Wataalam wa Mazingira: Kwanini kuna huduma za kijamii (Shule, Polisi, Hospitali) za kata lakini hakuna hifadhi ya misitu/miti (Mapafu) kwa ngazi hiyo?

Wataalam wa Mazingira: Kwanini kuna huduma za kijamii (Shule, Polisi, Hospitali) za kata lakini hakuna hifadhi ya misitu/miti (Mapafu) kwa ngazi hiyo?

Infantry soldier huko sawa kabisa. Upandaji miti hautiliwi maanani kwa sasa. Miti inahitajika sana lakini hakuna msisitizo kwa sasa. Chuo Kikuu Dodoma hawajawahi kupanda msitu maeneo yale. Miaka zaidi ya kumi tangu chuo kianzishwe imepita.

Kuna kata nyingi hazina misitu hata kuhamasisha wanaopata viwanja kupanda miri hakuna. Vijiji na mitaa sioni wakiwa na mipango endelevu ya kupanda miti. TUJISAHIHISHE
Katika baadhi ya maeneo hakuna mipango shirikishi: mabaraza ya madiwani wanaona kuwa faida kubwa kwa miji ni kuwa na majengo/makazi cum kuuza viwanja hivyo hawaoni unuhimu wa kuacha maeneo ya misitu. Tazama mfano wa kibaha, eneo lilotengwa msitu sasa limevamiwa na majengo ya serikali
 
Sehemu nyingi bado watu wanajenga kiholela..
Kama watu huwa wanafidiwa mali zao ili kupisha miradi ya maendeleo, kwanini sehemu zenye mbanano kama Magomeni, Manzese, Mbagala, Tandale kusifanyike fidia hizi ili kupata eneo kuwa la kujenga haya mapafu ya hewa safi walau ngazi ya kata tu?
 
mabaraza ya madiwani wanaona kuwa faida kubwa kwa miji ni kuwa na majengo/makazi cum kuuza viwanja hivyo hawaoni unuhimu wa kuacha maeneo ya misitu.
Daaah aisee, this is too sad mkuu...
 
Tazama mfano wa kibaha, eneo lilotengwa msitu sasa limevamiwa na majengo ya serikali
Nikiwa nina safiri kwenda nje ya Dar huwa ninapita Kibaha na kuona ile miti mpaka moyo wangu unafurahi, sasa unaponiambia kuwa wameanza kufyeka ile miti mkuu, kweli watu ni wabaya aisee.
 
Mf. Kama watu wanauza au wanajenga ktk viwanja vya michezo au maeneo ya wazi yaliyotengwa, watakuwa na akili ya kuwa na maeneo ya hifadhi ya miti?
Haloo...!!! Inaonekana hali hii inatisha sana mkuu...
 
Pia maeneo mengi ya shule, hospitali, na maeneo ya ofisi za serikali walikuwa na utaratibu wa kupanda miti ktk siku ya miti Sina uhakika Kama huo utaratibu bado upo..
Hii pia hata mimi ninaikumbuka sana mkuu wakati nipo primary school.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania wataalam wa mazingira eti;

Kwanini kuna huduma za kijamii (shule, polisi, hospitali) za kata lakini hakuna hifadhi ya misitu (mapafu ya hewa safi) kwa ngazi ya hiyo?

Au hiyo hifadhi maalum ya misitu kwa ngazi ya kata ipo lakini mimi ndio sijui?

View attachment 1588612

KWA UFUPI KUHUSU MSITU WA AMAZON (MAPAFU YA DUNIA)

==========

The Amazon (Msitu wa Amazon) is often referred to as Earth's 'lungs,' because its vast forests release oxygen and store carbon dioxide, a heat-trapping gas that is a major cause of global warming.

Msitu wa Amazon ndio msitu mkubwa zaidi duniani unaopatikana huko America kusini. Msitu huu una eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,500,000 ( Milioni 5) yani kwa ukubwa huu nchi ya TANZANIA iingie mara 6 kwenye msitu huo.

