Wataalamu naomba msaada hapa, nina Gono sugu isiyosikia Antibiotics

Wataalamu naomba msaada hapa, nina Gono sugu isiyosikia Antibiotics

Habari za Harakat za Maisha Wana forum.

Mimi ni kijana Nina miaka 32.
Nimeugua UTI mara moja last year mwezi nov, baada ya kutumia mlango wa nyuma....
Nikaenda hospital nikapewa flucamox na metronidazole siku tano nikapona.

3 months ago nimekutana tena na demu yuleyule, nikapiga kawaida Tu bila mpira..... Nikaikasirisha mizimu....

Nikajua ni Ile UTI tena imerudi, nimekunya flucamox mara 2, bila nafuu....
Nikaenda zahanati nimepewa Augmentin cluvamate nikapata nafuu kidogo tatizo bado linarud....

Nikaenda hospital agakhan kigamboni, wakanambia kwenywe vipimo mkojo uko Sawa Ila Kwa maumivu ya pumbu na uume pia kutoa semen yenye maji mepesi ya maziwa ni STD ambayo ni gono...

Nikapewa Ceftriaxone injection 1g
Doxycycline 2/siku 10
Metronidazole 400mg/siku 10
Nikapata nafuu kipindi natumia dawa siku ya kumi Tu maumivi makali Sana kwenywe uume na chini ya kitovu, mkojo hauumi nikikojoa.... Usaha mara moja sana Hadi mwishon mkojo nikojoa ndio naweza uona. Nikipekenywe urethra naona kama vidonda ivi au ulcers....
Napata maumivu makali Sana nikaa au nikilala...

Nimetumia antibiotics for 3 consecutive months Hadi mdomoni nimepata candida..
Nikajua hapa basi nishaukwaa...

Nimeenda kupima hiv imetoka -ve, Dr kanambia kama nilimnyonya mate na yeye alinyonya uume basi ndio nimepata fangus mdomoni... Sometimes nameza Kwa shida Sana....

Nikachoma pesa kwenda Agakhan Ocean road, nimefanaya vipimo vya uroflowmetry, urinalysis, na ultrasound... Mtaalamu WA urology akasema Nina prostatitis..

Nimepewa Lomefloxacin 400mg siku 14, Alfuzosin siku 14 na aceclofenac...
Problem ni Kua hizi dawa zinanizingua Sana.

Nikaenda hospital tena Jana kisiwani kufanya kipimo cha HIV na damu, HIV sina ni negtv, Ila kwenywe damu Dr kasema bado kuna STD... Pia fungus mdomoni...
Kaniandikia
Cefixime 400mg PO 1*1/5
Ceftriaxone 2g injection
Azitromycin 1g PO stat
Fluconazole 150mg/10 days Kwa ajili ya fungus

Leo nipo siku ya pili naendelea na dozi, (dawa za prostatitis nimeziacha Kwanza nimalize gono)

Swali
1. je nikawaida Kwa gono kutoka usaha WA maziwa mepesi mara moja moja na pia kwenywe semen Kua na kama maji maji ya maziwa.

2. Ni kawaida kuwa na maumivu makali ukikaa au kulala ukiwa na gono,
Mkuu pole kwa maradhi yako ya gono sugu nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia kwa dawa zangu upate kupona maradhi yako uguwa pole.
 
Utapona tu,ila ukome kufanya ngono kipumbavu.Pia mpigie simu huyo mwanamke na yeye akajitibu na yeye awapigie wote aliotembea nao na wao wawapigie waliotembea nao.Mweh ni vicious cycle. Get well soon. Hivi inatokeaje mtu unafanya ngono zembe ?Kwangu mimi utajiri number moja ni afya njema.Kamwe siwezi kufanya ngono hovyo hovyo na watu wa hovyo.
Watu wasio wa hovyo ndio wataokupa STD,s.....trust me sisi watu wazima tumeyaona
Sometimes hoe,s and player,s are better option to ride with!!
 
Mkuu unajua hata unaposema STI unamaanisha nini?
Unamaanisha Syndromic Approach ya Treatment ya UDS/GUD (Ulcers Disease Syndrome/Genital ulcers) sio STIs..?

Unayosema yote nayajua! Nimeanza kufanya kazi Tangu tunadunga sindano (Kuchoma sindano zilizochemshwa kwanza kabla ya kuchoma mwingine)

Mpaka sasa mnachoma sindano..

