Mkuu
Sky Eclat umenena vema sana lakini kwa namna hii ni sawa na mtu kutatua matawi ya matatizo ambayo chanzo kikuu hakiguswi.
Huyu mtumishi anayepokea mshahara kabla ya kustaafu hajui hata namna ya kupangilia hiki kiasi kidogo anachokipata kila mwezi, unategemea hicho kiasi kikubwa kikiingia baada ya kustaafu ataweza kukipangilia vizuri na kuiwekea malengo ya faida.
Nakupa mfano, mtumishi anapokea pesa mwisho wa mwezi ila ile hela yote inaishia kwenye matumizi ya nyumbani na ya kawaida. Pesa imeingia kalipa ada ya watoto, chakula, malazi na mavazi. Kiufupi hakuna kiasi anachotenga kwaajili ya malengo ya muda mrefu au uwekezaji wowote anaoufanya either katika biashara au kitu kingine, na hii yote ni kwasababu ya kukosa financial education yenye kumsaidia katika kufanya management ya pesa zake za kila mwezi.
Mshahara unaingia ana madeni ya kutosha, pesa akipiga hesabu yote imekwisha kabla hata hajaipokea. Mtu kama huyu akutane na mill 60 ghafla unategemea atafanyia nini pesa hii iendelee kuonekana??
Hivyo ishu siyo kutoa elimu wiki chache kabla ya kupokea pesa hii, yaani unatibu ugonjwa uliokomaa kwa muda mrefu ndani ya wiki moja ni ngumu sana.
Hii elimu wahusika wajifunze kuanzia mwanzo katika kufanya management ya mshahara ule anaopokea kwa mwezi. Maisha ya pata na kula, pata na kula, yaani pesa inaingia mwezi huu ikiisha unasubiria ya next month nayo ikiisha unasubiria nyingine hivyohivyo hujiangaishi ni kwa namna gani naweza tumia pesa ya miezi sita au 12 kujenga side income ambayo inaweza nisaidia kiasi kwamba hii ya miezi mingine nisiiguse kabisa au niiguse kidogo sana na inayobaki ifanye mambo mengine katika uwekezaji ??
Tatizo linaanzia huku mwanzo kabisa tena tukiwa bado vijana wadogo kabisa tunaingia makazini ila elimu ya mipango na fedha katika maisha halisi hatujifunzi.
Mtu kafanikiwa kujichanga kapata millioni kadhaa kupitia mshahara wa kila mwezi kisha anakuja uliza biashara gani afanye itakayompa faida haraka, huyu mtu akipata mill 60 au zaidi ghafla unategemea atakuwa na mawazo afanyie nini zaidi ya kusikiliza wengine wanasema nini?? na ndio mwanzo wa kupotea.
Hili suala lianze kabla ya watumishi kustaafu, wapewe elimu ya mipango na fedha katika maisha halisi ili IWAJENGE mapema ili hata wakipokea mafao yao waweze kuitumia vizuri.
Tujifunze kujenga utamaduni wa kutanguliza MIPANGO kabla ya FEDHA. Fedha ikitangulia mipango, uwezekano wa fedha kujiamulia wapi pa kwenda ni mkubwa sana, lakini mpango ukiwepo fedha ile itafuata ule mpango kwa lazima.
Semina zianzie makazini kabla hatujastaafu. Lakini pia tujenge utaratibu wa kujifunza na hata kusoma vitabu vinavyohusu maswala ya fedha.