Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mataifa karibu yote duniani yenye raia zao Sudan wanashindana kuwakimbiza nchini humo. Imekuwa kama ni siasa kuwahi kuwaondoa raia hao kwa mbinu tofauti. Nchi inayochelewa kufanya hivyo kama kwamba inahofia kuingia matatani kwa wananchi wake huko nyumbani.
Katika kuondoka huko kila nchi imekuwa ikifanya mbwembwe zake ili ionekane ni hodari zaidi katika kukimbia eneo lenye vita. Upande wa Marekani awali walisema wana mpanga wa kuwahamisha raia wake haraka. Kumbe wakati wakisema hivyo helikopta za Chinook zilikuwa tayari zipo Khartoum kuchukua maafisa wa ubalozi tu na familia zao wanaofikia 100.Wale raia wengine pacha wafikao 16000 kila mmoja ametakiwa aangalie usalama wake.
Uiengereza, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Spain na nchi nyingi zimeshafanya zoezi hilo. Kwa upande wa Urusi imesema raia wake wote wameshajikushanya ndani ya Ubalozi wa nchi hiyo Khartoum na wanaangalia muda muafaka ili kuwaondoa.Hali ni hiyo hata kwa vinchi vidogo kama Kenya na Misri nao eti wanafanya mipango kuondoa raia zao huo ambao huenda wala hawajui namna walivyoingia na wala idadi yao.
Majenerali wanaopigana nchini humo kila mmoja anajaribu kutoa picha kwamba ndiye aliyepanga mipango ya kusaidia kuondoka raia wa nchi moja baada ya nyengine. Kama wana madai ya kweli katika kuanzisha vita hivi basi badala ya kusaidia kuondoka raia hao wangewashikilia mateka mpaka usalama urudi nchini humo.Wangewaambia hawawezi kuwahakikishia usalalma wao.
Upande wa wananchi matukio hayo ya kukimbizwa kwa raia wa nje kumewakatisha tamaa sana.Alsadig Alfatih amesema kuwaona watu hao wakihamishwa na kuachwa wao wapigane kumemkatisha tamaa sana kwani alitaraji wao ndio wangesaidia kuleta amani.