Habari za mwamko woote.
Heri ya sikukuu ya mapinduzi ya ZNZ hapo 12/1/2018 siku ya Ijumaa (nawapa in advance).
Direct kwenye mada yangu. Naomba wataalamu wa masoko mnisaidie jina la hii baa.
Kuna baa mpya imefunguliwa eneo la Kahama - Buswelu karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela - Mwanza. Jina la Baa hiyo kwa kweli limenichanganya kidogo hivyo nikaona kwa kuwa JF imejaa wataalamu wa kila nyanja basi niwaombe wataalamu wa masoko wanitoe tongo tongo. Baa hiyo mpya, yenye hadhi ya kawaida jina lake ni "USIYEMPENDA LEO KAJA BAR".
Nilijaribu kuvuta picha labda Mgibeon ananipa mwaliko kuwa Nahuja tafadhali nakualika kupata kinywaji pale baa ya Usieyempenda Leo Kaja. Au hata Tantaw anamwalika Shunie, please Shunie karibu sana pale USIYEMPENDA LEO KAJA BAR nina maongezi na wewe.
Ni hayo tu kwa leo. Shikamoo kaka Jiwedogo