Wastara Juma aomba Watanzania tumuombee, Nyumba zake 2 zawekwa x

Wastara Juma aomba Watanzania tumuombee, Nyumba zake 2 zawekwa x

Bomoabomoa ni sawasawa na Oparesheni tokomeza ujangili vyote vili/naendeshwa kikatili.
 
Ni upuuzi aombewe anaimwa kubomolewa Nyumba zake ni ajabu waliobomolewa wasio nacho tisemeje akakate mauno getini ilkulu yakubalike atasamehewa tu
 
Ukiwa maskini harafu unaishabikia CCM kinafiki malipo yako ni hapahapa. Hao vigogo wa CCM watalipwa siku ya mwisho.
VIJANA BOMOA NYUMBA HARAKA SAAANAAAAAAAAAAA!!!
 
Watu mna roho mbaya sana! Mnafurahia matatizo ya watu?!? Mungu awasamehe hamjui mlifanyalo!
Ficus, sidhani kama kuna anayependa mwenzake adhurike. Huyu dada na bongo mie wenzake wanatumika sana na chama tawala, then wanatupwa. Sisiemu wako wapi ili wanusuru nyumba zake zisibomolewe ?
 
Nyodo, Maringo, Dhihaka na Kejeli za kutosha alizokuwa akizifanya Mitandaoni na Majukwaani ili kuisifia CCM huku akiwabeza wanyonge wa UKAWA ambao walikuwa wakiitwa Malofa, Wajinga na Wapumbavu, ndio zimeleta yote haya.
Bado sio sababu ya kufurahia matatizo ya mtu binafsi! Kile kilikuwa ni kipindi cha campaign na kila mtu ana haki ya kumshabikia/kumnadi mgombea anayeona anafaa!

Kama watanzania tutaendelea kuishi kwa chuki namna hii, tena ya kipuuzi hatutafika mbali.
Eeeeeh Mungu inusuru nchi yetu na dhambi hii.
 
Mlikejeli sana upinzani ninachopendea upinzani mipango yao si ya mabavu wanatumia akili zaidi hawakurupuki zoezi lolote ukilifanya kwa staili inayofanyika baadaye Nina hakika itaigharimu serikali kufidia gharama za makazi wanayobomoa hivi sasa najua Dar upinzani mliuunga mkono sana nawapa pole lakini matunda ya mbunge Kinondoni yataiabisha serikali
 
Last edited:
Asilimia kubwa ya watu ambao mnafurahia yaliyompata wastara ni graduates

hapo ndipo ninapowaambia watu kwanini watanzania tukiingia kwenye ushindani wa kutafuta kazi na wakenya tunashindwa

wasomi wengi wa nchi hii ni wamehudhuria tu madarasa lakini hawajaelimika

kule facebook msomi mwingine kampost Afande Ryoba R.I.Paliyekuwa msaidizi wa IGP na kusema eti hakuwa anajua kuwa polisi kuna watu handsome halafu aliyepost vile ni mwanaume sasa

hii nchi bwana
 
Last edited:
Kuna ujumbe aliuandika Instagram kuelezea changamoto alizokutana nazo wakati anamuuguza marehemu mmewe da Inasikitisha Sana baada ya siku mbili tena akaandika nyumba zake mbili zimewekwa X ,Naogopa kusema chochote maana tutazidi kumuondolea furaha ambayo amesema amaikosa tangia 2011 mmewe alipoanza kuumwa,Nami nampa pole aende Lumumba watamsaidia.

Hana furaha vipi wakati alikuwa akiimba kwa furaha majukwaani wapinzani tuwachanechane tuwatupeeee, na kumkejeli lowasa? na badoooo siku member wa ze comedy akisomeshwa namba ntafurahije!!
 
Back
Top Bottom