Unajua Hata kwanini Kuna syndromic Approach (Ukishapima ugonjwa huwezi tena kuuita STIs wala Syndrome)

Utauita kwa jina lake mfano kama ulivyosema Syphilis na matibabu ya syphilis hayawezi kuwa syndromic ...yanafahamika kwa Dx yake..

Nafunga mjadala Huu sidhani kama nitajb

proffesionalism na ethically kama una matibabu mazuri unaweza ukashare na sisi bila kuweka mabishano yoyote kila siku kunafanyika research nyingi sana za magonjwa so Mabishano haya kwangu hayana Afya kwa Matibabu ya Mgonjwa...

Ciao
Mkuu, me nadhani haujamuelewa mwenzako. Hapa habishani, bali ni professionalism discussion. Hata wewe pia unajifunza, na wala haupotezi muda.

Wengi tunafaidika sana na discussion hizi za nyie wataalam wetu, hata kama hatuna professions hizo zenu. Jukwaa la jf ni ufunguo wa maarifa, wekeni mambo bayana, hata wale wa chini yenu (medical assistants) huenda wakaambulia kitu!

Umekomalia ethics; hizo ndio siasa zenyewe! Hivi kweli watu wasidiscuss mambo yanayohusu afya au taaluma fulani eti kwa ajili ya kukumbatia ethics ambapo matokeo yake watu waendelee kuwa wajinga? Nadhani ethics considerations ziwe na limit, sio watu waache kudiscuss mambo ya maana kwa kuogopa kwenda against ethics!

Tuleteeni mautalamu yenu hayo ili na sisi wengine angalau hata tunusenuse tu harufu ya huko kwenu; maana hatuwezi kufika huko! Namshukuru pia mleta mada (ngonjwa) kwani ninyi wataalamu mngeendelea kubaki tu na haya manondo mnayotushushia hapa. Tupeni utamu, elimu yenu iwe msaada kwa jamii, na jamii yenyewe ndio wana jf!
 
Mkuu, me nadhani haujamuelewa mwenzako. Hapa habishani, bali ni professionalism discussion. Hata wewe pia unajifunza, na wala haupotezi muda.

Wengi tunafaidika sana na discussion hizi za nyie wataalam wetu, hata kama hatuna professions hizo zenu. Jukwaa la jf ni ufunguo wa maarifa, wekeni mambo bayana, hata wale wa chini yenu (medical assistants) huenda wakaambulia kitu!

Umekomalia ethics; hizo ndio siasa zenyewe! Hivi kweli watu wasidiscuss mambo yanayohusu afya au taaluma fulani eti kwa ajili ya kukumbatia ethics ambapo matokeo yake watu waendelee kuwa wajinga? Nadhani ethics considerations ziwe na limit, sio watu waache kudiscuss mambo ya maana kwa kuogopa kwenda against ethics!

Tuleteeni mautalamu yenu hayo ili na sisi wengine angalau hata tunusenuse tu harufu ya huko kwenu; maana hatuwezi kufika huko! Namshukuru pia mleta mada (ngonjwa) kwani ninyi wataalamu mngeendelea kubaki tu na haya manondo mnayotushushia hapa. Tupeni utamu, elimu yenu iwe msaada kwa jamii, na jamii yenyewe ndio wana jf!
Mkuu nashukuru Na nimependa Sana wallah ..
😀😀
Ila hapo kwenye Ethics nimecheka huwezi amin8 nimefurah mno..

Lakini Ethics ndo zinamfanya daktari aaminiwe hata na watu immagine umpate daktar li unamwambia siri zako afu kesho unakuta kayamwaga mtaani yote 😄😄

Watu wanajua mpaka doa lililopo sirini liko wapi..

Yeah Discusion ni nzuri sana niliipenda kwakweli na tulipokuwa tunafnya discussion nikagundia pia kuna Matatizo mengine hata mgonjwa kayaficha pia ....

Shukrani sana mkuu
 
Rudi tena mkuu hospitalini upate suluhisho la kudumu la hiyo UTI sugu.

Kunywa maji mengi inasaidia sana kiasi fulani ?

DR Mambo Jambo marisi schwein
ajaribu kutumia systemic Alkaliser Solution kunywa kwanza..
KAMA Disodium Hydrogen citrate Liquid (Cital) angalau Mils 20 Mara moja kwa siku kwa siku 7 (Japo inatakiwa ichanganywe na maji angalau 200 mills of water)

Cc: Wagumu Tunadumu
 
Thanks for your time, Kwa kweli limekua ni Jambo kubwa Ila Kwa msaada kama wenu nimepima Mpaka HIV Mpaka SASA najua nipambnae Tu nipone tuendelee na harakat za Maisha,.... Na hata kama nakufa basi Uzi huu uje uwe fundisho Kwa kwetu sote, sababu mim sio Malaya na demu alienipa ndio nilimwamini mno
Mtibu na huyo demu ugonjwa usiendelee kusambaa.
 
