kuna sehemu inaitwa DAKAWA kule wakimbizi wa South Africa walikuwa wakifanya yao.
nimesoma kule, hao nyoka ni wengi kiasi kipindi cha mvua huwezi maliza kilometa 1 hujakutana nao chini ya 10 -20. sasa leo ndio naona hatari iliyokuwa mbele yangu kipindi hicho. sababu nyoka hawa nilikuwa nawakamata kwa mkono nikiamini hawana sumu. nilikuwa nawakamata nawatia kwenye mfuko mkubwa, ninamaanisha nilikuw nikiingia pembezoni na mifereji mikubwa kipindi cha mvua nawafuatilia kutokana wana uzito flani hivyo wakipita wanaacha trace, nilikuwa nakamata mmpaka moma 100 kwa siku mbili. kuna mzee, alikuwa anakula hawa na nilikuwa nikimuuzia moma mmoja Tsh 200, chatu 5000. nilijifunza kula nyoka kipindi hicho. sasa mmnaposema wana sumu basi nilikuwa ktk hatari kubwa na sikuwahi kuumwa na aina hiyo ya nyoka, lakini nishaumwa na nyoka wengine wengi tu si chini ya mara 7 katika harakati hizo. yaani naposema kama kuna nyoka nilikuwa siwaogopi ni hawa kumbe yana sumu?