View attachment 1588819

Msitu wa Amazon unakadiriwa kuwa na miti billion 400 na aina mbalimbali za miti zaidi ya 160,000 pia kuna miti ya matunda tofauti tofauti elfu tatu katika msitu huo.

Asilimia 20% ya oxygen iliyopo dunia inatengenezwa katika msitu wa amazon ndio maana unaitwa mapafu ya dunia.
==========

Kwanini huduma nyingi za kijamii (shule, polisi, hospitali) zimeteremshwa kutoka ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata isipokuwa huduma hii ya kuwa na hifadhi nzuri za msitu (Mapafu ya hewa safi)?

View attachment 1588820

Kama watu huwa wanafidiwa mali zao ili kupisha miradi ya maendeleo, kwanini sehemu zenye mbanano kama Magomeni, Manzese, Mbagala, Tandale kusifanyike fidia hizi ili kupata eneo kuwa la kujenga haya mapafu ya hewa safi walau ngazi ya kata tu?

MSAADA PLEASE: Ni miti gani mizuri mtu anaweza kupanda pasipo mizizi yake kuleta madhara kwenye msingi wa nyumba?

WATAALAM WA MAZINGIRA NA MIPANGO MIJI MSIPITE PASIPO KUCHANGIA CHOCHOTE TAFADHALI.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Infantry Soldier 〜 A True Patriot 〜
Aliwatetea Mabeberu baada ya kuona maji yamezidi Unga yakaja kuomba radhi kwa Rais Magufuli.
 
Mkuu, yaaani una maanisha hewa safi sio hitaji la muhimu?
Hewa safi ni muhimu sawa!! pia jua kuwa TZ hatuna na maviwanda meeengi kiivo ya kuchafua mazingira yetu km nchi zilizoendelea kiviwanda siasa na uchumi mfano nchi km Canada, Usa, Russia, Japani nk. kuanzia leo jua kuwa tuna hewa safi!

Kujipendekeza kutunza Mazingira yetu ambayo si chafuzi kiasi hicho na wakati huo huo huna dawa Hospitalini, Elimu duni, Ulinzi dhaifu,Uelewa mdogo wa unachokifanya ni matumizi mabaya ya akili, tena hatari kuliko hatari yenyewe na adhabu yake ni kifo kwa wahusika wote!! wanyongwe mpaka wafe!!

Hatukatai kuiga mazuri ya kufanya kutoka kwa wenzetu but na hili nalo tuige yaani learning blindingly tu jamani hee? fikirieni some times what are you doin!! where! for what benefit, je kutunza mazingira wakati kina Mama wajawazito wanakufa ni akili nzuri?

Hayo mazingira unataka nani ayaishi endapo watu wanao stahili kuyaishi wanakufa kwa kukosa tiba murua Mahospitalini? au ni ili upate sifa tu baasi kuwa TZ tumetunza mazingira sana !!

Sisi km taifa Huru lenye nguvu Africa na Duniani tuna vipaumbele vyetu ni
kipi kianze kwanza na kipi kiwe cha mwisho pia

lini kianze? na kwa nini kianze?

je ni kitakuwa endelevu?

km siyo kwa nini?

na tufanyeje?

Hatulipuki km moto wa kifuuu tuna akili sana siyo kwa sababu ni waafrica tu, mna tuburuza tu mnavotaka tena kwa kutumia waafrica haohao!! weee! rudi kawaelezee hao! haya ma jamaa ni moto.

ukiangalia na kupima kwa kina tena vizuri haya ni mawazo ya kuambiwa tu, yaani bila kuchanganya na zako akili utahangaika sana!! siyo kwamba hujui vipaumbele vyetu km watanzani unajua fika! hao wazungu wanakampenia nchi zao! kwa faida zao! na wao ndiyo wamechafua hasa!

