Wastara Kikaangoni EATV, aibua mapya ya Mange Kimambi, Ali Kiba kumpa msaada na hasimu wake kumnyima

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Wastara amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, Wastara anasema kuwa alimuandikia barua Diamond Platnumz kuomba msaada pamoja na Alikiba lakini kwa Diamond alionekana yeye ni kama tapeli.

"Niliandika barua kuomba msaada hivyo nilimuandikia Diamond lakini watu wake walimfikishia taarifa kuwa mimi tapeli hivyo hakuweza nisaidia ila pia wakati huo huo nilimuandikia Alikiba na Alikiba akaniambia kuwa kuna watu walikuwa na show yao Kenya ila walikuwa hawana fedha yeye anazohitaji hivyo akaniahidi kuwa atakwenda kufanya show hiyo ili aje kunisaidia, kweli alikwenda na aliporudi aliniletea fedha hizo" alisema Wastara.

Mbali na hilo Wastara amesema kuwa moja ya sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.

Aibua mapya kuhusu Mange Kimambi

Msanii wa filamu nchini Tanzania Wastara Juma amefunguka na kumchana mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyu ana matatizo ya akili ndiyo maana anakurupuka katika baadhi ya mambo.

Wastara amesema hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa na EATV kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano saa nane mchana mpaka saa kumi jioni na kusema kuwa Mange Kimambi alizusha juu ya Cannula aliyowekwa mkononi na kusema alijiwekea mwenyewe, Wastara amesema kuwa mbali na kuzusha huko lakini dada huyo alikwenda mbali mpaka kuwauliza madaktari wa hospitali aliyokuwepo kama anatibiwa hapo.

"Mange Kimambi, aliwahoji madaktari India, mimi nikashangaa wale madaktari wanakuja wananiuliza kwani wewe ni nani Tanzania nikawaambia kuwa mimi ni msanii tu wa kawaida kule, wakaniuliza unamfahamu huyu mtu anajiita Mange Kimambi kwenye Instgram anasema ni dada yako, pia mwandishi wa habari anakuulizia mimi nikawaambia sina dada ana cheti cha Milembe" alisema Wastara

Mbali na hilo Wastara amesema kuwa kama Mange Kimambi angekuwa na akili timamu basi alipaswa kuangalia vizuri ile Cannula ambayo alikuwa amewekewa kwani ilikuwa imewekwa vizuri tu na wala si huo uzushi ambao yeye alikuwa anazusha.


 
Wastara anaonekana mlalamishi na asie na shukrani sijui kalelewaje? Kama kufiwa yeye sio wa kwanza tena ashukuru Mungu aliachiwa hata hivyo vitu vichache, kuna wanawake wanashida sana kuliko hata yeye lakini hawalalamiki na watoto wao wanawalea hivyo hivyo. Suala la kuchangiwa ni hiari ya mtu,,,,wangapi wanakufa hata hela ya panado hawana ,kuongea yupi kachanga na yupi hajachanga sio sawa,,,maana huwezi kupangia bajeti pesa iliyo mfukoni mwa mtu mwingine. Ina maana ndugu zake wote walimchangia?
Kila mtu angeanika shida zake pasingetosha.

Anyway ni mtazamo tu,,sina timu mie
 
Andika upya, unawahi wapi? Swali langu ni kuwa.. mtu asipokusaidia maana yake ni mchoyo?
Huwezi jua niko wap nnavo andika au nafanya nn i think msg yangu ume ielewa regardless of errors.
Yes! Especialky kama ana uwezo wa kusaidia. Ni mchoyo ila si lazima asiwe mchoyo.
Ukisoma hiyo stori fresh utagundua Diamond alifanya uchoyo. But na mimi namshauri wastara asi concentrate na alo mnyima msaada kwani si lazima kusaidiwa. A focus kwa alo mpa msaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…