Wataalamu wa China watoa maarifa ya kujikinga na magonjwa kwa wanafunzi wa Zanzibar

Wataalamu wa China watoa maarifa ya kujikinga na magonjwa kwa wanafunzi wa Zanzibar

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
微信图片_20250220134803.png


Kengele ilipolia katika Skuli ya Sekondari ya Simai iliyopo Pemba visiwani Zanzibar, wanafunzi darasani walichangamka wakiwa na hamu kubwa. Wataalamu wa China kutoka timu ya mradi wa kuzuia kichocho walikuwa wamefika kutoa mafunzo maalumu ya afya kuhusu kuzuia kichocho, ugonjwa unaodhoofisha wa vimelea.

Balozi mdogo wa Konseli Kuu ya China visiwani Zanzibar, Li Qianghua alihudhuria darasa hilo na kupongeza urafiki wa jadi uliopo kati ya China na Tanzania pamoja na ushirikiano wao mkubwa na wa kina katika sekta ya afya.

Li alisema China siku zote imekuwa ikijitolea kufanya kazi bega kwa bega na Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea barani Afrika ili kuboresha kiwango cha afya na uchumi wa wananchi kwa pamoja.

Kupitia juhudi za wataalamu hao wa China, anatumai kuwa mara hii elimu ya kiutendaji na yenye mwelekeo wa afya maishani itaweza kuletwa zaidi kwa wanafunzi wa Kisiwani Pemba ili kujikinga na maradhi ya kichocho, ambayo pia inajulikana kama homa ya Katayama inayosababishwa na minyoo inayoitwa schistosomes.

Kiongozi wa kikundi cha wataalamu wa mradi wa kudhibiti ugonjwa wa kichocho Zanzibar Dai Yang alitambulisha mfumo wa maisha, njia za maambukizi na njia za kujikinga na ugonjwa wa kichocho kwa walimu na wanafunzi waliohudhuria.

Akitumia njia rahisi na nyepesi kueleweka, Dai alielezea madhara ya kichocho na jinsi ya kuzuia ugonjwa huu kwa njia za kisayansi.

Dai alisisitiza umuhimu wa vyanzo vya maji safi katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kichocho, akitoa wito kwa kila mtu kutumia vyanzo vya maji safi, kuepuka kucheza kwenye madimbwi na vijito, na kuoga, na kushirikiana ili kuweka mazingira ya skuli yatakayofanya kila mtu awe anaelewa jinsi ya kudhibiti kichocho, na kila mtu ajue jinsi ya kujilinda.

Ili kuwapa wanafunzi wenyeji ufahamu zaidi na wa kina wa kichocho, kikundi cha wataalamu pia kilitayarisha kwa makini video maarufu ya sayansi kuhusu kichocho ambayo kupitia uhuishaji wa wazi na matukio halisi, ilionesha umuhimu wa kudhibiti kichocho.

Walipokuwa wakitazama video hiyo, wanafunzi walionesha udadisi mkubwa, wakisikiliza kwa makini au kuonekana wakifakari kwa kina huku wakiwa wameinamisha vichwa vyao. Wanafunzi walipata uelewa wa kimsingi wa madhara ya kichocho na pia wakaongeza mwamko wao wa kujilinda.

Ili kutathmini kama wameelewa kweli elimu hiyo ya afya na kuchochea shauku ya wanafunzi ya kushiriki, kikundi cha wataalamu kilipanga kipindi cha maswali na majibu ambapo wanafunzi wa eneo hilo walishiriki kikamilifu katika kujibu na kuuliza maswali.

Li aligawanya vifaa vya elimu ya afya, kama vile kalamu za rangi na rula, kwa kila mwanafunzi aliyejibu maswali, na wanafunzi walipopokea zawadi hizo, nyuso zao zilijawa na furaha na bashasha

Kupitia juhudi za wataalamu hao wa China na ushirikishwaji mkubwa wa walimu na wanafunzi wa skuli hiyo, inaaminika kuwa siku za usoni kisiwa cha Pemba kitakuwa sehemu ambayo imeondoa ugonjwa wa kichocho na kuwa na afya njema na bora zaidi.

Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Salum Hamad alisema kuwa njia hiyo ya elimu ya afya imechochea sana ari ya wanafunzi katika kupata maarifa na kuleta maarifa makubwa ya kujikinga na magonjwa kwa vitendo kwa wanafunzi wa skuli hiyo.

Hamad aliwashukuru wataalamu hao wa China na kutarajia shughuli kama hizo zitaendelea kufanyika katika skuli hiyo katika siku zijazo.
 
Back
Top Bottom