Kwa mfano rahisi unao kuhusu wewe!! kule kwenu Kiribho! Kong'enyi! hakuna hewa safi kule? tangu lini kule mazingira yale yaliharibiwa? na nani? na nini kwanza tuanzie hapo! hakuna Barabara nzuri ya rami tangu zama ,

kapo kabarabara kamoja tu kabayaaa!! hako kameharibu mazingira gani?, Hospitali kubwa ya kusaidia kina mama huko Kiribho haijawahi hata kufikiriwa acha kuzungumziwa, hata madaktari wa kawaida huko hawaendagi.

tangu Uhuru wa mama zenu huko Kiribho wanakufa kwa magonjwa mbalimbali husemi. unarukia mazingira majani na miti, wakati imejaa hapo mlimani tangu kuumbwa kwa Dunia hii!

Mgonjwa kupandisha ule Mlima Kwa kutumia miguu kwenda kutafuta huduma mjini ni tabu sana, hata Baiskeli katu haipandishi ule mlima! sijui hata Punda tu hapandi ile milima, rahisi tu! tuanzie hukohuko kwenu ni wapi penye ukame unao hitaji matunzo ya miti sema!!!

Hapo nimegusia Afya ya msingi tu, bado Elimu, Ulinzi wa mali zenu nk, ( mfano hata ukizalisha miti ikafanya mazingira kuwa mazuri inahitaji ulinzi wa mara kwa mara na ulinzi ni fedha je unazo kuendeshea zoezi hili?)

Sasa mleta mada unaacha hayo masuala muhimu unataka kuzalisha miti! na misitu! sujui majani wakati imejaa mlimani kwenu hapo! wala huendi mbali hii nayo akili au? yaani mleta mada umeona miti ndo muhimu kuliko Afya ya uhai wa wazee wenu, watoto mama/Dada zenu?

Ukae hivi hivi na humu humu Jf! manake wale jamaa wa nchini Mara! walivo na hasira wale, ukienda na sera hizi za misitu kimjini mjini hawakawiagi kuwapoteza Mazimaa watu km nyie muraaa!! tutashangaa tu hatukuoni humu!

Angalia Moshi Kwa marefu na mapana yake kijani tupu, isipokuwa sehemu chache sana km hedaru, Himo, parane ndo kidoogo haparidhishi, lkn Arusha, Iringa yoote ile wilolesi yake kote ni usipime misitu ya kijaniii! kuzuriii!

Pima vizuri Mtwara mjini yote ile kuanzia Naryendele mpaka Msimbati sijui Mahulunga kulee kuelekea Msumbiji ni kijani ya kutisha ni uzalishaji tupu wa korosho unaendelea! sasa una taka nini zaidi ya hayo? hizi sera!! unajua
ila umekula cha juu kulee uzunguni wewe si bure!

Angalia Dar yetu yapendeza ya kijaniii usipime OYSTERBAY, ukitia tu mguu Lugalo yetu kutokea Mwenge kijani mpaka mlangoni, kusafiii siku hizi hatukojoi hovyo! km zamani, kisarawe ndo kabisaa chanzo cha mvua kwa Dar,

Mstu wa kisarawe unavutia tangu ukiwa pugu hills! hapajavurugwa, nenda Muhangara kulee pugu juu! ukijani wake ulio sheheni Maembe dodo tena hovyo! utadhani hauko Dar, mazingira zaidi ya hapa ni uchizi! mtuache tulivyo!

Hapo naiweka akiba Mabwe pande forest na kibaha angalia maeneo ya uwanja wa ndg kule miti mingi kusafii! bado maeneo ya IKULU ya nyerere! mawee!!! yooo! wafwaaa!! saa unatakaje?

wazee wetu wamejitahidi sana Bhana! kututunzia mazingira, usijaribu ku under estimate!! hatuna budi kuendeleza! au una lako jambo mbali na kuwasifu wanastahili pongezi kubwa sana. sijakosea! yaani kubwasana na uwaombe samahani hadharani!!

