Wataalamu wa "Marketing" nitoeni tongo tongo kwa hili jina

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Habari za mwamko woote.

Heri ya sikukuu ya mapinduzi ya ZNZ hapo 12/1/2018 siku ya Ijumaa (nawapa in advance).

Direct kwenye mada yangu. Naomba wataalamu wa masoko mnisaidie jina la hii baa.
Kuna baa mpya imefunguliwa eneo la Kahama - Buswelu karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela - Mwanza. Jina la Baa hiyo kwa kweli limenichanganya kidogo hivyo nikaona kwa kuwa JF imejaa wataalamu wa kila nyanja basi niwaombe wataalamu wa masoko wanitoe tongo tongo. Baa hiyo mpya, yenye hadhi ya kawaida jina lake ni "USIYEMPENDA LEO KAJA BAR".

Nilijaribu kuvuta picha labda Mgibeon ananipa mwaliko kuwa Nahuja tafadhali nakualika kupata kinywaji pale baa ya Usieyempenda Leo Kaja. Au hata Tantaw anamwalika Shunie, please Shunie karibu sana pale USIYEMPENDA LEO KAJA BAR nina maongezi na wewe.

Ni hayo tu kwa leo. Shikamoo kaka Jiwedogo
 
Labda itakuwa ukiwa hapo kwenye hiyo bar adui yako anatokea Mara paaaap ndo maana wanaita usiyempenda Leo kaja
 
[emoji23] [emoji23] ndio sababu unaishi busweru, ivi tusi kama hilo linaweza kutolewa na KE? au mtu aliyelelewa na wazazi wote? Jibu ni hapana..maneno kama hayo hutamkwa na mtoto wa kahaba tu..nataka nikubadili dogo, unasemaje?
Ila kama kuna mtu mwenye ID nyingi hapa JF wewe unaongoza, sasa hadi na hii kumbe ni yako. Umenichafua roho mara mbili nikakutukana nikapigwa BAN hebu niache sitaki kupata BAN mwaka huu 2018.
Kila mara huwa nakuuliza hivi unaweza vipi kukumbuka pass word zooote hizo?
Mwisho kabisa naomba usinichafulie uzi wangu. wewe ni bwe.ge tu kama unavyojua kuweka thread kwa ID yako moja halafu unajijibu wewe mwenyewe kwa ID nyingine. Joseverest yule mwizi wa siku zile wa Avatar yako naona tena ana ID hii hapa.
 
Hata jina lake halina AMANI. Yamjazayo mtu ndio yamtokayo. Jibu umeshapata mkuu...
Umesema kweli dafity. Ndio maana hata viongozi wa dini wanatuasa tusiwe tunawapa watoto majina kama Tabu, Masumbuko, Mashaka na mengineyo ambayo yanaweza kuakisi maisha ya mtoto
 
Najua lengo lako nikutukane ili nipigwe BAN nakupia mwaka huu hunipati ng'oooooo. Kwa kuwa wewe unajua una ID nyingi ukipigwa BAN upande huu unageukia upande mwingine sasa wataka kuniponza mwenye iD moja, hunipati hilo sahau kabisa. kwa mara nyingine nakuonya acha kuniharibia thread yangu. na wala siku block nakuacha hivi hivi.
 
Jirani misele ya vijijini umeanza lini best?
 
Jirani misele ya vijijini umeanza lini best?
Kweli jirani hiyo baa iko nje ya mji halafu wateja wake wengi ni wenyeji wa pale pale Kahama. Eneo ni zuri lakini sasa mmmh! wana mambo yale ya huku kwetu kwetu kijijini
 
Mara paaap nafika Kahama, nakumbuka NAHUJA ni adui yangu namtumia mwaliko wa fasta ili ajue nipo mjini "Njoo hapa USIYEMPENDA KAJA BAR.."
USIYEMPENDA LEO KAJA hahahaha, ila kwa kweli kuna wakati mwingine tunatakiwa kuwa makini na majina ya biashara zetu. hahahahah. habari za asubuhi mtu wa Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…