Wataalam wa nyoka huyu ni nyoka gani?

Wataalam wa nyoka huyu ni nyoka gani?

Kuna mshikaji wangu alikuwa ameketi mahala kajamaa kakawa keshaanza kunyanyuka ili kurusha sumu. We kama bahati nilitokea nyoka akanigeukia Mimi Cha kushangaza alilala mwenyewe kama dakika Tano hivi nikasema ondoka lol alisepa balaa. Sasa Cha kushangaza sio mara ya kwanza huwa nyoka wakiniona wanalegea na kusepa. Nitashukuru mkinisaidia kwa hili ni kwanini
Hizi ni story unaleta nabii wa uongo.. Nyoka hana masikio [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyu ni puff adder mkuu jamii ya viper ni nyoka mwenye spidi kali sana ya kung'ata Ana meno(fangs) marefu kuliko nyoka wengine meno ambayo yana vitundu vya kupump sumu anapong'ata
Naongezea: Sumu yake hushambulia misuli(Myotoxin). Akikung'ata usipowahi matibabu misuli ya eneo alilong'ata itaanza kuoza taratibu na kadri sumu inavyoenea ndivyo na misuli huendelea kuathirika kwa kuoza. Ukizembea, kama ni mguu basi itabidi mguu ukatwe-hakuna dawa ya misuli iliyooza/kufa. Ila sio nyoka mkorofi na ukiwa mtulivu mnaweza kupishana tu hana shida na mtu ni mpaka aidha umkanyage au umkalie kwa bahati mbaya au awe amejeruhiwa kwa namna moja au nyingine. Harushi/hatemi mate. It is one of the timid (not active) snakes i.e. ni bozibozi, mzubaafu, duwanzi au amekaa kilegelege.
Ni mtamu sana nyama yake kushinda samaki jodari.
 
Naam umemena sahihi mkuu ila hapo kwenye nyama sina hakika
 
Akikuuma huyu hana dawa japo haui hapohapo dawa ya haraka ni kukata mguu. Yaan upo porini akikugonga mguu unaanza kuoza hapo hapo kadri sumu inapanda mguu unaoza kila inapopita mpaka unakufa
Wewe kama amekung'ata cha kujitetea ni:
1. Acha kupanic na ufanye yafuatayo e.g. kama ni mkononi na unaweza kufikisha mdomo wako mahali hapo chanja hapo na kamua kwa kuchua au nyonya kwa nguvu ili damu yote na sumu iliyoko mahali hapo itoke. Tahadhari Usiwe na kidonda mdomoni.
Osha kidonda hicho kwa mkojo wako au hata wa mwenzio (Utacheka na kudharau kwa sasa, lakini ndg. ukipatwa nakuhakikishia utaomba huo mkojo na hata kunywa utakunywa- ujeuri na kejeli zote huishaga)
2.Kama ni mguuni(Na hili eneo ndo mara nyingi hung'atwa) funga kamba au kitambaa kuzuia damu isisambaze sumu. Chanja hapo na weka jiwe la nyoka/sumu. Kama huna saga mkaa uwe unga mlaini halafu fungia hapo kwenye kidonda bila kuuloweka na maji i.e. tengeneza kimfuko cha nguo kuweka huo mkaa uliosagwa ndipo ukibandike/ukifungie hapo kwenye kidonda. (ww umevaa nguo kwa hiyo sitegemei kuulizwa eti porini ntatengenezaje kimfuko cha nguo)
## 3. Wahi Hospitali iliyo karibu kwa msaada zaidi. Kama Hospitali haiko karibu/huwezi kufika haraka, tafuta Atropine sulphate (maduka ya madawa) Lakini cku hizi kila mahali boda zipo.
NB: Yapo madawa ya Mitishamba/Asili ila kwa bahati mbaya mm siyajui - ngoja watakuja wazoefu zaidi)
 
Puff adder..tena dodoma wako wengi sana hasa maeneo ya Udom na kuelekea ng'ong'onha
Walinunuliwa na kupandwa maeneo hayo ili kupambana na panya waharibifu wa karanga enzi za "The great Kongwa groundnut Project"
 
Kuna mshikaji wangu alikuwa ameketi mahala kajamaa kakawa keshaanza kunyanyuka ili kurusha sumu. We kama bahati nilitokea nyoka akanigeukia Mimi Cha kushangaza alilala mwenyewe kama dakika Tano hivi nikasema ondoka lol alisepa balaa. Sasa Cha kushangaza sio mara ya kwanza huwa nyoka wakiniona wanalegea na kusepa. Nitashukuru mkinisaidia kwa hili ni kwanini
Utakua umechanjiwa dawa..uliza kwenu watakuambia
 
Puff Adder huyo waswahili wanaita kifutu mara nyingi usiku ndo utawakuta njiani... ni mzembe mzembe haumi ovyo ila akiamua kuuma anaweza kugonga mara nyingi bila kuacha meno

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Puff adder ni nyoka mmoja hana makuu na binadamu mwendo wake ni wa pole pole sana lakini usiingie katika kumi na nane zake hasa ukimkanyaga sumu yake ni moja ya sumu hatari sana anaye ua kwa haraka .
 
Puff adder ni nyoka mmoja hana makuu na binadamu mwendo wake ni wa pole pole sana lakini usiingie katika kumi na nane zake hasa ukimkanyaga sumu yake ni moja ya sumu hatari sana anaye ua kwa haraka .
Haui kwa haraka kivile kwani sumu yake hushambulia misuli(myotoxin) kwa kuiharibu uasili wake au kuiyeyusha. Unaweza kugongwa leo lakini hadi kifo inaweza kuchukua hata siku tatu kutegemeana na eneo alilong'ata. Yani misuli(nyama) huoza kadri sumu inavyoenea.
 
Back
Top Bottom