Nyerere, na Jakaya Hoyee! eeee! itikia ....
 
Hewa safi ni muhimu sawa!! pia jua kuwa TZ hatuna na maviwanda meeengi kiivo ya kuchafua mazingira yetu km nchi zilizoendelea kiviwanda siasa na uchumi mfano nchi km Canada, Usa, Russia, Japani nk. kuanzia leo jua kuwa tuna hewa safi!
Global Warming ni changamoto ya dunia nzima mpaka Tanzania au ni kwa nchi zilizoendelea tu kama Russia, USA na Japan?...
 
Global Warming ni changamoto ya dunia nzima mpaka Tanzania au ni kwa nchi zilizoendelea tu kama Russia, USA na Japan?...
Ok! ni suala la Dunia nzima hii haina tatizo!! je sasa swali Mura! chanzo cha tatizo Hasa la global warming ni nini? je ni wenyeji wa kiribho ambao wamesheheni Misitu tele bila hata chembe ya viwanda? tena imewazunguka kwa miaka dahari kwanza ukiwapa slogan km hizi hawata kuelewa kabisaaa! si unajua ware ndg zako walivo watata mura?

Simple logic!!! Usipojua chanzo cha tatizo, haiwezekani kumaliza au kutatua tatizo lako, linalo kukabili utacheza makida makida tu, je unataka watanzania wacheze Muziki wasio uelewa? at least mimi najua! je ndg zako wa kiribho wanajua?

Tulisha piga kelele kitambo sana kwenye vyombo vya kimataifa nani anapaswa kupunguza matumizi yaliyo pitiliza ambayo husababisha Global warming baadhi yao walipinga, na unawajua! sasa hao ndo mwiba kwetu! wewe unakazania wabongo ambao hawahusiki! hata kuyajua!

je una jua kuwa wao waliwahi kutegemea AIR Baloon reflectors ambazo zilipunguza Uharibifu huo wa mazingira kwa asilimia 80? sasa wewe mura unaongelea mazingira ambayo wao waharibifu ndo nambari moja wanajua mbinu mbadala! utaharibu zaidi tulia kwanza kunywa maji!

Sometimes haya majamaa kurya boy yako Right! sasa ona km wewe! Waki kukata mapanga ooh! hawa jamaa wakorofi!! siyo...
si nimekupa mifano ya misitu mbali mbali tena mingi iliyopo Bongo unapoishi? au hutembei mura!

Sasa miti yoote hii upande tena miti ya nini? haya majamaa hayakawii kutuita machizi!! si unajuaga hayana adabu! suala ni kuitunza Vizuri iliyopo tu baasi! liwe zoezi endelevu! ndiyo ungeshauri watu wafanye!

Na huko nchi ulizo zitaja ndiko chanzo cha tatizo kubwa liliko sasa anzia huko kuwaelimisha kwanza!! yaani ujifunze jinsi ya kujua chanzo cha tatizo utalitatua kirahisi sana. sisi huku Bongo Land-TZ tuko vizuri sana tu, unatuonea, tatizo ni hao Cauccasians ! au bado mura hujanierewa?

na mazingira yao ndiyo yameathirika zaidi mfano ni huko kwa miji ya viwanda vingi km Calfonia, Quebec, Wellington, New Delhi, yaani hapa ndo kabisaaa mpaka moshi uko mitaani waziwazi, vitoto vina vikohozi visivyo isha!! Nagasaki nk

Nimekupa mifano hai hapa, km hapo Mnazi mmoja huoni kulivosheheni majani mazuri, maua na miti? unataka uongeze ya nini hapo?! matumizi mabaya ya rasilimali watu ndo kama haya unayotaka huko ni kutupeleka peleka Blindly. please!! waache watanzania wangu wapumue! mimi ndiyo Rais wao!
 
Back
Top Bottom