kali linux
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 2,192
- 5,685
Hello bosses and roses.....
Kuna muda nilikua napata sana maumivu ya kichwa ila hospitali hawakunipa majibu yoyote ya kunisaidia. Hii ikafanya nitafute dawa tu ambayo itakua inanituliza maumivu ya kichwa yakianza. Nilijaribu panadol ikafeli, dawa tatu ikafeli. Nikaja kujaribu hizi 'Action' aiseee hii ilikubali na haichukui muda sana kukutibu.
Hivyo nikawa natumia action kwa muda mrefu sababu kila mara kichwa kikiuma tu nakunywa action zangu. Na huwa nakua nazo mfukoni mara nyingi sana.
Sasa kilichonifanya kuandika huu uzi ni hii issue nlogundua kama mwaka mmoja hivi umepita. Unajua action ukimeza huwa inakata usingizi, sasa siku moja nlikua nahitaji kukesha lakini nipo sehemu ambayo siwezi pata coffee na usingizi kama vile ulikua unanizidia, nikaamua kubugia action zangu 2 chap. Ndani ya nusu saa nikawa mpya kabisa, full focused, usingizi wote ukaisha. Kuanzia hapo nikawa nikikosa coffee basi natumia action.
Baadae nikaja kugundua, dakika kadhaa baada ya 'Action' kunikatia usingizi inanipa pia relaxation ya ajabu kinoma. Hii relaxation sijawahi kuipata hata kwenye pombe yoyote nlowahi kunywa. Hii relaxation haina ulevi lakini inakuchangamsha balaa na unakua na amani kwenye ubongo (sio amani moyoni, amani kwenye ubongo) yaan unahisi ubongo ndo mpya, kama vile umefanyiwa servicing fln hivi. Hii relaxation inakaa kati ya nusu saa hadi saa moja kisha inapotea.
Nimefanya udadisi sana hadi kutafuta uhusiano wa kiformula kati ya hii Dawa ya 'Action' na mavitu kama Ecstasy na stimulants nyinginezo lakini kwa upeo wangu sikuona uhusiano wowote kiformula labda kwa sababu nilikimbia Organic/Inorganic chemistry kule Mzumbe boys. Nilichokiona ni kwamba Dawa ya Action ina caffeine, ambayo pia hukutwa kwenye kahawa (coffee) na hapa nilipata jibu la kwa nini Action inaweza kukata usingizi kama ilivyo coffee, ila jibu la hio relaxation bado sijapata sababu huwezi sema relaxation hio inaletwa na caffeine kwana hata kahawa (coffee) ina hio caffeine ila hainiletei aina hio ya relaxation.
NOTE: Nimeleta hapa ili wataalam watoe muongozo lakini tafadhali msijaribu ku-abuse hizi dawa sababu huwa inabadili mapigo ya moyo, unakua ghafla mapigo yanapaa tu bila sababu yoyote.