katika uwekezaji ??

Tatizo linaanzia huku mwanzo kabisa tena tukiwa bado vijana wadogo kabisa tunaingia makazini ila elimu ya mipango na fedha katika maisha halisi hatujifunzi.

Mtu kafanikiwa kujichanga kapata millioni kadhaa kupitia mshahara wa kila mwezi kisha anakuja uliza biashara gani afanye itakayompa faida haraka, huyu mtu akipata mill 60 au zaidi ghafla unategemea atakuwa na mawazo afanyie nini zaidi ya kusikiliza wengine wanasema nini?? na ndio mwanzo wa kupotea.

Hili suala lianze kabla ya watumishi kustaafu, wapewe elimu ya mipango na fedha katika maisha halisi ili IWAJENGE mapema ili hata wakipokea mafao yao waweze kuitumia vizuri.

Tujifunze kujenga utamaduni wa kutanguliza MIPANGO kabla ya FEDHA. Fedha ikitangulia mipango, uwezekano wa fedha kujiamulia wapi pa kwenda ni mkubwa sana, lakini mpango ukiwepo fedha ile itafuata ule mpango kwa lazima.

Semina zianzie makazini kabla hatujastaafu. Lakini pia tujenge utaratibu wa kujifunza na hata kusoma vitabu vinavyohusu maswala ya fedha.
 
Uko sahihi kabisa, mi muhanga.
Mama kastaafu kapigwa mil 65 kajenga kanisa nyumbani
Waumini wote ye ndio anahudumia.
Kila anayekuja ana matatizo.
Mama ana huruma sana
Muumini badala ya kuleta sadaka ndo kwaanza anaomba nauli ya kurudi kwao.
Nilikua sijali na mambo yake ila siku aliponambia kisiri nimpe hela akawape nauli ndo nikaona sasa huu utani.
Nikavunja kanisa na
Siku niliwatimua na bange zangu hawatanisahau.
Hela zimeisha,waumini hawapo Mama anasalisha huko kanisani lutheran kama nilivyomshauri
Sasa hivi ndo matokeo,
mmoja mmoja anamfata anawaombea,wanafanikiwa na kwakweli wanamsaidia fasta kunapotokea chochote.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Hata sisi tulimjengea mapema akiwa bado kazini; nadhani ilichangia kumfanya abweteke na kuona hela hazina kazi hawa wazee ni watata sana kabla ya kustaafu tulikaa nae sana na kumpa semina elekezi sisi wenyewe na tulikua tunampa mfano wa wenzie walomtangulia kustaafu akawa anatuelewa vizuri sana na akatuahidi akipata tu mpunga atatuita; weeeh alivyopata hata hakutwambia yani hatukujua kapata lini na sh ngapi adi zilivyoisha ndo akafunguka [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Yuko mzee Ile kuzipata tu, alihamia gesti na mke wake.
Alikua anawasikia watu wakisema wameinjoi sana wakiwa gesti. N
Heri alihamia gesti na mkewe na sio wadangaji[emoji3]
 
Hiyo tabia ipo tu kwa Maganga hawa
Kuna mzee alipiga mil 200+ kwenye kamari akahamia hotelini mpaka zikaisha,
Ukimuona leo utashangaa
 
Sure,kunamzee alioa kibinti kidangaji,binti akapura zilepesa kwa fujo,dakika za mwisho watoto wa mzee wakamchapa yule binti,mzee akasalimu amri akamuacha. kucheki bank kwenye milioni 80 mzee kabakiza milioni 12 tu.
Hahahaha dah nguvu ya ppch ni noma
 
Sky umenikumbusha mbali sana maana ile hasira wakati natimua waumini, ndo leo nimekumbuka, kwasababu maza nikamwambia subiri hapo kumbe natoka na panga ingia kanisani nnanoa panga nje pale vurugumisha huku nawasindikiza panga linapepea
aisee walitoka baruti wanapiga makelele tunakuufwaaa mama mchungaji kumbe anakaa na kichaa🤣🤣🤣🤣
Narudi mama ndo kwaanza anasubiri nimpe hela awape nauli anauliza Mbona naskia makelele nje huko
Nikamwambia mama tulia hamna cha nauli wala nini washaenda hao nshawapa.👍
Na ndo siku hiyo hiyo kuita greda kuvunja kanisa lote kibabe,
Kisha kumwambia nenda ukagombee ama uhubiri chochote kwenye makanisa huko sio mnatuletea kero hapa nyumbani.
Aah mpaka leo ni mchungaji mzuri tu huko ila hela hamna namuhudumia.
 
Cha maana alichofanya ni kumkumbuka mke wake katika shida na raha.
😂😂😂 umenikumbusha mzee mmoja, aliisasambua milion 95 ndani ya miezi miwili, mwezi wa 3 wiki ya kwanza kaja kulilia monthly yake, Kilio kizito cha kufiwa, Watu babu vipi? Mtoto wake tena ndio anahadithia, Babu kupokea mafao tu, kavunja nyumba yote, akajenga upya, fenicha mpya nyumba zima kaja kununua mjini, akitokea wilayani huko. Sherehe kila mwisho wa wiki😂😂😂. Elimu wanapewa sana basi tu ile pesa inatia wazimu, mtu maisha yake yote hajawai kushika hata milion 10 leo ghafla unamuangizi milion 100
 
Ile hela ni kama ina laana, wengine wanauziwa almasi feki, kwakua anataka aagane na umasikini anajua ata double hela yake. Wengine wanakua walevi mbwa.
 
