Wataalamu wa Jiji vyumba maeneo ya upanga na maeneo jirani vinasomekaje

Wataalamu wa Jiji vyumba maeneo ya upanga na maeneo jirani vinasomekaje

Dodoma leo

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2021
Posts
1,336
Reaction score
1,658
Habri!! Muda si mrefu ninaingia hapo jijini, kuanza Kazi. Kituo cha kazi kipo Upanga, Sasa nauliza wazoefu wa mjini vyumba maeneo hyo vinapatikana kwa sh ngapi?? Mfano chumba na sebule au chumba ambacho ni self au Sio self coz nataka nijue najipangaje wakuu.
Au maeneo jirani na Upanga?!
 
Upanga sio kama kwenu Nyashimo.
Pili upanga zungumzia Apartment na sio chumba.
Kazi yako kama haina maslahi makubwa hela yote utatumia kulipia nyumba.

Mwisho wa siku lazima uangukie magomeni, kinondoni, makumbusho
 
So nitoke mbagala Mpaka upanga Ndugu Sio mbal sana...
Kwa swali hili ndugu yangu nakushauri acha ndoto za mchana. Kumbe unataka uishi Upanga kisa unafanya kazi hapo? Hizo gharama unazokwepa utazilipa mara nne ukiishi Upanga, hakuna huduma za Kiswahili kule kila kitu gharama haijalishi hata mamantilie ambao ni wachache.

Kapange hata Magomeni ndio karibu kabisa na usafiri hausumbui any time. Vyumba vya kutosha na gharama stahimilifu
 
Ukishindwana bei za appartment zinaanzia 400,000 kwa mwezi, tafuta hostel around 100,000 kwa mwezi umeme, maji juu yao ila ndo hostel tena unashare room
 
Back
Top Bottom