Wasudan wajiuliza kuhamishwa raia wa nje kuachwa wao wapigane kuna hekima gani

Wasudan wajiuliza kuhamishwa raia wa nje kuachwa wao wapigane kuna hekima gani

Let us call spade a spade vinginevyo Afrika hatutasonga mbele

Somalia wote waislamu mashehe wameenda kusuluhisha imeshindikana wanatwangana tu

Haya Sudan kaskazini hao wanatwangana sasa wote waislamu tena vita wameanza mwezi wa Ramadhan wasivyo hata na aibu dini moja hawaivi

Mifano iko kibao

Waislamu tumechoka na vita zenu za kutwangana wenyewe kwa wenyewe mnatia aibu bara letu la Afrika

Waambie na waislamu wenzao
Mwanaccm asiyejielewa
 
Kwan nchi si yao, kama wanaona vita ni sahihi kwao, basi wao ndo wakwanza kutokuwa na busara, waafrika tunapenda mteremko sana, tujifunze kwa Ukraine ilivyosimama kiume dhidi ya Urusi, sasa kama nyinyi pia mnataka muiache nchi yenu mnabusara kweli?
kwahiyo wabaki humohumo wapigane wao kwa wao wafe kiume, au?
 
Wamewachoka Sudani kusini Raisi na makamu wake walitwangana hasa mpaka baadaye akili ikawakaa sawa kumetulia

Sasa hivi ni zamu ya Sudani kaskazini Raisi na makamu wake wanatwangana akiki zitawakaa sawa mbeleni

Sudani zote mbili Raisi huwa na jeshi lake na makamu huwa na lake sijui wana shida gani

Mataifa ya kiislamu mfano ya uarabuni hata siku moja waislamu waafrika.nchi zenye waislamu watupu wakipigana iwe Somalia au Sudan,au libya,nk au popote huwa hawaingilii kati wala kutoa tamko la kulaani vita ila kwao.ikilipuka kelele kila kona wanataka dunia iwaunge mkono

Waislamu wenzao uarabumi hawasaidii wanaondoa raia zao wanataka Marekani wakristo ndio wawasaidie?

Marekani alijaribu kuingia Somalia awasaidie kumaliza vita alishambuliwa na majeshi ya pande zote zinapigana kuwa hawataki mla nguruwe Somalia toka Marekani akakimbia akawaacha

Afghanistan vile vile akakimbia akawaacha waendelee kutwangana wenyewe huko mwislamu akimtwanga mwislamu mwenzie hadi kieleweke
Waliohamishwa kutoka Sudan wamepokewa Saudia kwa mauwa.
 
Mataifa karibu yote duniani yenye raia zao Sudan wanashindana kuwakimbiza nchini humo. Imekuwa kama ni siasa kuwahi kuwaondoa raia hao kwa mbinu tofauti. Nchi inayochelewa kufanya hivyo kama kwamba inahofia kuingia matatani kwa wananchi wake huko nyumbani.

Katika kuondoka huko kila nchi imekuwa ikifanya mbwembwe zake ili ionekane ni hodari zaidi katika kukimbia eneo lenye vita. Upande wa Marekani awali walisema wana mpanga wa kuwahamisha raia wake haraka. Kumbe wakati wakisema hivyo helikopta za Chinook zilikuwa tayari zipo Khartoum kuchukua maafisa wa ubalozi tu na familia zao wanaofikia 100.Wale raia wengine pacha wafikao 16000 kila mmoja ametakiwa aangalie usalama wake.

Uiengereza, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Spain na nchi nyingi zimeshafanya zoezi hilo. Kwa upande wa Urusi imesema raia wake wote wameshajikushanya ndani ya Ubalozi wa nchi hiyo Khartoum na wanaangalia muda muafaka ili kuwaondoa.Hali ni hiyo hata kwa vinchi vidogo kama Kenya na Misri nao eti wanafanya mipango kuondoa raia zao huo ambao huenda wala hawajui namna walivyoingia na wala idadi yao.

Majenerali wanaopigana nchini humo kila mmoja anajaribu kutoa picha kwamba ndiye aliyepanga mipango ya kusaidia kuondoka raia wa nchi moja baada ya nyengine. Kama wana madai ya kweli katika kuanzisha vita hivi basi badala ya kusaidia kuondoka raia hao wangewashikilia mateka mpaka usalama urudi nchini humo.Wangewaambia hawawezi kuwahakikishia usalalma wao.

Upande wa wananchi matukio hayo ya kukimbizwa kwa raia wa nje kumewakatisha tamaa sana.Alsadig Alfatih amesema kuwaona watu hao wakihamishwa na kuachwa wao wapigane kumemkatisha tamaa sana kwani alitaraji wao ndio wangesaidia kuleta amani.
6d24f0c0-e272-11ed-bffb-d0e242b79dbb.cf.webp
Wamechagua kupigana na hakuna anayewskataza

Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime. Ni methali inayotumika hapo
 
Mwana kulitafuta , mwana kulipata
Janjaweed ambao ndio RSF waliundwa, walifadhiliwa na kulindwa na serikali ya Sudani ili wawauwe Wasudani weusi huko Darfur.

Warussi ndio walinzi wa migodi ya dhahabu huko MALI na SUDAN

HEMELTI mkuu wa RSF amezuru Russia karibuni
Wacha wakose wote, sisi tujiandae pokea wakimbizi tu
 
Na ndo shida ya kutengeneza na kukumbatia majeshi private kama wagner siku wakigeukana wanaanza vurugu kwenye nchi
Nchi haitakiwi kuwa na makundi pinzani, tena wote wakiwa na silaha
 
Dunia iko hivyo.

Niliangalia Hotel Rwanda jinsi foreigners walivyokuwa wakichukuliwa, ilinitia simanzi na kuniachia maswali mengi sana.
hizo ni kodi zao sio kodi zenu nyiny , so ilaumu serikai yako kwa kuitupa pemben aman na kujali matumbo yao kwanza
 
Ngoja tuangalie tujikumbushe.Lakini sidhani kuwa ilikuwa ni ushujaa wa Israel pekee iliambatana na ujinga wa vikosi vya Idi amin muda ule.Leo Israel hana ubavu huo tena
kwahiyi Uganda ya leo ni bora kuliko iran ya 2010s ?maana Israel kapiga mission huko Iran vya kutosha
 
Ngoja wapigane tu kwa sababu kwa waafrika kupigana vita vya kijingajinga hivi ni sifa kwa sababu wanajeshi wanaotakiwa kuwa kambini ili kuilinda nchi dhidi ya maadui kutoka nje eti ndio wanapigania madaraka..!!

Hao wanamgambo wa RSF wanaungwa mkono na Saudi Arabia na wapiganaji wao 40,000 walienda kuisadia Saudi Arabia kwenye vita vyake kule nchini Yemen.

Na sasa hao RSF wanataka eti jeshi ikae madarakani kwa miaka 10 ndio warejeshe utawala wa kiraia..!! Wakati huyo Jenerali Abdel Fatter Al Burhani anataka wakae kwa miaka miwili tu kisha warejeshe utawala wa kiraia.

Nchi zinazoisumbua Sudan ni Saudi Arabia na Misri ambazo zinaigeuza Sudan kama koloni lao. Zinataka ziwe na ushawishi kwa serikali yoyote inayoitawala nchi hiyo na mataifa hayo hayapendi kuona Sudan inakuwa na utawala wa kidemokrasia kwa kuhofia kwamba fikra ya kudai demokrasia inaweza kusambaa kwenda kwenye mataifa yao ambayo yanatawaliwa kiimla.
 
Back
Top Bottom