Huwa sielewi kabisa hesabu za mafao zinapigwa vipi. Kwa kanuni ambazo mifuko inatutangazia haiwezekani kipato cha laki nne unusu kikazaa milioni 60 hata ungefanya kazi miaka 50!
Ndio sababu ya kufanyia mabadiliko kikokotoo, ile formula ya zamani si rafiki kwa mifuko, unaweza kukuta mwanachama michango yake yote ni tsh 15,000,000 then analipwa 60,000,000 mpaka 70. Ndio maana hii mifuko ipo taabuni
 
Nadhani wastaafu huwa wanawadanganya ndugu zao kiasi gani wanapata...

Kwamba mwalimu wa laki saba kwa mwezi (grade A, shahada) anastaafu na mafao ya milioni mia.

Kwa mahesabu yepiii ?

Miaka 40 ya utumishi, mshahara wa mwalimu wa grade A fao la mkupuo ni:

700,000 X 12 X 1/580 X 12X 40 X 12.5 X 0.25

= 21.7 Mil
 
Kuna wale wazee aka wabishi kuzeeka,wako tayari wafie kwenye vinena aka vipochi manyonya.Nawafahamu wawili mmoja mzee wa bandari kastaafu na mwingine alikuwa UDSM alafu wote walikuwa marafiki walivyopata mafao waliondoka home kabisa na kuhamia kwenye nyumba ndogo baada ya pesa kuisha wakarudi kwa wake zao na korodani zao.

Hivi huwa wanarudije rudije [emoji3] maana usikute waliondoka kwa mbwembwe zote baada ya kupata mafao na kuhamia kwa mcheps. Nawaza akifulia sijui huwa wanapitia njia gani kurudi kwa maza hausi. Na pia reaction ya maza hausi huwa sijui inakuwaje [emoji848]
 
😂😂😂😂
 
Nadhani wastaafu huwa wanawadanganya ndugu zao kiasi gani wanapata...

Kwamba mwalimu wa laki saba kwa mwezi (grade A, shahada) anastaafu na mafao ya milioni mia.

Kwa mahesabu yepiii ?

Miaka 40 ya utumishi, mshahara wa mwalimu wa grade A fao la mkupuo ni:

700,000 X 12 X 1/580 X 12X 40 X 12.5 X 0.25

= 21.7 Mil
Kama hujui kitu aidha uulize au ukae kimya kuliko kuropoka watu wakajua kiuhakika kwamba kichwa chako Ni Cha kufugia nywele tu.
 
Kama hujui kitu aidha uulize au ukae kimya kuliko kuropoka watu wakajua kiuhakika kwamba kichwa chako Ni Cha kufugia nywele tu.
Kweli kabisa, sijui kitu.

Hebu wewe nambie, mwalimu aliyestaafu na mshahara wa laki 7 anapata pensheni ya mkupuo shiing ngapi ?

Assuming hajawahi kupewa mafao ya bima ya afya, mafao ya unempoyment wala disability.
 
Now you are talking.
Reverting.....
 
Wastaafu wengi huumizwa na mafao ambayo yalilengwa kuwasaidia. Kuna mmoja alipata milioni 200, wapambe walimshauri awekeze kwenye uchimbaji mdogo wa dhahabu. Alikaa huko miezi 18. Amerudi nyumbani hana kitu bahati yake mke ni mhangaikaji ana mgahawa.

Wahanga wa matukio haya ni wengi sana. Unamkuta mfanyakazi alikua anapokea laki nne na nusu kwa mwezi ghafla anamiliki milioni 60 benki. Kuna ambao wana malengo. Alikopa huko nyuma na kununua kiwanja na kujenga nyumba ya nyuma ili aachane na kulipa kodi. Alipanga mafao ndiyo ajenge nyumba ya mbele.

Ninachoona mifuko ya jamii iajiri wataalamu wa saikolojia na pia washauri wa uwekezaji. Ile wiki msataafu anayokabidhiwia pesa zake aelewe kuwa ana pesa lakini pesa ni liquid asset na ikishamwagika haizoleki. Apewe pia mawazo katika uwekezaji sahihi kama atapenda.
Mkuu huyo wa dhahabu, alibeba fuba lote akatokomea nalo mgodini?
 
Yuko mzee Ile kuzipata tu, alihamia gesti na mke wake.
Alikua anawasikia watu wakisema wameinjoi sana wakiwa gesti. N
Inaonekana huyo mzee alikuwa hana makazi aliyojenga.

Hivi gest panaweza kuwa 'patamu' kama nyumbani kama pako vizuri?
 
Back
Top Bottom