BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
maji chini ya ardhi zitakazotumika kama mbadala wakati wa kipindi cha ukosefu wa maji katika mikoa ya Dar es
salaam na Pwani.
Hatua hii muhimu ya WRWB ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya kwanza katika kutafuta vyanzo vipya mbadala vya vya maji katika kukabiliana na ukosefu wa mji katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani.
Utekelezaji wa uchimbaji wa visima virefu vya maji mbadala (back up) unatekelezwa na WRWB kwa awamu
mbalimbali katika jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani kama mbadala wa maji hii ni kutokana na kuwepo kwa
vipindi vya ukame jambo ambalo limekuwa likiathiri uvunaji maji katika bonde na kusababisha mgao wa maji
katika maeneo ya Pwani na Dar es salaam.
Aidha, uchimbaji wa awamu ya kwanza unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi June 2026 Kwa mujibu wa mtaalam wa haidrojia kutoka WRWB Omary Kizulwa alisema bodi imeamua kuwatumia wataalamu wake ili kubaini vyanzo vipya vya maji ili kuondoa kero ya maji katika mikoa ya Pwani na Dar es
salam kwa kuchimba visima mbadala vya kuhifadhi maji katika maeneo mbalimbali.
hizi zinatuwezesha kubaini maeneo ambayo yana vyanzo vya maji chini ya ardhi ili tuweze kuchimba visima”
“Visima hivi vitakua kama back up (mbadala) kusaidia kipindi ambapo ukame unapotokea au ambapo hata
ukame hamna viweze kutumika katika kutoa huduma ya maji” alisema.
“Zoezi la utafiti na uchimbaji linaendelea mpaka sasa tumeshafanya utafiti zaidi ya maeneo 40, Maeneo ya
Ruvu Juu, Ruvu chini, Kigamboni , Chamazi, Ubungo, Kinondoni na Mburahati” alisema.
“Tumeshafanya tafiti na tumeshaweka pointi na hivi sasa tunavyozungumza mitambo ipo site inaendelea na
uchimbaji mpaka sasa zaidi ya visima 17 vimeisha chimbwa na baadhi ya visima vimeonesha uwezo
mkubwa kutoa maji na ni maji mazuri, mfano eneo la Mburahati tumechimba kisima kikubwa pale kina uwezo
wa kutoa maji takribani lita elfu 50,000 mpaka 100,000 kwa saa na visima vingine kama Ilala na visima vya huku
Chamazi vina karibia elfu 10,000 mpaka elfu 20,000 na kuendelea”.
Aidha, mtaalam huyo alisema kuwa Tanzania haina uhaba wa maji huku akibainisha kuwa maji chini ya ardhi ni lita bilioni 21 na maji juu ya ardhi ni lita bilioni 105
MRADI WA KIDUNDA
Aligusia pia mradi wa maji wa kimkakati wa Bwawa la Maji Kidunda unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi
bilioni 336 kuwa utasaidia nao kuhifadhi maji ya juu ya ardhi kipindi ambapo kuna ukame Kwa mujibu wa serikali Mradi wa Bwawa la Kidunda ni muhimu kwa kuwa utawezesha kukidhi mahitaji ya maji kwa wananchi wanaotarajiwa kuongezeka na kufikia.
idadi ya watu 11,387,753 ifikapo mwaka 2032, ambapo
mahitaji ya maji yanakadiriwa kufikia zaidi ya lita bilioni
1.028 kwa siku. Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi
kutoka kampuni ya Sino Hydro Corporation ya nchini
China.
Bwawa la Kidunda, litakalokuwa na ujazo wa lita bilioni
190, litawezesha mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini,
yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya lita milioni 466 kwa
siku, kufanya kazi katika majira yote ya mwaka na hivyo
kuondoa upungufu wa maji wakati wa kiangazi.
Mitambo hiyo inahudumia zaidi ya asilimia 80 ya eneo
lote la huduma la DAWASA.
Kwa upande wake wakati wa ziara ya kukagua mradi wa
Kidunda msishoni mwa mwaka jana Waziri wa Maji Juma
Aweso alisema nchi nyingi duniani kwa sasa zinakabiliwa
na changamoto ya ukame inayosababishwa na
mabadiliko ya tabianchi, hali ambayo pia imeanza
kuathiri Tanzania.
Kutokana na hali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliielekeza Wizara
ya Maji kuchukua hatua za haraka na za muda mrefu ili
kukabiliana na changamoto hiyo.
“Wizara ya Maji tuliweka mkakati wa muda mfupi jijini
Dar es Salaam kwa kuchimba visima vitano
vilivyogharimu takribani Shilingi bilioni 23.6, sanjari na
mkakati wa muda mrefu wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda
mkoani Morogoro pamoja na mpango wa kutumia maji
ya Mto Rufiji mkoani Pwani ili kuongeza uzalishaji wa
maji,” alisema
Alisema kwa sasa mahitaji ya maji kwa Jiji la Dar es
Salaam ni takribani lita milioni 534 kwa siku, ilhali
changamoto ya ukame ikiathiri kwa kiasi kikubwa
upatikanaji wa huduma ya maji.