Wataalamu wa kigeni wapongeza mfumo wa demokrasia wa China, na kuutaja kuwa ni mfano wa nchi zinazoendelea

Wataalamu wa kigeni wapongeza mfumo wa demokrasia wa China, na kuutaja kuwa ni mfano wa nchi zinazoendelea

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1712624910103.png


Katika siku za karibuni kongamano hilo lililopewa jina la "Jukwaa la Tatu la Kimataifa la Demokrasia: Maadili ya Pamoja ya Binadamu," lilifanyika mjini Beijing. Lengo la kongamano hilo lilikuwa ni kuwaleta pamoja washiriki kutoka nchi za magharibi na nchi za kusini, kujadili kwa njia ya wazi mambo ya pamoja kuhusu demokrasia, na jinsi nchi mbalimbali duniani zinavyoweza kuwa na njia za kipekee kufikia demokrasia.

Kwenye kongamano hilo jumla ya washiri 300 wakiwa ni wanasiasa, wasomi na wataalam kutoka nchi mbalimbali duniani, walitoa mawazo yao kuhusu demokrasia, na kujadili mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa sifa maalum au sifa ya kipekee katika nchi fulani, mazingira fulani na kuwa sehemu muhimu ya demokrasia ya nchi hiyo.

Moja ya mambo ambayo washiriki walikubaliana ni kuwa China imepata mafanikio makubwa katika njia yake ya demokrasia yenye umaalum wa China, kwani njia hiyo siyo tu imeweza kuleta haki na uhuru kwa wachina wote, bali pia imeweza msingi imara ambao umeisaidia China kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Moja kati ya changamoto kubwa iliyopo sasa duniani kuhusu demokrasia, ni kwamba tafsiri ya demokrasia ni ile inayofungamanishwa na mazingira na utamaduni wa nchi za magharibi. Yaani demokrasia ni siasa za ushindani, mwenye nguvu ya uchumi kuwepwa nafasi ya kuongoza, na maslahi ya kiuchumi ndio lengo kuu la kutafuta udhibiti wa dola. Demokrasia ya namna hii ndio imekuwa chanzo cha migogoro katika nchi ambazo hazijafikia kiwango cha maendeleo ya nchi za magharibi, au kiwango cha uvumilivu wa kisiasa cha nchi za magharibi.

Demokrasia ya China mara nyingi inakosolewa na nchi za magharibi, na kupakwa matope kila mara kutokana na ukweli kwamba imeziba mianya ya uingiliaji wa mambo ya ndani ya China, na pia inaweka kipaumbele kwenye mambo ya msingi ya taifa, ikiwa ni pamoja na usalama wa nchi, haki muhimu za wananchi na maendeleo ya wananchi na ya taifa. Ukweli ni kwamba demokrasia ya China imejengwa kwenye msingi wa historia ya China, utamaduni wa China, mahitaji ya China na mazingira ya dunia.

China haijawahi kukosoa demokrasia ya magharibi, na inatambua kuwa demokrasia hiyo inafaa kwa nchi za magharibi. Lakini pia haijawahi kuzihimiza nchi za magharibi au nchi nyingine kufuata mtindo wake wa demokrasia hiyo. Mara nyingi inachosema China ni kuwa kila nchi ichague demokrasia inayoendana na mahitaji yake na mazingira yake.

Washiriki na wanazuoni kutoka Italia, Misri, Malaysia, Thailand, Japan, Uingereza na Pakistan walioalikwa na kutoa hotuba au kuchangia mawazo kuhusu demokrasia, wamepongeza juhudi za China katika kukuza njia ambayo kwa uhakika inafanya kazi vizuri nchini China. Lakini zaidi ya hapo wanaona mfano wa China ni msukumo kwa nchi nyingine zinazoendelea. Kumekuwa na dalili kwamba nchi za dunia ya tatu, na hasa nchi za Afrika, zinapoamua kufuata njia fulani kwa kujiamulia mambo kunakuwa na kila dalili ya kupiga hatua. Lakini inapotokea uingiliaji fulani hasa kutoka kwa baadhi ya mashirika ya kimataifa, mambo yanakwenda mrama.

Pamoja na kuwa wajumbe wa mkutano huo wanakubali kuwa mfumo wa demokrasia ya magharibi unafaa nchi za magharibi, wengi walieleza wasiwasi wao juu ya nchi za magharibi zinazoongozwa na Marekani kutumia demokrasia kama chombo cha kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kufanya kuwa ni njia ya kuzidhibiti nchi zinazokwenda kinyume na matakwa yao, na sio njia ya dhati ya kuhimiza demokrasia katika nchi hizo.
 
Wachina wamekutuma au umejituma mwenyewe?
 
Back
Top Bottom