Wataalamu wa kilimo wa China wachochea maingiliano ya kilimo na kubadili maisha ya vijijini nchini Ethiopia

Wataalamu wa kilimo wa China wachochea maingiliano ya kilimo na kubadili maisha ya vijijini nchini Ethiopia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
vvOQGtihuA3jPgws.png


China na nchi za Afrika zimekuwa na ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, biashara na ushumi, utamaduni, sayansi na teknolojia, kilimo, na sekta nyingine nyingi. Ushirikiano huu umekuwa na manufaa sana kwa nchi za Afrika, kwani zimeweza kupata maendeleo katika sekta husika kutokana na China kuwa tayari kuhamisha teknolojia zake ili kusaidia nchi hizo kujiendeleza kwa njia zinazoendana na mazingira halisi ya nchi husika.

China pia imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia nchi mbalimbali za Afrika kuboresha na kuendeleza sekta ya kilimo, ambayo ni uti wa mgongo wan chi nyingi za Afrika, na hiyo inafanyika kwa kupeleka wataalamu wa kilimo katika nchi husika kwa ajili ya utafiti na kujua mazao ya aina gani yanafaa kwa ardhi ya eneo husika, kutafiti ubora wa mbegu, na hata kuhamisha teknolojia zake bora za kilimo kwa nchi za Afrika.

Kupitia hatua hii, nchi nyingi za Afrika zimeweza kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza mavuno, na hivyo kuongeza kipato cha wakulima na kuboresha maisha yao, na pia kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika pato la jumla la taifa husika.

Asnakech Sitotasw, mkulima kutoka kijiji cha Godino Jitu, mkoa wa Oromia, nchini Ethiopia, anakumbuka siku ngumu wakati shamba lake dogo lilipokuwa linazalisha mazao yasiyotosheleza kwa chakula, lakini leo, kutokana na uungaji mkono wa wataalamu wa kilimo kutoka China, mama huyu wa watoto watano anafurahia maisha yaliyobadilika.

Kijiji hiki anachoishi Sitotaw kimekuwa mfano bora wa uzalishaji na matumaini, kikiwa na bustani zilizoshamiri, bwawa jipya la samaki, mabanda ya kuku, na vitu vingine vingi. Sitotaw anasema, zamani, mavuno yao yalikuwa haba, hasa kutokana na ukosefu wa mbegu zinazotoa mavuno mengi na ujuzi wa ufundi wa kisasa wa kilimo. Amewashukuru wataalamu wa China kwa kumpatia ujuzi uliomwezesha kufanya mabadiliko katika kilimo.

Mwezi Mei, 2024, kundi la nne la wataalamu wa kilimo wa China nchini Ethiopia lilizindua mradi wa uvumbuzi wa miaka mitatu wa kuondokana na umasikini katika kijiji hicho, kwa uratibu na Wizara ya Kilimo ya Ethiopia na serikali ya mkoa wa Oromia. Wataalamu hao walimpatia Sitotaw na wanakijiji wengine mbegu zenye mavuno makubwa, ujuzi muhimu katika kilimo, na mafunzo ya kivitendo.

Mkuu wa timu ya wataalamu wa kilimo ya China, Zhang Shihong anasema, wanapanga kutumia uzoefu wa kuondokana na umasikini wa China katika kijiji hicho kupitia kutambulisha mbegu za ubora wa juu, ufundi wa kisasa wa kilimo, mashine za kilimo na umwagiliaji unaohifadhi maji. Kazi ya timu hii inajumuisha ufugaji, kilimo cha mbogamboga, kilimo cha mazao, na mshine za kilimo, kwa lengo la kuimarisha sekta ya kilimo na usalama wa chakula nchini Ethiopia.

Sitotaw anasema, wataalamu hao walimpatia mafunzo ya njia za kisasa za kilimo, kutoka kilimo cha mbogamboga hadi ufugaji na ufugaji wa samaki nyumbani, na kuongeza kuwa, uungaji mkono wa kina wa wataalamu wa China uimebadili kwa kiasi kikubwa mlo wa familia yake na kuwaongezea kipato, huku akishuhudia mavuno makubwa ya nyanya, vitunguu, mahindi, ngano, na matunda kama papai na parachichi.

Mkulima mwingine aliyefaidika na mafunzo ya teknolojia iliyotambulishwa na timu ya wataalamu wa kilimo kutoka China kijijini hapo ni Abu Negash, ambaye kwa kuungwa mkono na timu hiyo, alitengeneza bwawa la samaki nyuma ya nyumba yake na kupata mbegu zenye mavuno makubwa.Anasema kutokana na msaada huo, kwa sasa wameongeza kidhahiri mavuno yao ikilinganishwa na miaka iliyopita. Pia mkulima huyu kwa sasa ana banda jipya la kuku alilojenga kutokana na ujuzi aliopata kutoka kwa wataalamu wa China, ambao unaunganisha ufugaji, uvuvi, na kilimo.

Naibu msimamizi wa kijiji cha Godino Jitu, Assefa Gudissa, amezungumzia athari chanya ya kazi ya wataalamu hao katika kijiji hicho. Amesema mavuno ya ngano yameongezeka kutoka tani 4.2 mpaka karibu tani 7 kwa eka moja mwaka huu, mafanikio ambayo yametokana na juhudi za kujenga uwezo zilizofanywa na timu hiyo na utoaji wa mbinu bora za kilimo na vifaa muhimu vya kulimia. Pia amezungumzia mchango wa timu hiyo mbali ya kilimo, hususan katika kufanya uratibu na watoaji huduma za mawasiliano ya simu, ambapo wataalamu hao kutoka China walijenga mnara mpya wa mawasiliano kijijini hapo, na kuboresha maingiliano na kuunga mkono maendeleo mapana ya jamii.

Kama alama ya hivi karibuni ya kupanuka kwa ushirikiano wa kilimo kati ya China na Ethiopia, wataalamu kutoka China walitoa msaada wa zaidi ya vifaa 70 vya zana za kilimo kwa kijiji hicho, ikiwemo mashina za kulima na kupanda, trekta, pampu za maji, kifaa cha kutotoa vifaranga, na taa zinazotumia nishati ya jua.
 
Back
Top Bottom