Wastara anamiliki hii hummer?

Wastara anamiliki hii hummer?

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Jamani wambea wenzangu wa humu jamii forum na bloggers, hii tabia nimeona inakua sana siku hizi , unakuta msanii au mtu yeyote maarufu kapiga picha na gari Kali na kutundika mitandaoni, unakuta wengine hawaandiki chochote kama wamenunua au wanayamiliki hayo magari, Sisi sasa tunavyowashwa kusambaza umbea kwenye ma blog na humu Jamii forum "Mkoko mpya wa msanii flani","huyu ndo msanii anayemiliki mkoko mkali kuliko wote apa Tz." Najua kila mtu anatamani awe wa kwanza kusambaza umbea kwenye ma blogs au mitandao mingine, ila tuwe wavumilivu ,hawa wasanii wetu ni wasanii sana wanatumia psychology Ku catch attention zetu, ki ukweli nimeona wasanii wengi wakipiga picha na magari ya watu na kusambaza mitandaoni , Ajabu kila siku tunapishana nao kwenye mabasi ya mbagala au wengine unakuta hawaendeshi magari wanayosambaza kwenye Mitandao.

Mfano halisi juzi kati msanii wa hip hop Young Dee alitundika picha ya Nyumba kwenye Mtandao wa Instagram. Wambea wenzangu sasa wasivyotaka kupitwa fasta kusambaza mitandaoni, flani kanunua mjengo wa million 800 , duh nilichoka nilivyokuja kusikia habari halisi ya hiyo nyumba aliyopiga picha young Dee yani vitu viwili Tofauti. Ukiona msanii kama masanja kapost picha na kusema " AHsante mungu kwa hii gari" apo ujue basi kweli msanii huyu hii gari kainunua, ukiona msanii kapiga picha na Ndinga kubwa halafu hasemi kit, we chukua jembe kalime. Na nyie mashabiki muache vihele hele mtu akipost picha na gari Mnaanza oooh hongera sana umetisha, hakuna kama wewe TZ , sifa kibao , halafu unakuta msanii husika hajibu chochote hakubali kuwa gari sio lake au kusema chochote.

Nirudi kwa wastara, pita pita yangu Leo IG nikaikuta hii picha imetundikwa na msanii wa bongo movie wastara. Nimeona pongezi kibao wakati mwenyewe ajaongelea chochote kuhusu hiyo picha. Bado haijajulikana kama kanunua au anaringisha kapanda hummer.
Nilikuwepo warumi.

attachment.php
 
Attachments

  • 1396257871086.jpg
    1396257871086.jpg
    42.9 KB · Views: 2,515
mashabiki tunakuaga na vihedenswede ila kwenye kucomment

unakuta mwenyewe anawachoreni tu.........
 
mashabiki tunakuaga na vihedenswede ila kwenye kucomment

unakuta mwenyewe anawachoreni tu.........

Umeona eeh? Na wenyewe kimyaa kama hawapo, nimeona leo wastara alivyo post hiyo ndinga mashabiki wanakwambia wakomeshe hao wastara umetishaa, miaka miaaa, jamani mitandao ina raha sana binamu.
 
Teh Wastara anunue hummer??? labda ahongwe tatzo mashabiki wanajitoa ufahamu sana.
 
Huyu ndio yule aliyetembeza bakuli kuomba msaada wa million 20 za kutibiwa sajuki au ni mwingine?

Hivi na mimi nikupload picha niko kwenye maana yake nimenunuwa ndege? ujinga mwingine ni shida kweli.
 
Huyu ndio yule aliyetembeza bakuli kuomba msaada wa million 20 za kutibiwa sajuki au ni mwingine?

Hivi na mimi nikupload picha niko kwenye maana yake nimenunuwa ndege? ujinga mwingine ni shida kweli.

Ah aah unanichekesha eti aliyetembeza bakuli kuomba msaada , dah humu watu mmepinda.
 
Wamuache miaka miaaa, Ndio msanii anayemiliki ndinga ya gharama kuliko wote TZ. Wakamtangazeee:banghead::banghead::what::

ataingia kwenye top ten ya wasanii wanaomiliki magari ya bei mbaya
mpambano ukiisha mwenye gari anachukua
wasanii wa bongo maisha yao maigizo kama hiyo fani yao
 
ataingia kwenye top ten ya wasanii wanaomiliki magari ya bei mbaya
mpambano ukiisha mwenye gari anachukua
wasanii wa bongo maisha yao maigizo kama hiyo fani yao

Aaaaah aah halafu huyu wastara naye siku hi I Sijui haya mashauzi kayatoa wapi, hakuwaga ivi zamani , kweli Dunia mzunguko.
 
warumi kwahiyo msanii anaeongoza kwa gari la gharama kubwa ni nani maana domo gari imemshinda kulipa japo walisema thamani yake ni 250M kumbe 100M wabongo bhana, kwasasa naamimi msanii mwenye achievement hapa Bombo ni Masanja, gari la gharama kwa waimbaji wa BF ni Lady Jaydee hapo tumemtoa Masanja sababu yeye haimbi BF wala HH.
 
Last edited by a moderator:
Huyu ndio yule aliyetembeza bakuli kuomba msaada wa million 20 za kutibiwa sajuki au ni mwingine?

Hivi na mimi nikupload picha niko kwenye maana yake nimenunuwa ndege? ujinga mwingine ni shida kweli.

self container ndani choo cha shimo unamiliki harrier engine ya rav 4 unamiliki hummer engine ya discover
 
Aaaaah aah halafu huyu wastara naye siku hi I Sijui haya mashauzi kayatoa wapi, hakuwaga ivi zamani , kweli Dunia mzunguko.

hivi aunt ezekiel ameachika?mbona siku hizi yupo hivo?
 
Back
Top Bottom