Wataalamu wa marketing kwanini sio Yas pesa ni Mixx by yas?

Wataalamu wa marketing kwanini sio Yas pesa ni Mixx by yas?

Nafikiri mshauri wao upande wa lugha kafeli!, Biashara inatakiwa inapinduka pinduka kufuata watu haswa kwa biashara inayohusu lika zote.
Si hivyo tu hata tamaduni za watu husika inaweza ikachukua baadhi kwa zile zinazofaa! hakukuwa na shida yoyote kuita "Yas pesa" ni rahisi kwa watumiaji wa Tanzania, amasivyo wangeita hata "Yas money" ni rahisi pia kwa mtanzania kueleweka !.

Ningekuwa mi ndo mshauri wao kwenye kikao lazima ningetoa mtu nundu..🤣
Kabisaaa
 
Sijajua kwanini wametumia hilo jina ila watakuwa na maana yao ambayo wameona ni bora zaidi!
 
Kwa hisia zangu. Kumbuka tigo imenunuliwa na kampuni ya Axian pamoja na Fintech zote za kiafrica. Lkn yas sio brand ya tanzania tu ni pamoja na nigeria, senegal, tanzania na nchi zingine 2 hv ambazo nmezisahau zote zinatumia brand ya YAS kama kampuni na MIXX BY YAS kama huduma za kipesa. Nafkr n kwa sababu 2
1. Kuweka usawa wa jina katika nchi zote hii Axian company inafanya kazi
2. Mixx by Yas. Kuonesha ni muungano wa Fintech na Axian
Tenda za kuuziana huwa zinatangazwa wapi?
 
Tigo sasa ni Yas na Tigo Pesa ni Mixx by Yas. Hakutakuwa na mabadiliko yeyote kwenye huduma au bidhaa zetu .

Ujumbe wa Tigo kwa sasa ni Yas , ki branding kwinini isiwe Yas pesa?
Tigopesa itakuwa na owner mwingine na Yas Share holder wengine,hivyo ni biashara
 
Please, Speed up, Elon Musk ahead!
makampuni mengi ya mawasiliano yatauzwa kwa Wala ukoko, Minara yote inaelekea ukingoni.
Mimi sielewi hizi biashara,ilitakiwa local people waweze kununua majority share kupitia Psssf scheme
 
Ilikuwa rahisi kwa hizo nchi nyinginezo kupokea Hilo jina pengine kwa kuwa ilikuwa ni huduma mpya, lakini ukija kwa hapa kwetu lazima iwe ngumu kidogo, kwakuwa huduma hii tayari ilishakuwa maarufu Sana yaani existing service, Tigo tayari walishatengeneza base ya wateja wenye loyalty ya Hali ya juu na huduma hii ya kifedha. Katika marketing tunaamini kubadili misingi ya nguzo za biashara ikiwemo jina la biashara au huduma hupelekea wateja kupoteza nguvu ya ushawishi na mvuto Zaidi katika huduma husika. Mabadiliko hayo yanaweza kupelekea mteja kuhama huduma moja ya kampuni A na kwenda kamuni B.. na hapa ndipo PR's huhitajika zaidi kuongeza awareness kwa wateja wao dhidi ya mabadiliko yaliyofanyika.

Binafsi nashauri wangetumia jina jepesi na fupi Zaidi ili kuzuia mkanganyiko wa wateja ambao wengi wao wanaweza kupotea kwa kukwepa matumiz ya jina jipya lenye asili ya lugha ya kigeni na lenye maana isiyo dhahiri hasa kwa watumiaji Sisi wa chini tusio na elimu ya lugha.
 
Kila kitu. Jielimishe kuhusu acquisition.
Kuna uhusiano gani kati ya kununua kitu na kukibadilisha jina.., ni kama leo mtu anunua brand ya castle lite halafu abadili jina.., inaingia akilini?
 
Jina Yas Ni zuri na tutalizoea tu over the time ila hii Mixx by Yas naona kama haijakaa Poa, Message za Transaction bana its better ije neno Pesa au Bank yani Mpesa, Tigo pesa Airtel Money neno Pesa liwepo ndo ina sound good
 
Ndo kilichobakia. Insingiza hasara kwakuendekeza ukiritimba. Yan mtej unataka huduma unawafuata hadi unachoka. Yan unaweza kuwaza hawakutaki ndugu mteja
TTCL wananishangaza Sana huduma za internet ziko vizuri ila kuja kukufungia utafuatilia hadi uchoke unawaambia utawapa hela ya soda bado wanakataa huwa najiuliza au wametupiwa pepo?
 
Sisi huku mtaani tunaendelea kuita tigo na tigo pesa.
 
Sasa kwanini isiwe VodaPesa badala ya M-Pesa?! Maswali mengine bhana🤔🤔
 
Back
Top Bottom