Huyo anapima mara kwa mara HIV sababu anauza mechi sana.Ana wanaume wengi na hawezi kupona coz hata akinywa dawa anaenda kukutana nao tena.Piga chini huyo demu. Sababu hata ukimaliza dozi,ukitembea nae tena atakuambukiza.
Demu yeye hawezi kupona? Mbona hafi ?

yani yeye anadunda tu kabeba mi bacteria na mi virus ya STD bila madhara ?

Victoire acha kumnyanyapaa huyo demu based on story ya huyu jamaa... Hatujui hali ya mwanamke na hatujui ugonjwa umetoka kwa nani kati yao...

Cefixime Kuywa 1x2...!! Ila ungechoma Spectinomycin upige na hizo Cefixime 400gm weka na tinidazole 1x2 pia.
achanganye
ACEFIXIME
SPECTINOMYCIN INJECTION
TINIDAZOLE

Mnaenda kumtoboa figo. Kubalini mnabahatisha.

Why not culture sensitivity tests ?????????????
 
Demu hawezi kupona? Mbona hafi ?

Huyo demu yani yeye anadunda tu kabeba mi bacteria na mi virus ya STD bila madhara ?

Victoire acha kumnyanyapaa huyo demu based on story ya huyu jamaa... Hatujui hali ya mwanamke na hatujui ugonjwa umetoka kwa nani kati yao...


achanganye
ACEFIXIME
SPECTINOMYCIN INJECTION
TINIDAZOLE

Mnaenda kumtoboa figo. Kubalini mnabahatisha.

Why not culture sensitivity tests ?????????????
Naisubiri iyo nimeambiwa after 5 days kutoka leo
 
Hivi vipimo vilikuwa na umuhimu gani ilhali culture and sensitivity ingemaliza kazi, na kuleta majibu ya dawa gani sahihi ya kuua hao bakteria uliopata kwa njia ya kujamiiana ( STI)?
Kwann inakuwa ngumu sana kwa mahospitali kufanya kipimo hiki cha culture??
Tatzo ni nini??
Je wanaona kuchelewa au nini hasa?
Maana unaweza kuwa na dalili zote za kaswende lkn ukipima unaambiwa huna hiyo homa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sipo kuelezea matatizo yote hapa...

Huyu mwanamke yeye alishatibiwa.... Ila nilipo mwambia naumwa naona kama anaufahamu huu ugonjwa mim ndio mgen nao.

Mwanamke aliyekuambukiza keshatibiwa, katibiwa na dawa gani ????

Ulipomwambia unaumwa akaonyesha anaujua huu ugonjwa ila wewe ndio mgeni, anaujua unaitwaje ?????

Haupo hapa kueleza matatizo yote, daktari nae ulimwambia hujaenda kumueleza matatizo yote ???????

Demu anaekuachia umsokomeze ukatili kinyume na maumbile kavu kavu na usaha juu anawezaje kukunyima taarifa za matibabu aliotumia akapona, au umekuwa uki repu mtoto wa watu kinyume na maumbile na ni wewe ndio unaambukiza ambukiza hilo li kaswende sugu lako na kesi iko pending...? ndo maana hutaki kugusia chochote cha hali ya demu ??

Next time ukienda hospitali inabidi uonyeshe kwanza Police Form 3 ya ulikopatia hayo majeraha...
 
Mlango wa nyuma!my friend!!

Kunywa maji mengi ukojoe sana!!

Halafu tafuta mizizi ya mlonge au drumstic au moringa oleifera safisha vizuri kata kata chemsha mpaka ichemke kama nusu saa au dakika 45!kunywa chai yake ni Kali Sana kooni kunywa vikonbe viwili vya chai asubuhi na jioni!utahisi KIU ya maji sana kunywa maji ushinde unakojoa kojoa Fanya hivyo Kwa siku tati Hadi saba!Kila siku chemsha mizizi mipya!!!


Najua jogoo atawika sana we piga kazi lakini tumia kondom kuzuia maambukizi mapya!endelea na dozi Hadi siku 7 ziishe!!utanipa mrejesho mkuu!!

mkuu hii dawa ina msaada wowote kwenye suala la nguvu za kiume?
 
Back
Top Bottom